Katika hizo timu kuna watu wa kazi maalum kama ilivyo kwenye mikutano, mijadala ya media, na hafla nyingi za kijamii.
Atakayeingia uwanjani na bendera za CDM na msafara wake ataanzishiwa vagi na “mashabiki” kisha kuzolewa na polisi na kufunguliwa chaji ya kutaka kufanya ugaidi kwenye mechi ya wananchi kulingana na intelijensia makini inayofuatiliwa na jeshi kakamavu - sio kwa kuja na bendera za CDM.
Hii ndio Tanzania ya leo. Ukiwa mshabiki au msemaji mwenye kelele nyingi hakikisha unakuwa upande sahihi - kwa afya yako.