Haya Magari yenye Bendera za CCM yanayoendeshwa bila kufuata sheria wahusika wakanywe

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Mimi ni mkereketwa wa CCM , mfurukutwa kada kindaki ndaki na mwanachama pia, hii tabia ya magari yanayopeperusha bendera za Chama kuendeshwa hovyo hovyo kwa kasi bila kujali sheria za barabarani haipendezi.

Ipo siku italeta balaa na siku sio nyingi.

Mfano majuzi pale gari moja ya kiongozi mkubwa tu wa chama pale moroko ilipita bila kuangalia taa na ingemfumua mlemavu mmoja aliekua akivuka bara bara.

Lile tukio lilinisikitisha mno kwakua chama ndio chenye dhamana ya kusimamia serikali na sio kutumia nafasi hiyo kuvunja sheria.

Tujisahihishe.
 
Wapate ajali wafe idadi ya watu waovu ipungue nchini
 
Mimi ni mkereketwa wa CCM , mfurukutwa kada kindaki ndaki na mwanachama pia, hii tabia ya magari yanayopeperusha bendera za Chama kuendeshwa hovyo hovyo kwa kasi bila kujali sheria za barabarani haipendezi...
Wangemkanyaga wangehamasishana wavae sare na kwenda kutoa pole pamoja na salamu za mama Samia kwa familia, pia familia ingewekewa kabomba ka maji nyumbani pao.
 
Leo kuelekea njia panda ya himo magari yanakimbia polisi wanachukua mpaka lane ya kulia ili magari yanayoenda opposite direction yanatoka barabarani na kusimama. Halafu unaona gari ya kijani!!

So sad!
 
ccm ni mazuzu wamelewa madaraka
 
Aisee tumakinike
 
Kutoa gongo Keko Mwanga ili ifike Kariakoo ni lazima gari inayobeba iwe na bendera ya ccm ili isiguswe na polisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…