Haya majina tusiwape newborn (watoto)

Haya majina tusiwape newborn (watoto)

Nilienda kutembelea shule ya sekondari kata moja barabara ya morogoro iringa kabla hujafika mikumi kuna mtoto albino yuko bright sana akaniambia anaitwa HASARA iliniuma sana.
 
Nilienda kutembelea shule ya sekondari kata moja barabara ya morogoro iringa kabla hujafika mikumi kuna mtoto albino yuko bright sana akaniambia anaitwa HASARA iliniuma sana.
Yaaah lazma iume inaonekana kama alipewa hilo jina kutokana na alivyo so sad. ila majina yanasadifu tabia jaman na maisha halisi ya mtu
 
Mashaka, chausiku, jua kali, shida, masumbuko, nayo huwa yana shida sanaa
 
Kuna mshkaji alioa mdada anaitwa FITINA.
walishaachana rasmi, dada alikuwa anatoa maneno kwake anapitishia kwa mamake na kumalizia kwa mama mkwe
 
Kuna kijiji kimoja kiko barabarani kutoka Mwanza kwenda wilayani Misungwi kinaitwa Ng'ombe!

Najaribu tu kufikiria watu wa kijiji cha Ng'ombe wakiwa ns akili kama ya huyu mnyama watajilaumu?

Kuna kijiji kinaitwa Lupingu (maana yako kupinga au Zuio) huko mkoani Njombe wilayani Ludewa. Hamna kitu kinaletwa hapo kijiji kikapita kiulaini bila kupingwa au kuzuiwa kwanza. Na kwa mara ya kwanza hiki kijiji ndio kilikuwa cha kwanza kupinga utawala wa ccm wilayani humo na kumchagua mgombea wa CUF kwenye nafasi ya udiwani (ikiwa haina ofisi wala balozi wa nyumba kumi wala wanachama zaidi ya mgonbea na wapambe wake wachache).

Haya majina tunayotoa kwa watu na vitu yanaathiri uwepo na ustawi wao!
 
kuna mtoto niliwahi kukutana nae,anitwa "sipendeki".mwengine anaitwa "matatizo".halafu kuna hawa wazazi wenye iman kali wanawapa newborn wao wa kiume majina kama "osama" nk.
 
Kuna mbulula wengi wenye majina mazuri kama Genius, Innocent, Wema and likely, hivyo napinga hoja yako hapa!
 
Masamaki, nyasato, mafuru, nyanchele, nyanyama, nyanjungu, ili kabila liko... Fond of food
 
Hivi kuna watu wanaitwa Mwaka Mbaya na Sura Mbaya?

Halafu, hivi hayo majina kama Tabu, Mawazo, na mengineyo ya hivyo mara nyingi huwa ni ya Waislam eeh, au nimekosea?

Kama ni hivyo huwa najiuliza kwa nini....

Mkuu salam
Nikusaidie kidogo maana mimi ni muislam. Ni hiviiii huwa kuna mambo matatu yanachanganywa kidogo na kuonekana uislam. Kuna "uswahili", "uarabu" na uislam wenyewe. Waswahili na waarabu wana culture zao ambazo bahati mbaya wakizifanya huwa attributed to uislam. Sasa kwa mfano kwa kuwa watu wengi wa coast ni waislam na hupendelea kuita watoto wao kulingana na matukio e.g mwamvua, mwachooni etc basi ni rahisi kuona waislam wanapenda kuita watoto majina haya. Hali kadhalika waarabu wana culture zao. Kiufupi uislam unafundisha kuita watoto majina mazuri yenye meaning nzuri na si vinginevyo.
Angalizo: sina nia ya kuanzisha malumbano ya dini na mtu yoyote nipo jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na urafiki! Asante
 
Ndg wana MM kwa uzoefu nilioupata baada ya kuishi hapa
duniani miongo kadhaa nimegundua kuwa watu wenye majina kama Shida, Tabu, mawazo, siamini, Mwaka mbaya, Sura mbaya, Sikitu, Tatizo na mengine yanayofanana maisha yao huwasumbua sana hivyo
"TUACHE KUWAPA WATOTO MAJINA HAYA" unaweza kutaja na mengine

kufa kunoga na sikudhani pia umeyasahau
 
Siajabu,hikinini,sihuyu,msichoke,lipijema,tukae
 
Back
Top Bottom