Haya majina tusiwape newborn (watoto)

Haya majina tusiwape newborn (watoto)

Hivi kuna watu wanaitwa Mwaka Mbaya na Sura Mbaya?

Halafu, hivi hayo majina kama Tabu, Mawazo, na mengineyo ya hivyo mara nyingi huwa ni ya Waislam eeh, au nimekosea?

Kama ni hivyo huwa najiuliza kwa nini....

cc:faizafoxy
 
Kisaikolojia, majina huwa yanazungumza maneno mengi sana kabla hata mhusika hajazungumza lolote pia jina lina nafasi kubwa ya kuamua hatma ya mwenye jina.
 
Kuna jamaa anaitwa CHAUVUNGU, ni shidaa kila demu akipata anataka akafanye nae mapenzi uvunguni
 
Sio kweli kuna mdada mmoja nilikua nae enzi za utoto anaitwa Chausku na sasa yupo mamtoni anakula bata, sisi ambao majina yetu yanaashiria utajiri RICH tupo majalala hapa bongo!!
 
Pia majina ya kurithi sometimes sio mazuri ukimpa mtoto jina ambalo ni na bibi yake na huyo bibi alikuwa mkorofi basi kuna uwezekano na yeye mtoto akachukua tabia mbaya za huyo bibi
 
Kuna classmates zangu walikuwa wanaitwa Sikitu, Jiulize, Usimalize teh teh..
 
Ndg wana MM kwa uzoefu nilioupata baada ya kuishi hapa
duniani miongo kadhaa nimegundua kuwa watu wenye majina kama Shida, Tabu, mawazo, siamini, Mwaka mbaya, Sura mbaya, Sikitu, Tatizo na mengine yanayofanana maisha yao huwasumbua sana hivyo
"TUACHE KUWAPA WATOTO MAJINA HAYA" unaweza kutaja na mengine

Mwigulu
 
Watu sikuizi wamebadilika sana, majina hayo yamepungua kwa kasi sana baada ya kuibuka majina ya kina Beyonce, Marichui, Ethan, Iyan nk...japo pia yanachukuliwa bila kujua maana
 
Kuna mshkaji alioa mdada anaitwa FITINA.
walishaachana rasmi, dada alikuwa anatoa maneno kwake anapitishia kwa mamake na kumalizia kwa mama mkwe

Majina yanaathiri
Unamwita mtoto shida, basi shida zitamwandama maisha yake yote

Au unamwita mtoto majuto, anaishia kujuta hadi uzeeni


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Badala ya kumuita mtoto shida, tabu masumbuko kwanini usimuite neema, rehema, furaha, shangwe au amani??


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hivi yule mbunge wa chalinze aliyefariki juzi ambae jimbo lake ndo lipo kwenye kampeni za kumsaka mbunge mwingine alikuwa anaitwaje?
 
Hayo majina ni marufuku kwangu hata kama mtoto kazaliwa kwa shida na mateso
 
Majina yote yawe ruksa.

Vinginevyo tutapunguza namna za kuwajua watu vizuri.

Unaweza kukutana na mtu anaitwa jina litakalokusaidia kujua socio-economic background yake.

Do not attempt to slow down some Darwinian dysfunctions with dire Draconian decrees. Dereliction is due.
 
Kisaikolojia, majina huwa yanazungumza maneno mengi sana kabla hata mhusika hajazungumza lolote pia jina lina nafasi kubwa ya kuamua hatma ya mwenye jina.

Kwanini Avater Yako Huyo Baba Amemkumbatia Mtoto Halafu Analia Kwa Machungu??

Just Curious Sir
 
Back
Top Bottom