Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kweli. Mleta mada ameandika kama vile Yanga ndio mara ya Kwanza kubebwa. Kama ni umoja basi ilitakiwa uanze sasa, yaani ukemee maamuzi mabovu yalikufaidisha la sivyo ni unafiki na wengine watafanya hivyo hivyo Kwa timu zaoMtoa mada hatetei ujinga! Isipokuwa anataka mashabiki tuwe na umoja linapokuja jambo linalo haribu taswira ya mpira wetu.
Mbona karibia mashabiki wote wa Yanga wamekiri hiyo penati ilistahili kuwa adhabu ndogo!Sio kweli. Mleta mada ameandika kama vile Yanga ndio mara ya Kwanza kubebwa. Kama ni umoja basi ilitakiwa uanze sasa, yaani ukemee maamuzi mabovu yalikufaidisha la sivyo ni unafiki na wengine watafanya hivyo hivyo Kwa timu zao
Wanafurahia kubebwa, siku wakibebwa na wanaume mmoja Kwa Moja ghetto.
Usiku wa deni hauchelewi, huwa mnafuatilia yasiyowahusu, Sasa sisi tunawaambia Mtibwa wao walete timu tu uwanjani mashabiki na posho za wachezaji wao hilo ni jukumu letu Yanga.Naona leo mmeamka kwa ajili yetu..
Asubuhi yote hii kweli?
TFF wamefeli Sana kwa suala la waamuzi maana haya matukio hata baina ya timu ndogo huwa yanatokea. Waamuzi wapimwe IQ, umakini wa mtu unaendana na IQ.Mbona karibia mashabiki wote wa Yanga wamekiri hiyo penati ilistahili kuwa adhabu ndogo!
Ila nyinyi sasa ndiyo mnakaza shingo na kusema refa amehongwa, na huku mkitambua fika waamuzi wengi wa ligi yetu ni kichomi!
Karibuni Tanzania Club africanUsiku wa deni hauchelewi, huwa mnafuatilia yasiyowahusu, Sasa sisi tunawaambia Mtibwa wao walete timu tu uwanjani mashabiki na posho za wachezaji wao hilo ni jukumu letu Yanga.
Mwaka huu tunataka kuwafundisha fitina ikoje maana mnatuzoea sana.
Wana Yanga kama tulivyokubaliana leo jumapili outing yetu ni kwa Mkapa kupiga kwenye mshono.
Tumeanza na hiliMtoa mada hatetei ujinga! Isipokuwa anataka mashabiki tuwe na umoja linapokuja jambo linalo haribu taswira ya mpira wetu.
Karibuni Tanzania Club african
Sasa kwanni bumbuli na manara walipopaza sauti walifungiwa ma tief efu kuhusina na hawa marefaUmeendeleza tu unafiki kama wale unaowalaumu. Tukio la Jana sio la Kwanza Yanga kufaidika na maamuzi mabovu, na mkiwa mnabebwa mnaleta unafiki na vimada uchwara kama hivi.
Msimu uliopita Yanga ilifaidika na maamuzi mabovu ya kupewa penati ya hovyo dhidi ya Namungo, goli halali la ruvu shooting kukataliwa. Iliwahi kufaidika na goal corner, pia dhidi ya Simba faulo nje ya 18 ilitengwa penati, n.k. na matukio yote hayo mlipiga kimya.
Mimi si shabiki wa Yanga lakini nakuunga mkono Jambo moja, mashabiki na Wachambuzi wa Soka wengi wana mapenzi dundo Kwa timu na siyo Kwa soka. Kwa ujumla wengi ni WASHANGILIAJI na siyo MASHABIKI. Yuko tayari kushangilia lolote hata la haramu. Nataka niongelee Mechi ya Jana Kwanza; wengi wanaongelea tukio la Penati Kwa vile liliifaidisha timu adui yao, lakini hata wachambuzi sijasikia hata mmoja akiongelea kitendo cha Kagoma kumrukia Kibwana kwenye paja na kuhatarisha Afya yake, faulu ambayo ilistahili red card na refa aliiona maana aliwapa Yanga advantage ya mpira wa kutengwa lakini Kagoma aliyejifanya kulala chini Kwa Muda hata hakuonywa achilia mbali hata Kadi ya njano.Nisikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane.
Kwanza ni kiri mimi ni shabiki wa Young Africans(Yanga),baada ya kukosa muda wa kuitazama ile mechi ya Yanga na Geita kwasababu ya ubize niliona ningeangalia marudio au matukio muhimu katika simu yangu!.Kabla hata ya kufika huko,nilianza kuwasikia watu na wadau mbalimbali kijiweni wakizungumza ya kwamba Yanga kapata bao la mkwaju wa Penati ambalo hakustahili kwasababu mchezaji wa Geita ni kweli aliunawa mpira lakini hakuwa ndani ya box ila alikuwa nje ya box,hivyo wakaendelea kupiga kelele kwamba Yanga kabebwa!.
Sikutaka kuamini maneno ya watu wa vijiweni,ilibidi nikae pembeni kisha niingie Instagram kwenye akaunti ya Azam sports ambapo walirudia kwa umakini lile tukio,nilipolitazama kwa umakini ni kweli kabisa nika kiri ya kwamba ile haikuwa penati halali,bali ilipaswa kupigwa faulu nje ya 18.
Sasa kwanini nimeamua kuandika haya?
Mashabiki,wadau na wachambuzi wa mpira nchi hii huwa wanatabia ya kujisahau sana,na kama si kujisahau basi huwa wanatabia ya kuegemea upande mmoja wanao upenda wao kwa maslahi yao na si kwa maslahi ya mpira!.
Mwaka jana timu ya Yanga ndiyo timu iliyoongoza kwa kuitisha press conference za kuwalalamikia hawa marefa wabovu katika ligi yetu,nakumbuka hadi wadau na wachambuzi wapumbavu wakaibabatiza jina la utani "WAZEE WA MALALAMIKO au MALALAMIKO FC".
Wakati Haji Manara na Hassan Bumbuli wakitoa malalamiko kwa vyombo vya habari kama mtakumbuka Shirikisho la Mpira Tanzania(TFF) liliwapiga faini kwa kuwazungumzia marefa kwa kuiminya Yanga na kuyakataa magoli halali ya Fiston Mayele.Wakati Yanga wanapiga kelele kuhusu waamuzi,Mashabiki wa Simba na timu nyingine pamoja na wadau wa mpira wapumbavu wao walikuwa wakinywa energy za Mo na Juisi za Azam huku wakipiga vigelegele na nderemo za kushangilia uharibifu wa soka la Tanzania uletwao na marefa!.
Wakati Yanga akilalamika hakuna aliyelalamika,wakati Yanga akilia alilia mwenyewe pasipo uungwaji mkono,sasa hawahawa marefa wabovu wanapoonyesha ubovu wao kwa kuiadhibu Geita na kuineemesha Yanga,wale wale waliowakejeli Haji Manara na Hassan Bumbuli leo wanalia na kuwalalamikia marefa wale wale ambao waliwasifia msimu uliopita!.Mlipokuwa mkishangilia Yanga kulalamika kuhusu hawa Marefa hampaswi leo kuumia Yanga kupendelewa,Fungeni mabakuli yenu na mtutolee upumbavu wenu!.
Hili suala la marefa lilipaswa wadau wote tuungane kulikemea,haijalishi ni wachambuzi au mashabiki,lilipaswa kukemewa kwa nguvu zote!,Kama mlishindwa kukemea msimu uliopita mkawadhihaki Yanga na kuwacheka leo kinachowaliza ni kitu gani?,kwa hiyo Yanga akiminywa na hawa marefa wabovu kwenu mnafanya sherehe,ila hao hao marefa wabovu wakiwapendelea Yanga mnakuja hapa kulia na kuanza kusema marefa wabovu?.Kama ni maumivu endeleeni kuyapata,sisi hilo halituhusu maana tulipiga sana kelele lakini tukaonekana vichaa!.
Hatutaki timu yeyote ipendelewe au kuonewa na ndiyo maana tuliyapinga haya kwa nguvu zote na tunapolalamika kuhusu marefa huwa hatulalamiki ili kuineemesha timu fulani halafu timu nyingine iumie,huwa tunapiga kelele kupinga upendeleo wa wazi wazi unao onyeshwa na hawa marefa wabovu,sasa wazungu wanasemaga "What goes around comes around".
ACHENI YANGA WACHEKE KWANI NI ZAMU YAO,NYIE MLIPOCHEKA HAKUNA ALIYEWABUGUDHI!.
HITIMISHO
Mkiamua kusema Marefa ni wabovu basi hiyo kauli itumike kwa timu zote na siyo wawe wazuri kwa timu mzipendazo nyinyi halafu wawe wabaya kwa timu mzichukiazo!.
Huwa mnakuja hapa na kauli za REFA NAYE NI BINADAMU, kwani hapa amekuwa Panya?Unatetea ujinga!