Haya mambo ya kipumbavu mmeyalea wenyewe, mnacholalamika ni nini?

Haya mambo ya kipumbavu mmeyalea wenyewe, mnacholalamika ni nini?

Mtoa mada hatetei ujinga! Isipokuwa anataka mashabiki tuwe na umoja linapokuja jambo linalo haribu taswira ya mpira wetu.
Jana niliamzisha mada ya kupinga maamuzi Yale dakika 3 Tu baada ya tukio. Lakini Napo watu waligawanyika kishabiki. Nimekuwa na Tabia ya kuwapinga marefa bila kujali ukubwa wa Mechi. Kuna nyuzi nilianzisha Mechi ya Ihefu v Prison, Singida BS v Mtibwa nk. Marefa wa Tanzania wanajificha kwenye kichaka cha utetezi wa kinafiki wa mashabiki uchwara, lakini tungekemea Kwa pàmoja wangejifunza maana uwezo wao ni wa chini Sana. Florentina Zablon si refa wa kupewa Beji ya FIFA labda kama alipewa Kwa upendeleo wa kijinsia. Mwingine ni Mwandembwa mpaka nimemuanzishia Uzi juzi.
 
Sio kweli. Mleta mada ameandika kama vile Yanga ndio mara ya Kwanza kubebwa. Kama ni umoja basi ilitakiwa uanze sasa, yaani ukemee maamuzi mabovu yalikufaidisha la sivyo ni unafiki na wengine watafanya hivyo hivyo Kwa timu zao
Mimi nimekuwa nikifanya hivyo naanzisha nyuzi za kuwakosoa marefa hata Mechi ndogo lakini napata uungwaji mkono mdogo Sana.
 
Umeendeleza tu unafiki kama wale unaowalaumu. Tukio la Jana sio la Kwanza Yanga kufaidika na maamuzi mabovu, na mkiwa mnabebwa mnaleta unafiki na vimada uchwara kama hivi.
Msimu uliopita Yanga ilifaidika na maamuzi mabovu ya kupewa penati ya hovyo dhidi ya Namungo, goli halali la ruvu shooting kukataliwa. Iliwahi kufaidika na goal corner, pia dhidi ya Simba faulo nje ya 18 ilitengwa penati, n.k. na matukio yote hayo mlipiga kimya.
Nyie mmefaidika mara ngapi na hao marefa? Mbona ulikuwa unakenua tu na kujimwambafai? Wakati yanga wanalalamikia kunyimwa magoli yao si mlikuwa mnasherehekea, leo hii mmepatwa na nini?
 
Kwa yanga kilicho halali kwao ni haramu Kwa wengine ila ni timu inayoongoza Kwa kuharibu ligi ndio maana wanaumbuka kimataifa
 
Nisikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane.


Kwanza ni kiri mimi ni shabiki wa Young Africans(Yanga),baada ya kukosa muda wa kuitazama ile mechi ya Yanga na Geita kwasababu ya ubize niliona ningeangalia marudio au matukio muhimu katika simu yangu!.Kabla hata ya kufika huko,nilianza kuwasikia watu na wadau mbalimbali kijiweni wakizungumza ya kwamba Yanga kapata bao la mkwaju wa Penati ambalo hakustahili kwasababu mchezaji wa Geita ni kweli aliunawa mpira lakini hakuwa ndani ya box ila alikuwa nje ya box,hivyo wakaendelea kupiga kelele kwamba Yanga kabebwa!.

Sikutaka kuamini maneno ya watu wa vijiweni,ilibidi nikae pembeni kisha niingie Instagram kwenye akaunti ya Azam sports ambapo walirudia kwa umakini lile tukio,nilipolitazama kwa umakini ni kweli kabisa nika kiri ya kwamba ile haikuwa penati halali,bali ilipaswa kupigwa faulu nje ya 18.

Sasa kwanini nimeamua kuandika haya?


Mashabiki,wadau na wachambuzi wa mpira nchi hii huwa wanatabia ya kujisahau sana,na kama si kujisahau basi huwa wanatabia ya kuegemea upande mmoja wanao upenda wao kwa maslahi yao na si kwa maslahi ya mpira!.

Mwaka jana timu ya Yanga ndiyo timu iliyoongoza kwa kuitisha press conference za kuwalalamikia hawa marefa wabovu katika ligi yetu,nakumbuka hadi wadau na wachambuzi wapumbavu wakaibabatiza jina la utani "WAZEE WA MALALAMIKO au MALALAMIKO FC".

Wakati Haji Manara na Hassan Bumbuli wakitoa malalamiko kwa vyombo vya habari kama mtakumbuka Shirikisho la Mpira Tanzania(TFF) liliwapiga faini kwa kuwazungumzia marefa kwa kuiminya Yanga na kuyakataa magoli halali ya Fiston Mayele.Wakati Yanga wanapiga kelele kuhusu waamuzi,Mashabiki wa Simba na timu nyingine pamoja na wadau wa mpira wapumbavu wao walikuwa wakinywa energy za Mo na Juisi za Azam huku wakipiga vigelegele na nderemo za kushangilia uharibifu wa soka la Tanzania uletwao na marefa!.

Wakati Yanga akilalamika hakuna aliyelalamika,wakati Yanga akilia alilia mwenyewe pasipo uungwaji mkono,sasa hawahawa marefa wabovu wanapoonyesha ubovu wao kwa kuiadhibu Geita na kuineemesha Yanga,wale wale waliowakejeli Haji Manara na Hassan Bumbuli leo wanalia na kuwalalamikia marefa wale wale ambao waliwasifia msimu uliopita!.Mlipokuwa mkishangilia Yanga kulalamika kuhusu hawa Marefa hampaswi leo kuumia Yanga kupendelewa,Fungeni mabakuli yenu na mtutolee upumbavu wenu!.

Hili suala la marefa lilipaswa wadau wote tuungane kulikemea,haijalishi ni wachambuzi au mashabiki,lilipaswa kukemewa kwa nguvu zote!,Kama mlishindwa kukemea msimu uliopita mkawadhihaki Yanga na kuwacheka leo kinachowaliza ni kitu gani?,kwa hiyo Yanga akiminywa na hawa marefa wabovu kwenu mnafanya sherehe,ila hao hao marefa wabovu wakiwapendelea Yanga mnakuja hapa kulia na kuanza kusema marefa wabovu?.Kama ni maumivu endeleeni kuyapata,sisi hilo halituhusu maana tulipiga sana kelele lakini tukaonekana vichaa!.


Hatutaki timu yeyote ipendelewe au kuonewa na ndiyo maana tuliyapinga haya kwa nguvu zote na tunapolalamika kuhusu marefa huwa hatulalamiki ili kuineemesha timu fulani halafu timu nyingine iumie,huwa tunapiga kelele kupinga upendeleo wa wazi wazi unao onyeshwa na hawa marefa wabovu,sasa wazungu wanasemaga "What goes around comes around".

ACHENI YANGA WACHEKE KWANI NI ZAMU YAO,NYIE MLIPOCHEKA HAKUNA ALIYEWABUGUDHI!.



HITIMISHO


Mkiamua kusema Marefa ni wabovu basi hiyo kauli itumike kwa timu zote na siyo wawe wazuri kwa timu mzipendazo nyinyi halafu wawe wabaya kwa timu mzichukiazo!.
Unbeaten ya propaganda si ya ubora.

Ubora unapimwa kwa kucheza mechi za kimataifa.

Tunajua usipokuwa bora,unaweza kupata tu ushindi kwa nchi hii.Ila kipimo sahihi ni pale utakapocheza mechi za kimataifa.
 
Yanga walilalama kwa makosa yasiyoonekana, wao hawakua na uwezo wa kushinda lakin walitamani kushunda kupitia tension ya wadau, makosa ya sasa yanaonekana na wao wanayafurahia sababu tu yamekua advantage kwao, mda utasema tena tuupe tu nafasi
Tena pamoja na kulalamika sana,bado wao ndio waliokuwa wananufaika kuliko mtu yeyote na makosa ya waamuzi.

Hii timu inadhani ina u special fulani hapa nchini kwa hiyo wanataka kuwa treated tofauti.
Simba wanaminywa mara kadhaa lakini hutasikia wanalalamika hovyo.
Hii mnayosikia sasa,ni tunataka tuwaonenye wazi hizo sifa mnazozitaka za unbeaten ni za uongo si ubora.

Hata timu za nje wameshajua hawawaogopi mtapigwa tu,hamna namna
 
Mtoa mada hatetei ujinga! Isipokuwa anataka mashabiki tuwe na umoja linapokuja jambo linalo haribu taswira ya mpira wetu.
Mnaharibu nyie na viongozi wa timu yenu kwa kuhonga,halafu unataka tuamini ni makosa ya waamuzi pekee?
 
Mbona karibia mashabiki wote wa Yanga wamekiri hiyo penati ilistahili kuwa adhabu ndogo!

Ila nyinyi sasa ndiyo mnakaza shingo na kusema refa amehongwa, na huku mkitambua fika waamuzi wengi wa ligi yetu ni kichomi!
Tuliwaambia mapema kuwa mmejaribu kumhonga Ntibazokiza mkashindwa,na hivyo mkahamia kwa waamuzi.
Tena mliopanga mfunge dk ya 44 kama script ingeenda sawa,ila mlifunga dk ya 46.
Hii ni michezo ya kuigiza
 
Tuliwaambia mapema kuwa mmejaribu kumhonga Ntibazokiza mkashindwa,na hivyo mkahamia kwa waamuzi.
Tena mliopanga mfunge dk ya 44 kama script ingeenda sawa,ila mlifunga dk ya 46.
Hii ni michezo ya kuigiza
Ata goli la Mkude dhidi ya Prison Simba ilitoa Bahasha Kwaiyo Kila mmoja ajivunie Bahasha zake.
 
Tuliwaambia mapema kuwa mmejaribu kumhonga Ntibazokiza mkashindwa,na hivyo mkahamia kwa waamuzi.
Tena mliopanga mfunge dk ya 44 kama script ingeenda sawa,ila mlifunga dk ya 46.
Hii ni michezo ya kuigiza
Kuna game nikiikumbuka nachekaga sana ile ya biashara na makolo kule mara
 
Usiku wa deni hauchelewi, huwa mnafuatilia yasiyowahusu, Sasa sisi tunawaambia Mtibwa wao walete timu tu uwanjani mashabiki na posho za wachezaji wao hilo ni jukumu letu Yanga.

Mwaka huu tunataka kuwafundisha fitina ikoje maana mnatuzoea sana.

Wana Yanga kama tulivyokubaliana leo jumapili outing yetu ni kwa Mkapa kupiga kwenye mshono.
Kuwa shabiki wa mpira tz inahitaji uwe na kiwango cha lami cha upumbavu ndio utainjoy, lakini ukiwa mjinga waweza elimika ukauchukia mpira, keep it up
 
Mwananchi mwenzangu ulieleta huu uzi unajua maana ya mbumbumbu????hapa umepoteza muda tu, mbumbumbu ana akili za kuvukia barabara tu, mbumbumbu fc ndivyo walivyo
 
Kuwa shabiki wa mpira tz inahitaji uwe na kiwango cha lami cha upumbavu ndio utainjoy, lakini ukiwa mjinga waweza elimika ukauchukia mpira, keep it up
Apo wewe upo kundi gani?mjing.a au mpumbav?
 
Tena pamoja na kulalamika sana,bado wao ndio waliokuwa wananufaika kuliko mtu yeyote na makosa ya waamuzi.

Hii timu inadhani ina u special fulani hapa nchini kwa hiyo wanataka kuwa treated tofauti.
Simba wanaminywa mara kadhaa lakini hutasikia wanalalamika hovyo.
Hii mnayosikia sasa,ni tunataka tuwaonenye wazi hizo sifa mnazozitaka za unbeaten ni za uongo si ubora.

Hata timu za nje wameshajua hawawaogopi mtapigwa tu,hamna namna
Simba hailalamiki ww ni shabiki wa kiluvya fc?
 
Back
Top Bottom