Haya mambo yasikie kwa wengine.Huyu dada alitamani ardhi ifunguke Immeze. Leo hii ana Ushuhuda mwingine

Haya mambo yasikie kwa wengine.Huyu dada alitamani ardhi ifunguke Immeze. Leo hii ana Ushuhuda mwingine

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
jana jioni nimetoka ofisini late kidogo tupo moja ya majengo machache marefu sana hapa DSM. basi nimeingia kwenye lift ghorofa ya pili kutoka juu ndani nikamkuta dada mmoja mrembo hasa.ile lift imefunguka tu naingia hivi nakutana naye anamalizia kutoa gesi (kujamba)

kiukweli hali ya mle ndani ilibadilika hasa... ukichukulia lift inavyokuwa mmejifungia.basi nlimwona yule dada akinitizama kwa aibu na huku akitembeza tembeza macho kama mgonjwa wa dege dege.basi nami nikaona ndo sehemu hiyo hiyo ya kumchokoza nikamwuliza "naona leo lunch ilikuwa bab kubwa?" akauliza huku akijizuia kucheka "kwanini?" nikamjibu huku nikimtizama usoni kiuchokozi "naona unatoa tu gesi mdada wa watu, tukifungiwa humu dk 10 mi naweza kufa au kuzimia...." aliangua kicheko na kusema "heeeeehhh ..... we kaka wewe.......yatakushinda...umeajuaje kama ni mimi" yule dada alicheka mpaka machozi yakawa yanamtoka. tumefika chini dada bado anacheka nami nikasema kimoyo moyo simwachii huyu kimwana.

basi nikawa naongozana naye analekea alipo park gari nikasimama naye kumsemesha. alikuwa ananitizama anacheka anafuta machozi sasa alikuwa anacheka kwa uhuru si kwa pozi zile za kisister du. nikaendelea kumsemesha "hicho chakula walichokulisha leo.. kimesababisha utoe gesi ambayo haiendani hata na hadhi na sura yako" akanitizama na kujibu "nyooooo..... kwenye kupuu kuna hadhi.... hebu niache mie niende zangu"

nlicheka kidogo na kumwambia "naitwa H........" huku nikimpa mkono. kiukweli nlimshtukiza so hakupata hata muda wa kudanganya jina kama ni mwenye tabia hizo. akanijibu naye " i am......" basi nikamwambia kesho lunch ipo juu yangu "sitaki tena wakalichafue tumbo lako here is my biz card" akachukua akaweka kwenye pochi yake na kwa uungwana pia akatoa yake akanipa. basi nikamfungulia mlango wa gari lake maana alikuwa amesha unlock... akaingia nikafunga nikaondoka bila hata kugeuka nyuma.

leo hii nimeenda kupata naye mtoto mzuri wa huku posta lunch.alivyo mstaarabu pamoja na mimi kumtoa lunch aligoma nisilipie vinywaji.she paid for drinks. tumepiga stories sana ya jana anasema kila akikumbuka anataka kufa kwa kicheko.binafsi si mtu ninayejua sana kucheka ila hupenda kuona mtu akicheka.so nikajikuta namtizama tu natikisa kichwa. nimepata rafiki katika mazingira ya kijinga sana.

nlikumbuka nami kuna kosa kama hil niliwahi fanya ofisini. nlijisahau nikaona nitoe gesi... hazikupita sekunde dada mmoja mrembo alikuwa amesimama mlangoni ana knock anataka kuingia. nlimwahi haraka sana pale mlangoni nikamwambia anisubiri kidogo kuna kitu nafuata nje then ntamruhusu aingie.nikaenda sehemu kwnza kutulia...then nikarudi ofisini kucheck hali ya hewa ikoje.nikapulizia na air freshener then nikamkaribisha.

usiombe uwe umetoka tu kutoa gesi kwenye lift halafu kuna watu wanaingia wanakukuta wewe...utatamani ushuke haraka sana.... maana kila mtu atajua tu ni wewe umechafua hali ya hewa kwenye lift.
 
sasa ungekuwa wewe dada yangu emmyta ungefanyaje? ungekausha? wakati inaonekana kabisa hali ya hewa imechafuka mle ndani na upo wewe tu... naye aliamua kujitoa ufaham kupunguza noma..baadaye tukawa marafiki tunacheka na kutaniana.

Hahahaaaaaaa. Duuh.

Katika ubora wako kaka ake GuDume. Yaani nimecheka kuanzia mwanzo hadi namaliza kusoma duuh.

Ila huyo mdada ana moyo wake aisee yaani kwa jinsi ulivyombamba bado kapata nguvu ya kukujibu. Lol.
 
Dah Gudume wewe ni noma sana kwa utunzi, lakini kinachonifikirisha ni nini huwa unawaza muda mwingi halafu wewe ni mtu wa aina gani. Maana inawezekana ukawa mtu moja serious tena mwenye heshima zake mbele za watu na ambaye akitoa hoja zinasikilizwa hadi na wazee huko kitaa au ndani ya familia, halafu huku JF unakuwa mtu wa vituko namna hii.
 
ha ha ha.. hapo no comment kwa kweli.

Dah Gudume wewe ni noma sana kwa utunzi, lakini kinachonifikirisha ni nini huwa unawaza muda mwingi halafu wewe ni mtu wa aina gani. Maana inawezekana ukawa mtu moja serious tena mwenye heshima zake mbele za watu na ambaye akitoa hoja zinasikilizwa hadi na wazee huko kitaa au ndani ya familia, halafu huku JF unakuwa mtu wa vituko namna hii.
 
Halaf hua hivyo ukijamba tu peke yako unashangaa mtu anakuja sijui kwanini,
Nakusubiria ukija Mwanza kwenye zile lift pale.......... ntakujambia buuuuuuuuuuuuuuuu
Alafu siku iyo ulee maharage na mchemsho wa sato jumlisha yai la kuchemka [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Hicho kinyambo chake lazima mtu azimiee
 
Hahahahaha umenikumbusha siku niliyonyambaa ushuzi ukapita kwenye papuchi nikasikia tu tetemeko kwenye mashavuuu prprprprppararapararrr

Asikwambie mtu kunyamba ni kitu kingine
Jinga sana wewe[emoji23][emoji23][emoji23]
Mwenzio kakutana nao kwenye lifti
 
Hahahahaha umenikumbusha siku niliyonyambaa ushuzi ukapita kwenye papuchi nikasikia tu tetemeko kwenye mashavuuu prprprprppararapararrr

Asikwambie mtu kunyamba ni kitu kingine
ila wewe mkuu usipotaja papuchi kwenye sentensi zako hujisikii vzr kabisa
hahahhahaha wewe ni nomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Unaweza kuzimia nakwambia kuna siku

Tumekaa kwenye kikao cha familia aiseee kuna mtu akanyambaa niliangua bonge la kichekooo watu wote wakasema mm ndo nimenyamba

Ikabid nikubali tu kuuua sooo
Hahahah
 
Back
Top Bottom