Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Ilipaswa awe yeye sema tu viongozi wetu hawana maono. JK alikuwa na nafasi ya pekee kabisa ya kuacha legacy ya kipekee sana kwa kutupatia katika mpya (kijitabu) ambayo ingeweka mwelekeo mpya wa nchi yetu. Mchakato akauanzisha. Tume ya Warioba. Wananchi wakatoa maoni yao. Bunge la katiba likakaa sijui miezi mingapi. Mabilioni yakatumika. Samia akang'ara. Rasimu nzuri ikapatikana. Kikwete huyu huyu akaenda bungeni na kuikana katika ile ya Warioba. Na mambo yakaishia pale.Bado wanasubiriwa ambao majina yao yataandikwa kwa wino wa dhahabu.
Alijua kuwa kama angeipitisha katiba ile na upepo ule hasimu wa kisiasa wa wakati ule, inawezekana CCM isingechomoka mwaka 2015. Leo hii naye eti anabwabwaja. Alipoteza nafasi nzuri Sana iliyotukuka; na sasa, mbali na mambo mengine machache mazuri, atakumbukwa pia kwa ufisadi uliopitiliza na........
Hata kwenye demokrasia ambako aling'ara sana, bado tu akatia sahihi ile sheria kandamizi ya makosa ya mtandao mbali na sheria hiyo kupingwa karibu na kila mtu.
Legacy hasi...🪣🚮🚮🚮