round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Wiki ya kwanza tu baada ya kurejea Ikulu, Rais wa Marekani Donald Trump aliharakisha usafirishaji wa shehena ya mabomu 1,800 aina ya MK-84, kila moja likiwa na uzito wa tani moja, mabomu hayo yamewasili rasmi Israel siku ya Jumamosi, tarehe 15 Februari 2025 kwenye bandari ya Israel.
Uamuzi huu unaleta mabadiliko makubwa katika mkondo wa diplomasia ya Marekani kuelekea Israel, hasa baada ya mtangulizi wake, Joseph Biden, kuzuia usafirishaji wa silaha hizo.
Wakati wa utawala wa Biden uhusiano kati ya Marekani na Israel ulikuwa umedorora, kulikuwepo uvujishaji wa taarifa nyeti kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran, Biden alikataa kumpokea Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alipowasili Marekani na hata hakuhudhuria hotuba yake katika Bunge la Wawakilishi, ingawa idadi kubwa ya wabunge walihudhuria.
Mabomu ya MK-84 yanajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa uharibifu, yanaweza kupenya hadi inchi 15 za chuma au futi 11 za saruji, na kusababisha mashimo yenye kipenyo cha takriban futi 50 na kina cha futi 36 baada ya kulipuka. Usafirishaji huu unasisitiza uhusiano wa kijeshi ulio imara kati ya Marekani na Israeli na unafanyika katikati ya usitishaji mapigano.
Video inaonyesha mfano