Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mwalimu ndiye alianzisha mbio za Mwenge nchini, nia ikiwa kuenneza upendo na umoja kati ya Mwatanzania.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, 1958 wakati akihutubia kikao cha 35 cha Umoja wa Mataifa na kuyarudia tarehe 22 Oktoba, 1959 wakati akihutubia Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika (LEGCO) alisema.
“Sisi watu wa Tanganyika, tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pamejaa chuki na heshima palipo na dharau”
Maneno haya hata baada ya miongo ni mazito na yanatia tumaini kwa yeyote anayeyasikiliza. Na ndiyo maana tunayaenzi kivitendo hadi leo, tunaenzi fikra zilizo njema za Mwalimu.
Mwalimu Nyerere alizaliwa 13th April 1922, na kufariki 14th October 1999.
Tukio la msiba wa baba wa Taifa nalo lilikuwa kubwa sana kwa nchi hii na sina nia ya kurudia kueleza umuhimu wake.
Sasa leo nimeona hata katika magazeti watu wanatumiana HAPPY NYERERE DAY!
Maoni yangu ni kama ifuatavyo:
1. Kuzima Mwenge ni shughuli nzito na mahsusi kwa makusudi yaliyotarajiwa. Sielewi kwa nini imechanganywa na siku kama hii ya kumkumbuka Mwalimu Nyerere.
2. HAPPY NYERERE DAY iwe siku ya KUZALIWA Mwalimu Nyerere na sio siku ya kumbukumbu ya msiba wa kitaifa.
Tarehe ya 14 October 1999 ni simu ya REMEMBRANCE ya Mwalimu.
Hatuwezi kuwa na Happy Nyerere Day siku ya kumbukumbu ya msiba mzito uliotupata wa Mwalimu.
Wadau naomba tujimwage maoni maana kuchanganya hivi vitu, vizazi vijavyo havitatuelewa.
Nawasilisha!