Haya ndio maboresho ya Mtaala wa Elimu yanayoenda kufanyika Tanzania katika jitihada za kuboresha Elimu

HAYA NDO MABORESHO YA MTAALA WA ELIMU YANAYOENDA KUFANYIKA TANZANIA KATIKA JITIHADA ZA KUBORESHA ELIMU
Habari za mchana WanaJF

Katika kuboresha elimu, Hivi karibuni serikali ilitangaza mabadiliko ya Kisera Na marekebisho ya Mitaala na baadhi ya Sheria ili Elimu iweze kuenda sawa na Sayansi na Technoljia ya Dunia..
u..
Tusione aibu Watanzania maendeleo ni kuiga kwa waliofanikiwa
Hapa Hakuna Tija yeyote bado Siasa mingi We need committed people to implement the programme.
Watanzania wanataka watoto wao wajue kingereza Shule zote ....Hakuna cha Swahili medium wala English Medium.

Kwa nini tutengenezewe makundi? Wengine watanzania rangi na lugha Wengine watanzania lugha Haifai. Wewe need same Tanzanians
Tukikutana tuamue tuongee Kiswahili au kingereza Sio tuongee Kiswahili Kwa vile hatuna namna nyingine Hii haifai

Alafu Siku zote imejulikana watu walioshindwa shule Ndio wanakimbilia ualimu
Ni dhahiri kwamba msipotengeneza mfumo mpya wa kupata waalimu mtakwama tu
Na hili la waalimu linatakiwa kipewe kipaumbele Kwa sababu Ndio wanaupokea huu mfumo mpya So watangulizwe mashuleni kwanza.
Kwa bahati nzuri nimeoa mwalimu So nawaelewa vizuri Vichwa ni vyeupe kabisa.
Serikali itengeneze mpango sahihi wa kumpata mwalimu bora.
 
Si ndo hilo Historia ya Tanzania na Maadili
Kwenye hilo somo hakuta kuwa lolote la kustaajabisha zaidi historia ya kina Nyerere{siasa ya ujamaa na kujitegemea},Mwinyi{Ruksa + Azimio la Zanzibar},Mkapa{Ukweli na Uwazi+ubinafsishaji},Kikwete{Amri mpya,Nguvu mpya na kasi ya ajabu,maisha bora kwa kila mtanzania,kilimo kwanza na BRN},John{Hapa Kazi tu na Tanzania ya V-wonder} na Samia {Kazi iendelee na kuifungua nchi}.
 
Kama ukitazama leo imefikia hatua mwalimu kukagua nywele za wanafunzi wa kike imekua ni kosa kisa hijabu kuingizwa mashuleni ....watakuambia mwanafunzi kuvaa hijabu ni maadili kumbe ni miemko ya itikadi za kidini na maadili ya kidini yanapenyezwa taratibu kwenye serikali

Hivi nywele za mtoto wa Kike wa kibantu kwa Tanzania zinahusiana vipi na elimu yake darasani?
 
Maboresho yanaonekana ni mazuri sana; hongera sana kwa Mh. Waziri na watendaji wengine wote walio chini yake
 
Na hijabu ina husiana vipi na elimu au na uhadilifu ...mbona wana vaa hijabu na ni malaya kupita miaka ambayo walikuwa awavai

Ndugu jibu swali ama Kama hujui sema hujui. Masuala ya hijabu Mimi hayanihusu.

Nimekuuliza kuhusu uhusiano uliopo kati ya nywele kichwani za binti wa kibantu na elimu yake darasani maana shule nyingi sana hasa za Serikali ni sheria kunyoa upara kwa mabinti na wavulana.

Nywele zao kichwani zinazuia vipi wao kuelimishwa darasani?
 
Nani alikuambia ubantu ni hijabu ? Hayo mambo ya hijabu ni mambo ya waisrael na waarabu siyo mambo ya kibantu ....hijabu inatumika kuficha uchafu wa mwanafunzi ...ndiyo maana hata nchi za kiarabu zina anza kuzuia baadhi ya mavazi ya kiislamu .
 
Hebu nenda kaweke chakula tumboni kwanza maana naona ubongo hauchakati taarifa vizuri.

Nakwambia tena hijabu hazinihusu na wala sijazizungumzia.

Nazungumzia nywele za binti wa kibantu kwanini ni sheria kuzinyoa upara awapo shuleni? Zinahusiana vipi na elimu yake darasani?
 
Wewe ndiyo ubongo auchakati taarifa ...nani kazungumzia kunyoa nywele au kutokunyoa ...mimi nimezungumzia ukaguzi wa usafi wa mwanafunzi kama kanyoa vizuri au kasuka vizuri ...kuna mabinti wanaficha viduku kwenye hijabu na minyoo ya kihuni....
 
Hakuna kitu hapo sisiemu nini [emoji117][emoji90][emoji90]tu elimu ya msingi ilitakiwa kuongezwa darasa moja iwe mpaka darasa la 8 ambayo ingekuwa sawa na form 2 ya sasa secondary miaka 4 kisha chuo hiyo secondar zote ziunganishwe .

Primary ibebe hadi kidato cha pili
Secondary ibebe hadi kidato3 cha 6
Hivyo pawe na daraja 3
Hili ni jaribio ambalo linakwenda kufeli tena vibaya sana kwa sababu ni wanasiasa wachache wamejifungia ofisini na kuandaa huu uharo. Hivi hawa viongozi wana laana gani? Kwa nini hawashirikishi wananchi kuanzia ngazi za chini na ikiwezekana wakafanya pilot study? Huwezi kubadili mfumo wa elimu ghafla ghafla namna hii. Inatakiwa maandalizi ya muda.
 
Kwann hawa viongoz bado wanalazimisha watoto wa shule za msingi wajifunze kwa lugha ya kiswahili wkt watt wao wanasoma english mesium school? Badilikeni acheni roho mbaya na ubaguzi wa wazi
 
Na Mwalimu wa shule ya Msingi atapatikanaje? Maana hawa Ndio wanaotumaliza kabisa Wako chini ya kiwango sana Tutafikiaje malengo ya kupata wahitimu bora wa shule za msingi Kama waalimu ni wabovu?
Ili
Nilitegemea kuona Somo la Katiba na Sheria tangu shule ya msingi.

Nonsense
Ili liwaondoe madarakani? Thubutuuuu 😝😝😝😐😐
 
Iko wazi serikali inashauri watu wajiendeleze. Isitoshe mabadiliko yanapokuja yanakuwa na kipindi cha mpito ambalo serikali unasema itakuwa na utaratibu wa walsha na mafunzo kazini kuhakikisha watu wanaendana na mtaala huo. Mfano mzuri ni walimu wa upe, kwa sasa nadhani wanaishia, ko kukishaondoshwa elimu ya cheti inamaana watu hawatosomea tena.
Na Sisi wenye Cheti tunaofundisha msingi tunaenda wapi?
 
1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).

3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa Kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa shule za English medium.

5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa.

11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na
uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
-kilimo na ufugaji
-umakenika
-biashara na ujasiriamali
-sanaa bunifu
-elimu ya michezo
-ufugaji wa nyuki
-uchimbaji wa madini
-urembo

13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
-hisabati
-elimu ya biashara
-kiingereza
-historia ya Tanzania na maadili

15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
-cheti cha amali (NACTVET)

16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.

19. Coding itafundishwa shule ya msingi.

20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.

21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.

25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
-sanaa
-lugha
-muziki
-michezo
-TEHAMA

28. Masomo ya O-level yatakuwa:
-biology
-physics
-chemistry
-history
-geography
-historia ya Tanzania na maadili
-hisabati
-kiswahili
-english
-elimu ya biashara
-utunzaji wa taarifa za fedha
-computer science
-bible knowledge
-elimu ya dini ya kiislamu etc

29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.
31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.
 
Sio mbaya sana
 
Back
Top Bottom