Haya ndio maboresho ya Mtaala wa Elimu yanayoenda kufanyika Tanzania katika jitihada za kuboresha Elimu

Haya ndio maboresho ya Mtaala wa Elimu yanayoenda kufanyika Tanzania katika jitihada za kuboresha Elimu

Ila bado muda wa Elimu yamsingi muda ni mkubwa sana ilitakuwa kuwa miaka saba tuu au nane ! Sijaona mabadiliko yeyote hapa ..ilitakiwa kuanzia la kwanza hadi la nane iwe imecover hadi form four au la kwanza hadi la 10 iwe imecover hadi form six hivyo akitoka hapo ana kwenda chuo au ufundi! Maana yake tungefata mfumo wa Kenya!

Halafu bado tuna shida kwenye lugha ya kufundishia na lugha ya kuwapima watu au kuwasaili ! Nilitegemea Wizara ichukue uamuzi Mgumu kuanza kutumia lugha ya kingereza kufundishia mashuleni halafu kiswahili liwe somo la lazima!

Halafu nilichopenda ni kada ya Ualimu kuchukuliwa kwa Userious mkubwa sana sana. Kwani ni vyema walimu wapatikane kwa kupimwa kama Kada nyingine zozote. Walimu naoa wafanyiwe usaili kama wengine.
hiyo hata marekani hakuna, secondary na high school no lazima,
 
lugha inabaki kama ilivyo sasa. nguvu inramuliwa iwepo kwenye ubora wa walimu na elimu. ila lugha ni kama sasa, govt kiswahili shule za msingi. ila naona kingereza kimepewa kipaumbele
 
Nimeona hapo et Coding..

Nimecheka sana Usiku huu, nani huyo wa kufundisha coding shule ipo Nyanchanyoko ndani ndani huko?

Alafu unakuta alieweka hilo wazo hata kuandika line moja iliyonyooka ya HTML hawezi..

Tuwe serious kidogo mipango mingiii utekelezaji sasa..
 
😂😂
Mkuu Huenda tukafika maana nasikia kwa Olevel na Advance wanaanza mwakani
 
Hamna kitu hapo kwanza kitu kinachodumaza elimu ya nchi hi iwe Haina thamani ni kukumbatia kiswahili

Na sijui Kwa Nini serikali inalazimisha kiswahili ndio iwe lugha ya kufundishia shule ya msingi

Hizo fani zilizowekwa hapo ni upuzi mtupu
Ufundi ambao ulitakiwa ufundishwe shule za msingi na secondary ni

Computer science
Electronics
Electrical
Graphics

Kijana akimaliza shule akiwa na ujuzi wa hivyo vitu Wala hapato taabu mtaani
 
😂😂
Mkuu Huenda tukafika maana nasikia kwa Olevel na Advance wanaanza mwakani
Sio rahisi.. huko Chuoni tu.. na kuna Comp Lab ila wahitimu wengi wanamaliza weupe.. leo hii Sekondari ya Mbagala Charambee ifundishe coding.. waalim wenyewe hawa hawa au wataajir kila shule Mtaalam wa Programming? Ni hectic
 
HAYA NDO MABORESHO YA MTAALA WA ELIMU YANAYOENDA KUFANYIKA TANZANIA KATIKA JITIHADA ZA KUBORESHA ELIMU
Habari za mchana WanaJF

Katika kuboresha elimu, Hivi karibuni serikali ilitangaza mabadiliko ya Kisera Na marekebisho ya Mitaala na baadhi ya Sheria ili Elimu iweze kuenda sawa na Sayansi na Technoljia ya Dunia..

Haya hapa chini ni baadhi ya Maboresho yanayoenda kufanyika Katika Elimu ya Msingi, Elimu ya Secondary, Elimu ya Juu ya Sekondary na Ualimu.

SHULE YA MSINGI
  • Elimu ya Awali itaanza mtoto akiwa na umri wa miaka 5
  • Elimu ya Msingi itakuwa miaka 6 yaani mwisho Darasa la sita tofauti na sasa miaka 7..
  • Kutakuwa na Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la sita kabla ya kuingia Form one (Standard six National Assesment)
  • Mtihani wa Kumaliza Shule ya Msingi Utafutwa na hivyo mwanafunzi atakayeanza Darasa la kwanza atalazimika kusoma mpaka kidato cha nne
  • Masomo ya elimu ya Msingi yatakuwa
    • KKK (kusoma,Kuhesabu na kuandika),
    • Jiografia
    • Kiswahili
    • Sanaa na michezo,
    • Hisabati
    • Sayansi
    • Historia ya Tanzania na Maadili,
    • Dini
    • Kingereza
    • Stadi za kazi...
  • Lugha ya kufundishia au kujifunza itakuwa Kiswahili Huku English ikiwa ni somo kwa Shule za kawaida (Kiswahili medium) na Vivyo hivyo Kiswahili kitakuwa kama Somo kwenye shule ya English medium na English kama lugha ya kufundishia.
  • Kingereza (English) kitafundishwa kuanzia Darasa la kwamza kwa shule za kiswahili na kiswahili kitafundishwa Kuanzia Darasa la kwanza kwa shule za English medium.
  • Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni mfano Kichina, Kifaransa, Kiarabu nk.
  • Maarifa ya Jamii na Uraia na maadili Vitafutwa kwa sababu maudhui yake Yameingia kwenye somo Jipya la Historia ya Tanzania na Maadili.
Ziada ni kuwa Coding itaanza kundishwa shule ya msingi

SHULE ZA UPILI (SECONDARY)
  • Mwanafunzi ataingia kidato cha kwanza mara baada ya kumaliza Darasa la sita na kufanya mtihani wa Kuassesiwa..
  • Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato cha nne ili kumuwezesha kujiajiri au kuajiriwa pindi anapomaliza Shule.
  • Elimu ya Secondary itakuwa na mikondo miwili tu Mkondo wa Amali (ufundi) na mkondo wa masomo ya Jumla (Masomo ya kawaida)
  • Mwanafunzi atachagua mkondo kulingana na uwezo wake na matarajio yake ya baadae..
  • mkondo wa amali utakuwa na Masomo ya ufundi na mfano wake ni kama..
    • Kilimo na ufugaji
    • Umakenika
    • Biashara na ujasiriamali
    • Sanaa na ubunifu
    • Elimu ya michezo
    • Ufugaji wa nyuki
    • uchimbaji wa madini
    • Urembo
  • Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua walau masomo manne (4) ya masomo ya jumla na somo moja kwenye masomo ya Amali..
  • Masomo ya jumla kwa wanafunzi wa amali (Ambayo ni lazma)
    • Hisabati
    • Elimu ya Biashara
    • Kingereza
    • Historia ya Tanzania na maadili..
  • Wahitimu wa Mkondo wa amali watapata vyeti viwili
    • Cheti cha kumaliza elimu ya Msingi (CSEE) kutoka NECTA..
    • Cheti cha mafunzo ya ufundi kutoka NACTVET
  • kila shuke itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia Ubora wa maswala ya ufundi..
  • kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi (masomo amali) hii ni kwa ajili ya ufanisi wa fani zinazotolewa ili iendane na eneo husika kwa ubora wa hali ya juu
  • Somo la Civics Litafutwa na litaunganishwa kwenye Historia ya Tanzania na Maadili.
  • Masomo ya lazma yakakuwa 6 badala ya saba ya sasa..
  • Masomo ya Biology, Geography, yatakuwa masomo ya kuchagua kama ilivyokuwa kwa physics na Chemistry kwa sababu maudhui yake yake yamekuwa kwenye masomo jiographia na sayansi ya shule ya msingi, kwa mfno afya ya jamii, afya ya uzazi na magonjwa ambukizi..nk
  • Michepuo katika elimu ya Olevel imeongezeka kutoka michepuo 4 hadi Tisa michepuo iliyoongezeka ni ..
    • Sanaa
    • Lugha
    • Muziki
    • Michezo
    • TEHAMA
  • Masomo ya Olevel (Ya jumla) yatakuwa.
    • Biology
    • Physics
    • Chemistry
    • History
    • Geography
    • Historia ya Tanzania Na maadili
    • Hisabati
    • Kiswahili
    • English
    • Elimu ya Biashara (Commerce)
    • Utunzaji wa Taarifa za fedha (Book keeping)
    • Computer science
    • ELimu ya Dini (Maarifa ya dini ya kiislamu ,Bible knowledge etc)
  • information and computer studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa computer science (somo limesukwa upya)
ADVANCE (ELIMU YA JUU YA SECONDARY NA UALIMU)
  • General Studies G.S Imefutwa kwa sababu maudhui yake yapo katika somo la Historia ya Tanzania na maadili na somo la Mawasiliano ya kitaaluma
  • Kutanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (Academics communication) Hii ni kwa wote Advance na Ualimu
  • Astashahada (cheti) ya ualimu itafutwa Rasmi kisha kutabaki na diplom ya ualimu katika nyanja zifuatazo(Diploma ya elimu ya awali, Diploma ya elimu ya msingi, Diploma ya Elimu makundi maalumu)
  • Vyuo vilivyokuwa vinatoa Astashahada (Cheti) na stashahada ya elimu kwa ujumla (Diploma isio na specification) vitatumika Kutoa Continuos Proffesional Developmemts (CPD).
  • Walimu Wa sekondari wote Watatakiwa kuwa ni wale walimaliza shahada tu.
  • Na watakaosoma Shahada ya Elimu ni wale tu waliomaliza kidato cha sita na shahada hiyo itasomwa kwa miaka miwili.
Asante...

Haya ni masomo kwa mujibu wa Rasimu Ya Elimuu..
Wadau wa elimu wameshirikishwa katika maamuzi hayo?What we are seeing is the continued destruction of the education system na kuendelea kuingiza katika mitaala maudhui ambayo hayalengi kuboresha ufahamu wa msingi wa mwanafunzi,bali vitu hewa kama sanaa na michezo.

Sababu zinazotolewa za kupunguza madarasa Std.VIII to Std VII na sasa VI ni very flimsy.Mbona wenzetu Kenya na Uganda hawajapunguza,tuseme sisi ndio wajanja zaidi,I don't think think so.

Ukweli ni huu,upo mpango wa NWO wa kuzalisha wajinga kwa kuharibu elimu,ili waendelee kututawala na kuiba rasilimali zetu,na hili ndilo linaloendelea.Ukweli huu unaonekana kwa wahitimu wetu wa shule za msingi,sekendari na vyuo.Literally hawajui kitu,kwa kuwa mfumo wa kufundishia umeharibiwa kabisa,and there are no efforts at all being made to reverse the situation.Instead the destruction continues,as if the destruction that has already been done is not enough.Very sad indeed.

Why has this been possible,hivi sisi wenyewe hatuoni kinachoendelea?Ukweli ni huu,our state machinery is heavily infiltrated by the NWO Cabal,kwa hiyo hao mamluki ndio wanao amua kila kitu.Simply put it our government is "captured."
 
Sio rahisi.. huko Chuoni tu.. na kuna Comp Lab ila wahitimu wengi wanamaliza weupe.. leo hii Sekondari ya Mbagala Charambee ifundishe coding.. waalim wenyewe hawa hawa au wataajir kila shule Mtaalam wa Programming? Ni hectic
😂😂
kuna wakati huwa wanapanga hizi sera kufurahisha ila tuwape muda tuone..
Maana kwa Secondary wanaanza mwakani
 
Wadau wa elimu wameshirikishwa katika maamuzi hayo?What we are seeing is the continued destruction of the education system na kuendelea kuingiza katika mitaala maudhui ambayo hayalengi kuboresha ufahamu wa msingi wa mwanafunzi,bali vitu hewa kama sanaa na michezo.

Sababu zinazotolewa za kupunguza madarasa Std.VIII to Std VII na sasa VI ni very flimsy.Mbona wenzetu Kenya na Uganda hawajapunguza,tuseme sisi ndio wajanja zaidi,I don't think think so.

Ukweli ni huu,upo mpango wa NWO wa kuzalisha wajinga kwa kuharibu elimu,ili waendelee kututawala na kuiba rasilimali zetu,na hili ndilo linaloendelea.Ukweli huu unaonekana kwa wahitimu wetu wa shule za msingi,sekendari na vyuo.Literally hawajui kitu,kwa kuwa mfumo wa kufundishia umeharibiwa kabisa,and there are no efforts at all being made to reverse the situation.Instead the destruction continues,as if the destruction that has already been done is not enough.Very sad indeed.

Why has this been possible,hivi sisi wenyewe hatuoni kinachoendelea?Ukweli ni huu,our state machinery is heavily infiltrated by the NWO Cabal,kwa hiyo hao mamluki ndio wanao amua kila kitu.Simply put it our government is "captured."
Na umesikia implementation inaanza mwakani 2024 kwa Wanaoingia Form one
 
😂😂
kuna wakati huwa wanapanga hizi sera kufurahisha ila tuwape muda tuone..
Maana kwa Secondary wanaanza mwakani
Tuombe uhai..

Tatizo hawakusanyi ushauri kwa Wadau wanaojielewa. Waanzishe online poll pale system ichuje maoni bora na ambayo yapo rated.

Wakae chini na kusuka mikakati kwa phases.. hiyo ni transformation kubwa sana inahitaji muda na kugawa vitu kwa phases mbalimbali..

Najua mpk wanakuj kuimplement Computer language inakuwa sio marketable tena unakuta AI inagonga code fulll kbs ni ww kuingiza proposal yako na AI inakuchapia code..

Sasa hao wanafunzi unawafundisha coding then haina matumizi ki reality.. muda na tech vinasogea havisubiri mtu.
 
Hii elimu ya ufundi itakuwa nadharia? Nafikiria baadhi ya ufundi waliouandika hapo bila vitendo ni bure.
 
Katika vitu ambavyo watunga sera Bado hajatupeleka mbele ni kubaki kutumia lugha ya kufundishia kuwa ni kiswahili, badala ya English
I concur with you! Huu wa kutokuweka bayana lugha ya kufundishia ni upumbavu bado hatotatua tatizo kabisa! Yani bado wana ng’ang’ana na kiswahili lakini ukienda kwenye uhalisia kabisa lugha ya kingereza ndio inatumika mahali pote rasmi kuanzia mashuleni hadi vyuoni bila kusahau kwenye kutoa huduma na pia kwenye usaili!

Huu mtaala ni bure kabisa kama bado lugha ya kufundishia itabaki kiswahili halafu wanafunzi wakifika juu wanaanza kuteswa na kingereza…Huu ni upumbavu tuu…
 
lugha inabaki kama ilivyo sasa. nguvu inramuliwa iwepo kwenye ubora wa walimu na elimu. ila lugha ni kama sasa, govt kiswahili shule za msingi. ila naona kingereza kimepewa kipaumbele
Ni vyema tuchague moja ni lugha gani ya kufundishia na yenye manufaa? Yani kiswahili hiki kinampeleka wapi mwanao? Kina manufaa makubwa zaidi ya kingereza kama tutaendelea kukitumia kufundishia? Kiswahili kina matumizi makubwa kwenye maisha yetu kuliko kingereza? Lugha yetu rasmi kwenye shughuli za serikali kitaifa na kimataifa ni ipi? Na kwanini ni lugha hiyo? Lugha ambayo inatumika kwenye kila shuguli hata tukichangamana na wengine kwanini isiwe lugha ya kufundishia hiyo?
 
Hii nchi ina watunga sera mazuzu na wapumbavu,kwenye huo mtaala Kuna mambo ya kijinga na upumbavu.Nitabainisha machache.

Mosi,Lugha bila kupepesa macho kiingereza kinapaswa kuwa Lugha ya kufundushia kuanzia shule ya msingi,sio kama ilivyo wekwa hapo.

Pili,Dini unafundisha masomo ya dini,mashuleni ili ugundue nini hasa,huu upumbavu wa kuanza kulishana itikadi utakuja kuleta shida uko mbele.

Tatu,Historia ya Tanzania hili SoMo litajaa siasa za hovyo za nchi hii za kusifu viongozi kama miungu watu.
 
Ni vyema tuchague moja ni lugha gani ya kufundishia na yenye manufaa? Yani kiswahili hiki kinampeleka wapi mwanao? Kina manufaa makubwa zaidi ya kingereza kama tutaendelea kukitumia kufundishia? Kiswahili kina matumizi makubwa kwenye maisha yetu kuliko kingereza? Lugha yetu rasmi kwenye shughuli za serikali kitaifa na kimataifa ni ipi? Na kwanini ni lugha hiyo? Lugha ambayo inatumika kwenye kila shuguli hata tukichangamana na wengine kwanini isiwe lugha ya kufundishia hiyo?
Mkuu kiingereza ndio msingi wa maarifa mengi na hii ni kutokana na kuwa na Literatures nyingi,jambo ambalo watu wengi hawafaham ni kwamba kukua kwa Lugha huenda sambamba na kukua kwa mawazo (fikra) kwa sababu fikra mpya au mawazo mapya lazima yapate misamiati ya kukamata hayo mawazo na hapo ndipo Kiswahili kinapo feli,mfano neno Ethics na Moral,katika Kiswahili hupewa maana Sawa kitu ambacho sio Sawa,lakini Kiswahili phone hawalioni hili kama tatizo.
 
Ovyo sana! Kwa maandalizi gani waliyofanya? Hizo elimu za ufundi zinahitaji nyezo, waalimu (wabobezi) wa hizo taaluma.
Tuna walimu wangapi wenye uwezo wa kutosha shule zote?
Hapo sijaelewa kwa kweli!
Hili taifa kila jambo ni siasa mpaka kwenye mambo ya msingi kama elimu,afya nk.shule za kata tu zina miundombinu mibaya na hovyo,sasa mambo ya karakana za kisasa yatawezekana kweli ?

Somo la historia ya Tanzania ilikuwa utashi wa mtu mmoja,lakini watu wamefanya agenda ya watu wote,yaani siasa kwa kila jambo
 
Back
Top Bottom