Haya ndio machimbo ya bidhaa Kariakoo

Haya ndio machimbo ya bidhaa Kariakoo

Nitapata wapi hiki kifaa cha kuulia mbu kwa bei ya jumla
20230731_234249.jpg
 
Anaandika Kelvin kibenje

Wengi mmeuliza kuhusu #vijora na Madera na magauni ya batiki. utayapata Mtaa wa nyamwezi na narungombe lango la kuingilia shimoni jengo la baserona. Namba vijora +255 715 333 880

Hilo jengo pia ndio kuna magauni marefu ya aina zote na Abaya na Hijab. Ukifika panda floor ya kwanza zunguka humo.

Wale mnaotafuta Korosho nendeni soko la Kisutu utapata jumla utawakuta Wamakonde na watu wengine chukua, Brand, uza.

Apples, zabibu na baadhi ya vyakula vya matumizi ya nyumbani kama blueband,sukari, tishu, mafuta ya kupikia hupatikana mtaa wa kiungani na Sikukuu, kiungani na Sukuma

Kwa tisheti kule aggrey majengo muhimu ni pamoja na Miami, Thailand tower na J. H adson karibu na tommy touch.. Hapo pia Kuna maduka ya midoli na henga utapata.

Kama Unataka vifaa vya simu ili ufanye biashara Earphone, waya na kava za simu na screen protector nenda mtaa wa Masasi na msimbazi. ( hii biashara ni nzuti na unaweza anza na mtaji mdogo)

Machimbo ya AC, water DISPensa na mafriji ni NDANDA na MASAS pia LIKOMA NA AGREY.

Duvet, shuka za china na turubai fika kariakoo crdb bank/mkabala Kuna duka la Mchina. Amal house zipo

Wale mnaotengeza content mtandaoni mnaotaka mic za simu, taa za kurekodia (Ring Light) , selfie stick nenda jengo la msimbazi namba +255 655 724 009

Mashuka kama vile (king size,Shuka uganda,Shuka za Nida) Mataulo, Neti Aina zote, Maduvet, Mapazia, Mito, Fimbo za mapazia Ni Mtaa wa mchikichi na Swahilli kwa Big_Man Stores utapata namba yake +255 744 334 554

Kazi imebaki kwako kufanya biashara. Hakikisha una save hii post iki ikusaidie siku Ukihitaji hizi bidhaa au siku ukienda Kariakoo.

Machimbo yote hayo ni uhakika wa bei nzuri na usalama wa kupata mzigo wako.

Kumbuka kwenye group utapata machimbo yote hivyo jiunge leo pia Utajifunza kuagiza china mwenyewe na kupata number za supplier wa china. Kujiunga na group la whatsapp darasa la May Tuma ada yako Tsh 10,000 kwenda 0762815104 kisha tuma message whatsapp kwa namba hiyo hiyo nikuadd kwa group la mafunzo.

Machimbo yamesaidia wengi mno kuanza biashara na kuongeza mauzo kutokana na kupata bidhaa za uhakika bei nzuri.

Part 2
Tunaendelea tulipoishia...
.
Wale mnauliza vifungashio na mifuko mbalimbali Nendeni mtaa wa Tandamti na swahili opposite Na linapojengwa soko jipya.
.
Vifaa vya ushonaji utavipata Makutano ya mtaa wa Nyamwezi na mkunguni
.
Cherehani ni zinapopaki daladala za masaki_gerezani.
.
Vifaa vya kilimo na madawa ya kilimo ni mtaa huo huo wa nyamwezi na mkunguni yapo maduka mengi.
.
Aya, msimu wa Ligi unaanza na jezi zitanunuliwa sana, kuna chimbo ana jezi za timu zote mpaka za saudi. Chimbo liko mtaa wa Narung'ombe na congo. Lipo uchochoro ambapo lipo duka la @welldone_turkish_fashions Huyu welldone yeye ana mashati yale Quality na mimi huchukua hapo.
.
Kona ya Nyamwezi na Pemba utapata maduka ya vitambaa ( fabrics). Pia mtaa wa mkunguni.
.
Makutano ya mtaa wa Narung'ombe na livingstone vifaa vya magari. Mtaa wote huo ni vifaa vya magari. Pia mtaa wa lumumba vifaa vya magari ila zaidi urembo wa magari.
.
Jeans chambuu, Boyfriend jeans zilizo kwenye Fashion na makoti ya jeans SPESHO ni Kariakoo opposite na Bigbon 0767637399
.
Perfume wengi mnauliza fika mtaa wa mkunguni na bonde kariakoo 0719909042
.
Vifaa vyote vya simu ingia mtaa wa likoma na Aggrey, huu mtaa ingia yale maduka ya Ndanindani yale utafurahi.
.
Vyombo vya tani vizito +255 675 092 742
.
Vidani, nakshinakshi, cheni, hereni ingia mtaa wa mchikichi na sikukuu. Unaweza kufika kwa huyu +255718875987
.
Mashuka ya uganda na Duvert utayapata kwa @mam__mashuka__store yuko msimbazi 0717 313 792
.
Wengi pamoja na kuwafundisha kuagiza china wenyewe bado imekua mitihani, aya Wale mnaotaka kuagiza china kupitia Kampuni yetu ya Finbuy sasa unaweza kuagiza tembelea @machimbo_kariakoo_china @finbuy_tz
.
Barabara ya uhuru Jengo la Nhc plot 19/54 hapo kuna godawn kubwa la magodoro
.
Vitambaa vya jora Ndanda na narung'ombe kuna maduka mengi hapo jumla.
.
Unaweza kufika mitaa Hiyo kupata hayo Mahitaji ili kuanza Biashara yako.

Wale wa mikoani ukifika mara moja unaweza kufanya tafiti zako na kupata chimbo sahihi kwako. Ambao hamuwezi kufika tutawasaidia namba za chimbo kupitia groups zetu za whatsapp.
.
Save itakusaidia na share kwa rafiki yako mpambanaji.
.
Chimbo gani unaongeza sahihi? Lipi bado unatafuta.?
.
Machimbo mengine tuendelee Kwenye comments.
[emoji122][emoji2935]
 
Asante sana. Nashukuru pia kwa kutambua Mtoa post.

Machimbo ni msaada kwa wengi hasa kwa wale ambao wanaanza Biashara na wenye mitaji midogo wasioweza kwenda China.
.
Unaweza kupata machimbo zaidi na updates za machimbo kwenye page yangu insta ya jina la @kelvinkibenje link Www.instagram.com/kelvinkibenje
 
Zingeandikwa bei elekezi.

Siyo unafika lale unakuta jinzi elfu 18 sawa sawa na anayeuza mtandaoni
 
Kitu kingine ukitaka kujua chimbo hili ndio la bei nzuri la jumla wahi mapema asubuhi ,duka utakalokuta Lina wateja wengi hasa vijana ndio best zaidi ,pia na maduka ya wachina wako cheap sana. Uzuri wa Kariakoo maduka mengi ya bidhaa zinazofanana yako eneo moja....mtu unayekwenda mara kwa mara kariakoo lazima utaiva na kujua mitaa na maduka yote yako wapi..
 
Mipira jezi na vifaa vya michezo kwa bei rahisi sio yale maduka ambayo ukienda kununua wao wanaenda kuzinguka ndio wanaleta
Therealhamis
 
Back
Top Bottom