Haya ndio machimbo ya bidhaa Kariakoo

Asante ndugu umeshanisaidia nilikuw nahitaji biashara moja umeieleza na kuandika mawasiliano nimeshaongea na mwenye namba bado kumtuma mtu wangu kufuata.
 
Mkuu machimbo ya vigari, visimu, vishada, visimu vimask vya watoto yapo mitaa gani?
 
Naona uzi umepoa. Ngoja nishushe vitu.
.
Unataka Kufanya Biashara ya Vyombo vya plastiki kama viti, meza, vikombe, majagi, mabeseni nk. maduka ya viwanda yapo kariakoo mtaa wa Livingstone na Aggrey mpaka mchikichi na mahiwa close huko utapata kwa bei nzuri na ukiuza utapata faida nzuri.
...
Vyombo vingine utavipata mtaa wa Aggrey na livingstone
.
Maua bandia utayapata mtaa wa Aggrey na sikukuu. Hapo kuna mchina yuko opposite na Bank ya NCBA.
.
Nguo za wanawake kama T_shirt skins, Bwanga, tops, gauni utapata mtaa wa Raha na Muhonda zaidi ingawa maduka ya nguo za wanawake yameganyika mitaa mbalimbali sana.
.
Vijora, Mitandio, Abaya na baibui utavipata mtaa wa nyamwezi na Narung'ombe jengo la Barcelona floor ya pili.
.
Nguo za wanaume kama suit, jeans, Track, shati, T_shirt, kadeti nk utavipata jengo la Mchikichi complex.
.
Shati quality za kiume chimbo ni kwa @welldone_turkish_fashions congo na narung'ombe
.
Pochi kariakoo makutano ya likoma na muhonda
.
Vifungashio kama makopo, chupa, mifuko, mabox ya bidhaa aina zote utapata mtaa wa Tandamti na sikukuu
.
Mnaulizia sana mtumba Grade A kuna marafiki zangu wanaleta mtumba mzuri ambao huwezi kujutia wako ilala Boma
.
Wale wa mtaji mdogo nenda ilala boma saa 11 asubuhi utapata mtumba ata nguo za 1000 ukauze minadani
.
Viatu vya kike vipo mtaa wa congo na narung'ombe, ukienda saa 11 asubuhi utajua machimbo ya wachina maana wengi wanashusha kutoka stoo asubuhi.
.
Viatu Vya kiume vipo Nyamwezi na Narung'ombe. Lakini ukihitaji viatu vya Mtumba hivyo utavipata mtaa wa Karume, nenda pia asubuhi saa 11.
.
Unahitaji Nywele, unahitaji rasta nenda mtaa wa jangwani na mafia. Huko kuna maduka mengi na mawakala wa viwanda vya rasta. Ni ule mtaa zinapopaki Daladala za makumbusho gerezani.
.
Kwa upande wa Vipodozi aina zote pia nenda huu mtaa wa Mafia na Jangwani hapo kuna duka maarufu la @kariakoovipodozi utapata vipodozi.
.
Lakini tusikalili kuna Machimbo mengine hayapo kariakoo ila wanashusha mizigo kwa bei ya chini na kuweka stoo.
.
Turudi kariakoo, mtaa huu wa mchikichi na nyamwezi kuna duka kubwa la vifaa na nguo za watoto wachanga, yaani nguo, mabeseni, matoroli, babyshioo, pot aina zote nk. Hilo jimbo kama una duka la watoto na wajawazito utanishukuru.
.
Mashuka ya uganda nenda kwa mchina opposite na Bank ya Crdb
.
Nguo za ndani Nenda makutano ya mtaa wa mchikichi na sikukuu. Hapo kuna duka kubwa mno utapata nguo za ndani jumla kwa aina zote.
.
Kuna Chimbo Waturuki wana vyombo imara vizuri vya kituruki pia wanakopesha kwa wenye maduka. Ni vizuri hata kwa matumizi binafsi
Chimbo gani lingine unaongeza lipi unatafuta? Endelea kwenye comments
.
Unataka number zao? Sijui kama hapa inaruhusiwa ila instagram kwenye page yangu ya @kelvinkibenje utapata machimbo yote na Number zao
 

Attachments

  • Screenshot_20231012-005812.jpg
    240.5 KB · Views: 82
Chimbo la plumbing material and sanitary ware
 
Chimbo la plumbing material and sanitary ware
nenda gerezani kwa imma ukifika maeneo hayo ndipo hardware zilipo mpaka unakaribia kidongo chekundu zote ni hardware utapata unachotaka hapo
 
Viatu vya kike vipo mtaa wa congo na narung'ombe, ukienda saa 11 asubuhi utajua machimbo ya wachina maana wengi wanashusha kutoka stoo asubuhi.
.
hapa waende mtaa wa narung'ombe ddc frame no 42 ukifika tizama jengo la upande wa pili zimo meza za chinga kama 11 wanaouza jumla kwa kukata kuanzia pc 3,5,6,10 kuendelea kwa wale wenye mtaji mdogo a,mbao hawamudu caton kwa mchina NB ukifika hapo ulizia dada anaitwa sweet manka ama jamaa anaitwa mourinho ndipo pa simpo shoes.
na pia ukitaka kujua wachina wako wapi utaoneshwa pia mfano EXELLENT, MERU.F.S, YOUNG FEY MAUA,SHOWS,LILIDAS,FASHION NK.
 
Mkuu, naomb msaada wa kupata çhimbo la simu (bei ya jumla)
 
Mkuu, naomb msaada wa kupata çhimbo la simu (bei ya jumla)
sawa simu za aina gani hizi za smart ama hizi ndogo zwa viswaswadu au zote. kama upo kariakoo nitafute nikupeleke moja ya duka za jumla pia ujumue mwenyewe255784705349,255674846674
 
Alipokosea utume 10,000 uungwe kwenye group la whatsapp.
Hivi,alipoandika mada hiyo,hakutumia bando lake au muda wake? Akuelekeze,upate faida,bule tu. Wakati kuna ambaye angeweza kwenda na akaibiwa! Af,kukuunga group hilo,umejiuliza kuna faida gani? Unapokua na watu mbali mbali,hata mawazo utapata. Maswali utauliza,utajibiwa.
Wangapi wamefaidika na andiko lake?
Lakini lingekuwa group la kudinya, hata 50k mngetoa.
 
sawa simu za aina gani hizi za smart ama hizi ndogo zwa viswaswadu au zote. kama upo kariakoo nitafute nikupeleke moja ya duka za jumla pia ujumue mwenyewe255784705349,255674846674
Zote mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…