Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 16,879
- 31,253
Urusi, Afrika Kusini na China kuanza mazoezi ya kijeshi February 23.
Urusi, Afrika Kusini zatetea mazoezi ya kijeshi na China
Afrika Kusini na Urusi zimetetea uamuzi wa kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na China mwezi Februari, huku Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, akianza ziara yake nchini Afrika Kusini.
Lavrov aliwasili siku ya Jumatatu (Januari 23) kwenye mji mkuu wa Afrika Kusini, ambako alipokewa na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Afrika Kusini, Naledi Pandor.
Kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, waziri huyo wa mambo ya nje wa Urusi alisema suala la mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya washirika hao watatu halina utata na asingelipenda kamwe lihusishwe na kashfa yoyote.
Lavrov aliongeza kwamba nchi yake imeshatoa "taarifa zote muhimu juu ya mipango yake kwenye mazoezi hayo ya kijeshi", ambayo yamekosolewa vikali na mataifa ya Magharibi na washirika wao.
Afrika Kusini yashikilia msimamo wake
Waziri Pandor aliwaambia waandishi wa habari kwamba nchi yake inaendelea kushikilia msimamo wake wa kuwa tayari kuunga mkono suluhisho la amani kwa migogoro ya ndani ya Afrika na ya kwengineko ulimwenguni.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Naledi Pandor (kulia) akiwa na mgeni wake, Waziri wa Mmabo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Pretoria siku ya Jumatatu (Februari 23).
Hata hivyo, Lavrov alidai kuwa nchi yake daima imekuwa tayari kwa majadiliano, lakini ni upande wa Ukraine ndio unaokataa mazungumzo ya amani,
Licha ya kwamba Afrika Kusini ina kiwango kidogo cha biashara na Urusi, lakini inazingatiwa kuwa kinara wa mtazamo unaoungwa mkono na China na Urusi ambao unataka dunia yenye mihimili mingi ya nguvu badala ya ulimwengu wa sasa unaotawaliwa na nguvu moja tu ya Magharibi, hasa hasa Marekani.
Pandor alisisitiza kwenye mkutano huo na waandishi wa habari kwamba nchi yake haitaburuzwa iegemee upande wowote, na badala yake ameyakosoa mataifa ya Magharibi kwa kuilaani kwake Urusi huku yakipuuzia masuala mengine kama vile ukaliaji wa mabavu wa Israel kwenye ardhi ya Wapalestina.