Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!

Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!

Joined
Apr 27, 2006
Posts
26,584
Reaction score
10,400
"Kuifufua Tanganyika ni Kuiua Tanzania,Sikubaliani Kabisa na Swala hili,Kwa Sifa tu na Uroho wa Madaraka na huku Wakishabikiwa na Mazuzu kuna watu Watafanya Kila hila Zanzibar Ijitenge na Tanganyika,Nasema Dhambi hii ya Utengano na Iwatafune,Naomba Mungu anisamehe,Hakika Dhambi ya Utengano na Iwatafute hawatabaki Salama" - By.Mwl.Julius Nyerere.
 
Kumbe mnamkumbuka tu kuhusu muungano vipi kuhusu rushwa, ufisadi na uhujumu rasilimali za taifa?
-mikataba feki unaizungumziaje?
-utawala wa kifalme unaochipuka kwa kasi unauzungumziaje?
-vyombo vya dola kuua raia wasio na hatia unazumgumziaje?
-kuwafanya wananchi watumwa katika nchi yao vp?

**KAMA KWELI MNANUENZI NA KUMKUMBUKA MWALIMU BASI MKUMBUKENI KWA MATENDO.

My take: Tanzania kwanza wageni baadae
 
"Nasema Dhambi hii ya Utengano na Iwatafune,Naomba Mungu anisamehe,Hakika Dhambi ya Utengano na Iwatafute hawatabaki Salama"...

Haya maneno hutamkwa na watu wasio wema, na kamwe watu wasiopata katika shauri wakitengana sio dhambi...

Nyerere sio Mungu na ndio maana leo hii hayupo tena kama ambavyo wengi wetu kesho hatutakuwepo...
 
Mimi na nina hakika tupo wengi tu hatuutakki muungano lakini si kwa nia ya kutaka vyeo au madaraka kwa hiyo maneno yake hayo hayatuhusu. Anayewalenga yeye ni wale wanaotaka kuuvunja muungano kwa ajili ya vyeo na madaraka.

Halafu binadamu gani huyo "anayewaapiza" wenzake kwa ajili tu wametofautiana kimtazamo?
 
Achana na ushabiki wa huyu Mzee, Mbona hakutaka kuizika Zanzibar tukawa nchi moja ya Tanzania ? Makosa aliyoyafanya kwa kutoizika Zanzibar ndo yanatu cost hizi vurugu zote , Kama unataka muungano wa kweli shabikia Tanzania moja ya nchi moja na serikali moja
 
"Kuifufua Tanganyika ni Kuiua Tanzania,Sikubaliani Kabisa na Swala hili,Kwa Sifa tu na Uroho wa Madaraka na huku Wakishabikiwa na Mazuzu kuna watu Watafanya Kila hila Zanzibar Ijitenge na Tanganyika,Nasema Dhambi hii ya Utengano na Iwatafune,Naomba Mungu anisamehe,Hakika Dhambi ya Utengano na Iwatafute hawatabaki Salama"
- By.Mwl.Julius Nyerere. [\Quote]

wakati akiongea hayo kulikuwa na nchi moja na serikali mbili. sasa kuna nini?
 
Labda nikuulize Zanzibar imejipa mamlaka kamili wakati gani? je ni wakati Nyerere akiwa madarakani au baada ya Kung'atuka? Zanzibar wameishajipa Mamlaka kamili na inatambulika kama Nchi na wewe ukienda kuishi huko lazima uwe na kitambulisho cha Ukazi wa Huko tofauti na huku Bara Wazanzibar wanaishi kama wapo katika nchi yao.

"Kuifufua Tanganyika ni Kuiua Tanzania,Sikubaliani Kabisa na Swala hili,Kwa Sifa tu na Uroho wa Madaraka na huku Wakishabikiwa na Mazuzu kuna watu Watafanya Kila hila Zanzibar Ijitenge na Tanganyika,Nasema Dhambi hii ya Utengano na Iwatafune,Naomba Mungu anisamehe,Hakika Dhambi ya Utengano na Iwatafute hawatabaki Salama" - By.Mwl.Julius Nyerere.
Hapo kwenye RED alichokitamka Nyerere Dhambi hiyo ya utengano itawatafuna/Inawatafuna CCM kwani kule Zanzibari waliosababisha utengano huo na kuipa mamlaka kamili Zanzibar ni CCM wenyewe na hivyo utambue Zanzibar imeishajitenga kulingana na Katiba yao ilivyo kwani wana Bendera na Nyimbo za Taifa lao.
 
Haka ka mungano mbona kanaliliwa hivi. Kwani Kana nini cha maana. Mbona Mimi sioni. Mpaka inafikia kuombeana laana kwa mwenyezi.

Marekani miaka ya 1800 kipindi cha rais abraham lincoln walipata sakata kama hili. Wakapigana civil wars so to defend the union. Lakini Hawa walikiwa sahihi kwa sababu walikiwa na nchi nyingi Zilizoungana, na sio mbili kama sisi. Hapa point ya defence ipo. Lakini kwa Tz na znz siioni.

To hell with this non profitable union.

Note. Sim yangu ina tatizo la letter 'u' so don't mind where it brings some confusions.
 
Achana na ushabiki wa huyu Mzee, Mbona hakutaka kuizika Zanzibar tukawa nchi moja ya Tanzania ? Makosa aliyoyafanya kwa kutoizika Zanzibar ndo yanatu cost hizi vurugu zote , Kama unataka muungano wa kweli shabikia Tanzania moja ya nchi moja na serikali moja

Sawa kabisa, na hiyo dhambi itawatafuna Wazanzibari kwa kutangaza kuwa Zanzibar ni nchi, ambayo ni sawa na kuuvunja Muungano
 
Back
Top Bottom