Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!

Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!

Kumbe mnamkumbuka tu kuhusu muungano vipi kuhusu rushwa, ufisadi na uhujumu rasilimali za taifa?
-mikataba feki unaizungumziaje?
-utawala wa kifalme unaochipuka kwa kasi unauzungumziaje?
-vyombo vya dola kuua raia wasio na hatia unazumgumziaje?
-kuwafanya wananchi watumwa katika nchi yao vp?

**KAMA KWELI MNANUENZI NA KUMKUMBUKA MWALIMU BASI MKUMBUKENI KWA MATENDO.

My take: Tanzania kwanza wageni baadae

Mkuu na ku LIKE, ASILIMIA 100 UMESHAMALIZA KUMJIBU HUYU KIUMBE DHAIFU... Bg up sana
 
wapuuzi sana ninyi walafi na walaghai, inapofika muda wa maslahi mnamtaja baba wa taifa kutumia maneno yake yanayoishi, inapofika wakati wa kuwatendea haki wananchi na kufisadi na kuiba maliza umma HATUSIKII YEYOTE AKINUKUU MANENO YA BABA WATAIFA, WALAFI SANA NINYI TUSHA WAZOEA. HAKUNA MWENYE UWEZO WA KUMISHI MWALIMU.
 
W. J. Malecela nyie mnatubagua sana sisi wazanzibar. mnamuita nyerere ndio baba wa taifa kwani karume sio baba wa taifa la tanzania? bila karume kuna tanzania? na nyie ccm ndio mmetuchokoza hatuutaki muungano huu.

Nyerere anaweza kuwa mwasisi wa tanganyika sio tanzania maana tanzania ni muungano wa nchi mbili huru. wana ccm manachefua waznz na kwa taarifa yako sisi huku znz ni wamoja hakuna cha ccm wala cuf ndio maana tumebadili katiba yetu mishipa ya shingo inawatoka. na mtachoka sana mwaka huu.

- Kaka punguza jazba kama vipi mtukane Mwalimu ndiye aliyesema maneno hayo niliyoyaleta mimi ni messenger tu sasa mbona mnalia sana vipi maneno ya Mwalimu Baba wa Taifa yanawagusa nini ndugu zangu, ha! ha! ha!

- Hayo maneno ni msumari wa moto, ukiyasoma yanakugusu mpaka moyoni unaanza kuweweseka, ha1 ha! ha!


Le Mutuz
 
wapuuzi sana ninyi walafi na walaghai, inapofika muda wa maslahi mnamtaja baba wa taifa kutumia maneno yake yanayoishi, inapofika wakati wa kuwatendea haki wananchi na kufisadi na kuiba maliza umma HATUSIKII YEYOTE AKINUKUU MANENO YA BABA WATAIFA, WALAFI SANA NINYI TUSHA WAZOEA. HAKUNA MWENYE UWEZO WA KUMISHI MWALIMU.

- Kaka punguza hasira haya maneno sio yangu sasa pingana basi na Muasisi wa Muungano aliyesema sio mimi ndugu yangu, vipi maneno yanawasuta haya ni mazito I know, ha! ha! ha!

Le Mutuz
 

Kwani William aliesimamia na kukaa kimya mpaka zanzibar wakavunja katiba si Raisi wako dhaifu Jk au hufaham kwamba mambo mengi yamebadilishwa wakati wa utawala wa Rais Aman karume wa zanzibar na Kikwete wa Tanzania... Kikwete ni Rais dhaifu ambae hajawahi tokea hapa tz...wenye kuelewa wataelewa...
 
- Kaka punguza jazba kama vipi mtukane Mwalimu ndiye aliyesema maneno hayo niliyoyaleta mimi ni messenger tu sasa mbona mnalia sana vipi maneno ya Mwalimu Baba wa Taifa yanawagusa nini ndugu zangu, ha! ha! ha!

- Hayo maneno ni msumari wa moto, ukiyasoma yanakugusu mpaka moyoni unaanza kuweweseka, ha1 ha! ha!


Le Mutuz
Mbona karume humnukuu aliposema muungano ni kama koti likikubana unalivua?
 
Tehetehe!! Mkataa kwao mtumwa turudi kwetu Tanganyika. Mbona yeye amerudi kwao Butiama baada ya siku zake kuisha?.
 
- Unajua sometimes ukinyamaza unaweza kuonekana una akili sana kuliko kujivua nguo namna hii, sasa unapingana na nani hapa Mwalimu au mwenyewe maana maneno ni ya Mwalimu, yaani hawa Great Thinkers wengine kweli ni shidaaa!!


Le Mutuz

Sijui nisemeje? ulipoleta hii nukuu ya mwalimu ulikuwa na maana gani? Kwani napata shida kuelewa kama unaunga mkono nukuu hiyo au umenukuu tu na kuyaacha. Ulitakiwa ufanye uchambuzi kidogo kwani nukuu yenyewe ilishapitwa na muda kwa kuwa Zanzibar siyo ile tena wakati mwl akitoa nukuu hii.
 
Nyerere sio MUNGU na wala neno lake sio sheria. Wakati wake umepita sasa tufanye yetu kwa wakati wetu huu tulionao.
 
Mkuu W. J. Malecela nilkusoma kwenye uzi wako fulani hapa ukisema wale wa serikali mbili mnahitaji kujipanga ili kumjibu mzee Warioba. Unataka kuniambia hiki ulichokileta hapa ndo kinatokana na kujipanga kwenu? Kama ndivyo basi ni bora mkakiri tu kwamba hamna lolote la maana la kuwaambia watanzania.
 
Last edited by a moderator:

Kaka Willy mie ninakubaliana na maono ya Mwalimu na wewe Mnukuru, kwanini Mtawala tuliye naye ametufikisha hapa pa kumnukuru Mwalimu ama kusaka nini kauli ya Muasisi wa Tanzania?

Je yeye halioni hili? Je CCM yetu haiioni HATARI yake? Kama wanaona kama Mwalimu, lengo la move hii ni kuthibitisha nini? Kama hawakubaliani na Mwalimu nini mashiko wa kuruhusu move hii na pia kuletewa taarifa ama press releases via Nape?

Wewe William na mimi tulimuona Selina Kombani na Jaji Werema wakisema hapana kwenye issue ya Katiba mpya 2010-11, ghafla tukamsikia Rais akisema YES , ajabu akatokea Comrade wa Rais wetu Ndg Kingunge Ngombale Mwiru akimkatalia M/kiti wake kuwa hiyo si agenda yetu 2010-15, wewe mwenzangu Willy na MiMi tulichukua hatua zipi kama wana CCM juu ya viongozi hawa wanne wa CCM?

Naona kuna mixeup nyingi mno hapo.....tumsubiri Rais aendelee kutupa picha kama alivyowaambia viongozi wa Vyama pale Whitesand.....
 
Chama Cha Mapinduzi chenye wanachama wenye akili,na ukweli,na ujasiri,hakiwezi katu kukubali sera ya serikali tatu, kikijua wazi wazi kwamba matokeo na shabaha ya sera hiyo ni kuiua, na kuizika Tanzania. Chama Cha Mapinduzi kikiwa na msimamo huo, na wala kisiuonee haya, Tanzania itadumu.
Julius K Nyerere
UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA ;1994
 
Nyerere baba wa Taifa sijui Karume atakuwa nani,nafikiri atakuwa mama wa taifa kwasababu anapokuwapo baba na mama lazima awepo

Tuwekee na kauli ya mama wa taifa kuhusu mungano, Mkuu ......Moja katika aliyosema karume kuhusu mungano ni :- "Mungano kama koti linapokubana unalivua",

kuhusu ujamaa alisema: "Azimio la Arusha mwisho wake Kisiwa cha chumbe",,,,,,,,,,,kwa mtazamo wangu hapo Karume tayari alikuwa ameshavunja mungano
 
Sijui nisemeje? ulipoleta hii nukuu ya mwalimu ulikuwa na maana gani? Kwani napata shida kuelewa kama unaunga mkono nukuu hiyo au umenukuu tu na kuyaacha. Ulitakiwa ufanye uchambuzi kidogo kwani nukuu yenyewe ilishapitwa na muda kwa kuwa Zanzibar siyo ile tena wakati mwl akitoa nukuu hii.

- Kaka toa hoja kuhusiana na maneno ya Mwalimu kama ulitaka maoni yangu hapa hayapo so far wewe deal na maneno ya Mwalimu kama huyawezi tuliza boli kaka waachie wengine wanaoweza kujibizana na Mwalimu.

Le Mutuz
 
Nyerere alikuwa binadamu kama wengine maneno yake siyo msahafu kuwa yasipingwe, hakuna anayetaka kuvunja muungano tatizo la huu muungano una matatizo mengi.

Watu wanaitaji muungano wenye maslahi pande zote mbili, Jaji Warioba kaeleza kero za muungano huu wa kimaghumashi.

Siyo wote wanahoji huu muungano wanataka madaraka.
 
Back
Top Bottom