Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!

Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!

Mwalimu Nyerere katoa kauli nyingi mno lakini hadi Leo hazikumbukwi kwa maslahi ya wanasiasa muflisi. Mwalimu Nyerere alipenda azimio la Arusha na aliongea mengi kuhusu azimio Hilo. Wanasiasa fisi wameliulia mbali.Nyerere alimlaani Malcela lakini Leo watoto wake wanamiliki blogs ambako hata siku moja hawajawahi andika laana hiyo. Hatutaki unafiki.
 
"Waasisi wa taifa hili waliacha nchi moja serikali mbili lakini sasa kuna nchi mbili serikali mbili" walioachiwa walikuwa wapi yakitendeka haya? walioapa kuitetea katiba walifanya nini hadi haya yakatokea? wawakilishi wa wananchi walifanya nini baada ya kuona katiba inavunjwa au imevunjwa? kura ya kutokuwa na imani si bado ipo? kwani sasa imechelewa?
 
Nyerere siyo MUNGU full stop. Alikuwa binadamu kama wewe, na hamna binadamu asiye na mapungufu yake. Moja ya mapungufu makubwa ya Nyerere ni katika huu muungano wa kimagumashi. kila uwambialo usikariri, changanya na akili zako.
 
KARUME'muungano ni kama koti ukilichoka unalivua'wazanzibar washavua koti kwa kuwa na katiba, ,wimbo wa taifa,bendera na sasa wanataka mamlaka kamili yaani wawe na kiti UN.unachoongea hapa na kuweka maneno ya Nyerere ni kazi bure ningekushauri uende zanzibar uwaeleze busara hizi za mwalimu
 
- Mkuu punguza hasira maneno ya Mwalimu hapa mimi sijasema kitu, kama unataka pingana na maneno ya Mwalimu Baba wa Taifa kama alivyofanya Warioba, usinilaumu mimi hapa sijasema anything punguza hasira haya sio maneno yangu kaka ni ya Mwalimu!1

Le Mutuz

Hivi Mungu hajakataza Uzinzi mbona binaadamu wanaendelea kuzini?
Ikiwa Mungu kaweka mipaka ya binaadamu na bado binaadamu wanachupa mipaka itakuwa kwa mtu km Nyerere ambaye hata unabii hana!.
 
Nyerere na Karume ndio Waasisi wa huu Muungano. Kwa vyovyote vile lazima Nyerere atetee kitu alichokianzisha!Si dhambi, na hapaswi mtu mwingine yeyote kumzuia mwenzake kufikiria njia bora ya kile anachokitaka.Muungano ni mzuri endapo utanufaisha pande zote mbili kwenye huo muungano.Hadi kufikia sasa, Zanzibar ndio waliouvunja Muungano kwa kutamka waziwazi kwamba wao ni Nchi!Mnataka Tanganyika wasemeje?Na pia hatuwezi ishi kwa kuongozwa na mawazo ya kichwa kimoja as if ndiye mtu pekee ambaye Mungu alimpa Akili!Kila mwanadamu yupo huru kufikri na kuamua, bila kulazimishwa kufuata anachokiwa Mwingine.Tusiwe men of Iron kazi yetu ikawa kutukuza wengine tu kama vile sisi hatuna Akili ya kupambana na maisha yetu.Nyerere alifikiria kwa UPEO WAKE, NAWE FIKIRIA KWA UPEO WAKO!Hizi Si Enzi za ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI!
 
Nyerere alikua ana maanisha kua ni Lazima Tanganyika iendelee kunufaika kwa kuidhulumu Zanzibar...kwa Hili Nyerere yuko motoni anachomwa kwa kuawadhulumu watu wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
 
Siku hizi William naona umeanza kupevuka na kuja na mada zenye mashiko kidogo.. Au nguvu ya maji ya kujani imeanza kupungua mwilini?
 
Willy yaonekana ama hukumsikiliza warioba au ulimsikiliza na kwa makusudi ukaamua kumpuuza.muungano tulioachiwa na waasisi sio huu tuliokuwa nao leo.walituachia serikali mbili na nchi moja,lakini leo tuna serikali mbili na nchi mbili.je wakati Zanzibar wanafnya marekebisho ya katiba yaliyopelekea nchi yao kutambuliwa kama nchi na hiv yo kuvunja katiba ya nchi,hamkuwepo.safari hii hamtoki,na mwenyekiti wenu yuko kwenye dilemma asijue afanye nini kati yakupinga maoni ya wananchi jambo ambalo litamvua nguo,au kusariti misimamo haramu ya chama chenu.pole.
 
William hayo maneno ni halali kwa heshima ya msemaji lakini kwa upande wa CCM hakuna kwa sasa anayestahilii kuyatumia wala kuyaongelea kwani hadhi hiyooo hakuna mwenye nayo ndani ya chama na serikali.
Kama Zanzibar iliruhusiwa na viongozi wa Muungano na CCM kuvunja katiba ya Muungano kupitia Marekebisho ya KUMI ya katiba ya Zanzibar, lipi tenaa la kujadili hapoo!! Kiburi au utovuu wa nidhamuu kwa Muunganoo wetu???
Kasoroo kubwaa mpaka sasa viongozi wanaamini wao ndo Muungano kwa maslahi yao ya kisiasa.
Umma uachwee ujadilii kwa uhuru na nafasi hatima ya MUUNGANOO kwa masilahi ya WATANZANIA.
 
Wacheni kuipa znz mamlaka ya Bandia nyinyi wajinga mpaka leo Rais wa Zanzibar anahisabika kama waziri wa kawaida akiingia Bungeni...ni Mamlaka au ndo katika kujihalalishia kuibia zanziba. Kama znz ina mamlaka mbona TRA inachukua hela za wa znz kila siku kama zao...msianze kuukimbia ukweli wa Warioba kua mlikua mkiibia znz...Tena wizi wa mchana...Laana iwe juu yenu
 
Nyerere alikuwa binadamu kama wengine maneno yake siyo msahafu kuwa yasipingwe, hakuna anayetaka kuvunja muungano tatizo la huu muungano una matatizo mengi.

Watu wanaitaji muungano wenye maslahi pande zote mbili, Jaji Warioba kaeleza kero za muungano huu wa kimaghumashi.

Siyo wote wanahoji huu muungano wanataka madaraka.


Aiseeeee
Ni ww kweli?
 
Back
Top Bottom