Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!

Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!


Hayo maneno mkawaeleze waliozembea na kuiruhusu Zanzibar kuandika Katiba inayoitambua kama nchi yenye karibu kila kitu kasoro madaraka kamili.Na kama hizo ndizo hoja zenu za kutetea muundo wa Serikali mbili basi huo ni upuuzi na uzuzu uliopita kiwango!
 
Kwa maneno hayo si kwamba hataki siri kali 3. Bali muungano uwepo ili mradi ni njia gani ya kuufanya uwepo. Sisiem kama wanataka mbili wakae tayari kunyolewa. Na watambue sa hivi hatuishi kwa historia sie

Hakuna hoja hapo.

Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji mstahafu Joseph Sinde Warioba ameweka wazi kabisa kwamba, Baba wa Taifa Nyerere(RIP) na Abeid AmanI Karume(RIP) walokuwa waasisi wa Muungano huo na hawakutaka kuanzishwa kwa Tanganyika hawakuacha SERIKALI MBILI NA NCHI MBILI, baali wao walituachia SERIKALI MBILI NCHI MOJA!

Sasa tuwaulize CCM na hao Wazanzibara na Wapemba, hii nchi inayoitwa JAMHURI YA ZANZIBAR yenye MAMLAKA KAMILI(Sovereighty state)yenye BENDERA YAKE,WIMBO WAKE wa TAIFA,BUNGE LAKE NA RAIS WAKE imetoka wapi????

CCM mlikuwa wapi wakti ZANZIBAR wanavunja Katiba ya nchi?

CCM mlikuwa wapi wakti AZIMIO LA ARUSHA linakanyagwa,kupondwa pondwa na kuzikwa hukohuko ZANZIBAR?

Je, inawezekana CCM mlishaigeuza ZAZIBAR kama kichaka cha kuvunja KATIBA na kupindisha mambo kwa kadri mnavyoona inafaa??

Kwa sasa Watanzania tunasubiri maamuzi ya BUNGE LA KATIBA kuhusu mwelekeo upi utafaa kati ya Serikali 2 au 3 kwa kutumia UBABE wenu wa aidha kura ya WAZI au ya SIRI!
 
Hoja sio kulilia muungano,tuangalie faida za muungano kwa raia sio kwa viongozi,hiyo laana ya Nyerere iwapate wanaosafirisha twiga na mafisadi.
 
chama cha mapinduzi chenye wanachama wenye akili,na ukweli,na ujasiri,hakiwezi katu kukubali sera ya serikali tatu, kikijua wazi wazi kwamba matokeo na kshabaha ya sera hiyo ni kuiua, na kuizika tanzania. Chama cha mapinduzi kikiwa na msimamo huo, na wala kisiuonee haya, tanzania itadumu.
Julius k nyerere
uongozi wetu na hatima ya tanzania ;1994

nakubaliana na wewe ngugu
 
Nyerere siyo MUNGU full stop. Alikuwa binadamu kama wewe, na hamna binadamu asiye na mapungufu yake. Moja ya mapungufu makubwa ya Nyerere ni katika huu muungano wa kimagumashi. kila uwambialo usikariri, changanya na akili zako.

Wamuache mzee wetu apumzike kwa amani. Mwalimu alizungumza hayo maneno kipindi na mazingira tofauti ya kisiasa! Akiwa kaburini waliwaruhusu Wazanzibari wavunje Katiba ya JMT! Hata walipoelezwa na akina Lissu kwamba Katiba ya Zanzibar imekihuka vifungu muhimu vya Katiba hawakujali. Haya majamaa ni manafiki sana.
 
Wakati huu tulionao hata angekuepo Nyerere asingeweza kuzuia serikali tatu,Zanzibar walishavunja muungano toka pale walipopitisha katiba yao.

Hiv huwa najiuliza hawa viongozi walikuwa wapi mpaka zanzibar inatengeneza katiba yake?
 

Aliwahi kunukuliwa vilevile akisema ...."Iwapo wananchi walio wengi wa Zanzibar wataamua, bila msukumo wa kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, kwamba muungano unaathiri kuendelea kuwepo kwao, siwezi kuwalazimisha kwa kuwapiga mabomu.... Muungano utasita kuendelea pale ridhaa ya washirika wake itakapoondolewa"

Julius Nyerere, The Observer (London), April 20, 1968

 
William umechagua tunda chungu sana, sijui kama utalila, maana reflections za uzi wako zinawarudieni huko mlipo.

Wakai unawekkauli za Nyerere tunaomba ujiandae pia kuweka kauli za Karume.

Pia tungeenda utujulihe, Je mlikua wapi wakati Zziba waafanya maekebisha ya katiba, yaliyopelekea kumua mamlaka raiswa muungano na kurebiha mipaa yao na kujitangaza kuwa ni nci huru? Kwa nini mjitokeze sasa kwa wgi wenu?
 
hata ukimfuata mkulu pale magogoni ukimwambia muungano una faida gani? atakuambia hauna faida yeyote

ccm/serekali wanachohofia muungano ukivunjika zanzibar haichewi kuwa kama somalia
na huku tanganyika hatutakuwa salama

wazazibar wengi ni watu wasiopenda kufanya kazi ni watu wanapenda kushinda vijiweni na kunywa kahawa mchana wa jua kali.

muungano ukivunjika ndio mwanzo wa kuipoteza zanzibar sababu pemba na unguja nazo zitatengana

Stupid Lincon nawe uanrudia hayo hayo alofanya mleta mada Le Mutuz nendeni migandini mkanywe chibuku na mbege
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu wa ajabu sana, kwenye muungano baba wa taifa, wizi, ufisadi, ukatili, hakuna baba wa taifa
 
Naomba Mungu leo Bungeni kuwe na maswali ya papo kwa papo baada ya JK kuhutubia bunge tuone kitavyonuka hapo mjengoni!
 
Mr.Malecela,Tanzania inachangamoto nyingi sana,haiwezi kuchukua maneno ya Nyerere kwa ajili ya kizazi cha miaka hamsini ijayo,Muungano ambao wananchi wanataka ni ule wenye manufaa,na ndio maana warioba alitoa rasimu ambayo ni mapendekezo ya wananchi,Nyerere alikuwa mwadilifu lakini hakufanikiwa sana kwenye masuala kama uchumi etc
 
- Kaka punguza hasira haya maneno sio yangu sasa pingana basi na Muasisi wa Muungano aliyesema sio mimi ndugu yangu, vipi maneno yanawasuta haya ni mazito I know, ha! ha! ha!

Le Mutuz

Nenda katayarishe maonyesho ya Miss Reds Tanzania huko ndio faida ya kisomo.chako mtoto mdogo wewe. Wewe alikutuma huyo 'Babako wa Taifa'? Unamtukanisha Mzee Malecela kama vile hakuweza kufanya kitu hata ukajipa ubaba mwengine wewe? Au mzee hajakuandikai urithi? Teh teh teh
 
Back
Top Bottom