Haya ndio Mapinduzi ya Zanzibar, yamerikodiwa live na waitaliano 1964

Haya ndio Mapinduzi ya Zanzibar, yamerikodiwa live na waitaliano 1964

Bin Faza

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2013
Posts
502
Reaction score
191
Wana JF

Wengi ya washabiki wanaojadili mapinduzi haramu ya zanizbar ya 1964, wanakuwa wanasema watakavo au kwa mujibu wa taaluma walizipata kutoka kwa vyombo vya habari vya tz au wana propaganda wabaguzi wa ASP/TANU/CCM

Wengi wanashindwa kujiuliza ni nini hasa kiljiri siku hizo,lakini ukweli ni kwamba watu wapatao 17,000 (wakiwemo wanawake, watoto, vizee na wagonjwa) waliuliwa bila hatia yoyote kwa usiku mmoja kosa lao kubwa ni kuwa Mungu wamewajaala kuzaliwa kutoka familia za kiarabu kwahivo kabila na rangi zao ndio zilowasababisha kuuliwa kinyama kabisa. masaka kubwa hii ambayo hadi sasa haizungumzwi kisheria.

La kushangaza zaidi ni kwamba wengi ya washabiki hawa hawajui kwamba mapinduzi/mauwaji hayo yalirikodiwa live na wataliana na waingereza.

suala hapa ni kwanini watalaiana? walijuwaje kwamba tarehe 12 jan usiku wa 1964 kutakuwa na mapinduzi zanzibar? nani alowaalika kwenda kurikodi mauwaji hayo? waingereza ingaingia akilini kwasababu wao ndio waliokuwa wakitawala east afrika yote

video hapo chini for your watching pleasure

ikiwa hujui kitaliana, nyengine zimefasiriwa kwa kiarabu na subtitled kwa english

Last edited by a moderator:
Kaka wengi wa wazee wakizanziabri wameliswa sumu ya mapinduzi na maji yabendera ya CCM huna vyakuawaambia kuhusu muungano na baadh ya vijana mbulula wasioa Soma wana kula hayo mabaki bila yakujielew wanacho kifanya ila kwawale wanao jijua na kuifuatilia historia ya nchi yao ndio wajua ukweli wanchi yao.
Niliingiwa na wasiwasi na haya yaitwayo mapinduzi yaliyo leta ukoloni hadi hii Leo.
 
Attachments

  • zanzibar_uhuru_63_scaled.jpg
    zanzibar_uhuru_63_scaled.jpg
    49.1 KB · Views: 1,029
Sasa Angalia unafiki ulio fanywa na Julius Nyerere na Abedi Amani Karume. John Okelo wakampoteza kwenye ramani ya. Zanzibar na Tanzania, na Mohamed Babu wakamkimbiza nchi akaishi na kufia uhamishoni. Nadhani mnaona wenyewe hapo Babu alivyokua ana poromosha Ngeli la ukweli kuashiria kua kwa kipindi hicho alikua ni Msomi wa hali ya juu.

Enyi wa Zanzibari na Watanganyika Zindukeni sasa. Yatosha!
 
Du! Kumbe 2005 iliku hivi, mama yangu wewe! Mimi ningekua Mzanzibari! Ningeandika historia ya Tanganyika, Zanzibar na Tanzania Upya kabisa. Daah! Let it repeat! Nitanunua Ugomvi tu! I swear!
 
Kwa kweli ni hatari tupu,ndio maana zanzibr siku za uchaguzi hupelekwa vifaru kutoka mrima.

mi nafikiri hizi video zinaweza kuleta tafsiri ya huruma kwa wale walioathiriwa na mapinduzi. lakini ktuoka moyoni bado naamini kulikuwa na uhalali wa kufanya mabadiliko ya kisiasa zanzibar wakati ule. na kwa vile udhalimu haukuruhusu mabadiliko ya amani mapinduzi yasinge epukika. madhambi yaliyofanywa na waarabu kuwakamata, kuwatesa na kuwatumikisha weusi kama watumwa lazima yangelipwa tu hata na vitukuu vya waarabu husika. unyanyasaji wa hali ya juu kufanywa na serikali ya Jamshid ndani ya mwezi mmoja baada ya uhuru ulitosha kuiondoa serikali yoyote madarakani. mfano kukamata, kutesa na kufungia wapinzani, kufungia magazeti yanayokosoa serikali, kufukuza kazi polisi wote wenye aasili ya bara na kushindwa kurekebisha mgawanyo wa ardhi wa kibaguzi uliokuwepo ni miongoni mwa uhuni uliofanywa na serikali ilyokabidhiwa uhuru desemba 1963.
 
Msitufanye wajinga hizi si scenes za cinema iliyochezwa kwa madhumuni ya propaganda?

Shukran sana;

1. Video ya kwanza yenye mauaji na maiti makaburini ni ya rangi. 1964 ni vigumu kikundi cha kiitalia kuwa na colored videography ya ku-shoot zenj

2. Ukiiangalia hiyo helikopta kuna mahali wanatupa kitambaa cheupe, Chanini?

3. Makaburini maiti wamepangwa na wengi wana kofia zao vichwani!!!!

4. Mtangazaji anazungumza Nyerere, Rais Tanzania wakati hakukuwa na Tanzania wakati wa Mapinduzi hayo

5. Maiti wote wameuliwa chini ya MTI wa KIVULI!!!!!!! wamelaliana bila dalili za kukurupuka kuhami maisha yao. Wamefia kivulini!!!!!!

6. Kaburi lilichimbwa siku gani? ya kupindua au kabla au baada? na ukiyaangalia yamefuatana.

7. Angalieni mengine na nyie.
 
Dah kaka mengine ya utesaji yapo mpaka leo na hawa maccm,kweli inabidi kujikomboa
 
Shukran sana;

1. Video ya kwanza yenye mauaji na maiti makaburini ni ya rangi. 1964 ni vigumu kikundi cha kiitalia kuwa na colored videography ya ku-shoot zenj

2. Ukiiangalia hiyo helikopta kuna mahali wanatupa kitambaa cheupe, Chanini?

3. Makaburini maiti wamepangwa na wengi wana kofia zao vichwani!!!!

4. Mtangazaji anazungumza Nyerere, Rais Tanzania wakati hakukuwa na Tanzania wakati wa Mapinduzi hayo

5. Maiti wote wameuliwa chini ya MTI wa KIVULI!!!!!!! wamelaliana bila dalili za kukurupuka kuhami maisha yao. Wamefia kivulini!!!!!!

6. Kaburi lilichimbwa siku gani? ya kupindua au kabla au baada? na ukiyaangalia yamefuatana.

7. Angalieni mengine na nyie.

Hata uletewe video polisi anarusha bomu mkutano wa chadema arusha utabisha utasema huyo polis ni wa chadema.
 
Hata uletewe video polisi anarusha bomu mkutano wa chadema arusha utabisha utasema huyo polis ni wa chadema.

Bobwe; wenye ile documentary ya Okello ni ya BBC hata mwandishi anajulikana. Angalia kuwa ni ya Black and white. Video zote mbili zimepiga tukio la siku moja hiyo hiyo. Uwezekano wa kikundi cha kiitalia 1964 kiwe na COLOR VIDEOGRAPHY halafu BBC wawe na black and white HAUPO.

Huwezi kusanya watu 500-600 chini ya mti wa kivuli ukaanza kuwafyatulia marisasi bila kutokea patashika ya baadhi kukimbia na kuondoka walipokuwa wamekaa. Hiyo video hayo marehemu wote hakuna dalili za kukimbia toka hicho kivuli cha huo mti

Zoom down kwenye image yenyewe tafuta wenye damu za marisasi zionyeshe!!!!!

By the way, umeona mitaa ya zanzibar? Hawa si walikuwa na ndege?

Mwisho ni kuwa usije-confuse kuwa sina huruma na wale waliopoteza maisha yao katika jambo hili. Nachokwambia na wote pia ni kuwa ukiona jambo chunguza. Aliyeiweka hiyo video pia ana yake. Mi namsikia tuu akisema "barbaric africans killing ARABS AND MOSLEMS" sijui hao waarabu ni dini ipi na waislamu ni kina nani!!!!
 
how about kung'oa kucha mabwepande, kurusha mabomu ya kuua watu halafu unasingizia CHADEMA? KUMTESA NASARI NAYO NICHADEMA, KUNG'OA KUCHA ZA CHIBANDA NA DR ULIMBOKA ...................?
 
Msitufanye wajinga hizi si scenes za cinema iliyochezwa kwa madhumuni ya propaganda?

kumbe bado wajinga wapo jf.wewe cjui ni standard seven ama vp?ama kama sio hvyo wewe ni mwanadada fulani hvi asiyependa mabadiliko.kama huelewi hyo ndo hali halisi iliyotokea zanzibar hata wazazi wangu wanazo tape to vcd nowadays kama unazihataji njoo uchukue.thats why wapemba wanapinga ccm na wanapinga muungano.
 
Back
Top Bottom