Hizo propaganda ndio tulizosomeshwa shuleni kuwa warabu waliwanyansa na kuwafanya watumwa watu weusi lakini hiyo sio kesi ya zanizbar,watumwa walikuwa wanaletwa zanzibar kuuzwa tna waliokuwa wakikamata watumwa ni waafrika wenyewe kutoka na tafauti zao za makabila,hakuna mzanzibari aliyewahi kuwa mtumwa,wazanzibar ni watu waliochamnganya damu na wakabila mbali mbali ya afrika na nje ya afrika
Katika afrika mashariki na kati zanzibar ndio likuwa nchi yenye wafrika wasomi kuliko nchi yoyote katika ukanda huu wa Afrika,mafano angali hao akina babu,Hanga na wengineo,watu weusi wa zanzibar walikuwa wanamiliki ardhi walikuwa wamechanganya damu na famili za kisultani,kwaupi hao wanaotwa masultani walikuwa ni machotara wakiarabu waliochanganyika na wamanyema
kama hayo unayoyasema kuhusu utawala Jemshid ni kweli mbona akina karume wameishi mpaka wakuwa maraisi,moja katika mahojiano na mke wa Karume aliwahi kusema kuwa karume alikuwa anapinga mapinduzi,sasa jiulize kwanini Karume alikuwa anapinga mapinduzi kama utawala wa jemshid ulikuwa wa kinayama?Uongo huo haufanyi kazi tena katika karne hii ya "Information technology" kila kitu kiko wazi
Hayo uliyoyasema kuhusu udhalimu wa utawala wa Jemshid kuwatesa na kuwakamata watu ndio tunayoyaona sasa kati ya utawala wa CCM na wapinzani je serikali ya CCM nayo ipinduliwe wanachama wa CCM wauliwe kama kuku!!!!? au unataka kuniambia wapinzania hawakatwi na kuteswa na utawala tuliona sasa!!!? tafakari
Kuuwa ni dhambi,kuuwa watu walikuwa hawana hatia ni kufuru na dhambiMapinduzi ya zanzibar yalikuwa ni "Genocide"
Chabuso.
Salaam. Nimeisoma bayana yako kwa utuvu mwingi.
Lakini kwa mtazamo wangu nakhis umechanganya khabar/
History nyingi kwa pamoja!?
Kwanini sisi tusijikite mno tu kuanzia pale
1961 onwards!? Nakhis hii itarakhisisha hoja/mazungumzo yetu na kufanza iwe wepesi kufahamiana kwa utuvu baina yetu
wanajamvi!?
Nimeshtushwa kiduchu pale uliponena yakuwa ati hakuna
Mzanzibary alowahi kuwa mtumwa!?...hii
History Sheikh wangu unaianzia tangia mwaka/karne ipi!?
Kama
Waarabu waliwahi kufanzana watumwa baina ya makabila ya wao kwa wao,sasa kipi tena ati ndo kiwazuie pale walipofika
Unguja/Zanzibar ndio ati waache/wasitishe zile dasturi zao za kinyama na umaluuni!?
Huu unyama na udhalimu umefanzwa na makabila/jumuia takriban zoote duniani na mpaka kesho haya majambo yanaendela kwingi mno duniani.
Tunajua yakuwa hata Wazungu nao walianza kufanziana utumwa na udhalimu mwingi mno baina yao hata kabla hawajaanza kufikiria kufika/kuja
Afrika.
Pia tuna mifano ya
India,China,Mongols na mpaka hivi karibuni ki-Historia vituko vya
Oliver cromwell kwa Ma-
Irish!?
Waafrika nao hawakuwa nyuma asilan katika kufanziana utumwa na udhalimu uso mipaka kabla hata yakuwa influenced na hao Waarabu au Wazungu. Tutazame pia kiundani unyama,utumwa na uharamia ulo kubuhu alokua akifanza
Kabaka,MwanaMutapa na
Chaka Zulu dhidi ya watu weusi wenzao kwa miaka mingi mno,tena wala sio
centuries nyingi zilizopita!?
Angalia wale
freed Slaves nao ule uharamia,unyama na utumwa waliowafanyia
watu weusi/Waafrika wenzao pale
Liberia - The freed land!? Inasemekana na ushahidi mwingi wa kina upo,yakuwa mambo walofanza wale
Afrikan Amerikans (waliojikhis light/fair skinned) dhidi ya ndugu zao
natives Afrikans...hayakuwahi kufanzwa hata na hao manguli wa utumwa na udhalim Wazungu!?
Tukumbuke hivi vituko na unyama huo ndo mpaka kesho bado unaendela na umeacha makovu makubwa katika History ya pale
Liberia maskini!
Labda nakuunga mkono tu pale uliposema yakuwa
History ya Tanganyika/Tanzania,imepindishwa mno kiasi ya kwamba
wasomi/Watanzania wengi wamekua mapunguani wa maarifa.
Nina maana yakuwa
Ilm/History;imejazwa chuki ,hasama,fitna,uzandik
falsifications and fraudulently claims...ili kuwapendezesha
Wazungu(the so called Orientalists) na
propagandas zao.
Hii inawasaidia mno Wazungu ati waonekane wao walikua ni
"wavumbuzi" na "Missionaries" tu,na walikua wastaarabu na watu wazuri mno kwa watu weusi/Waafrika na wao ndo walokataza biashara ya Utumwa na kuhama makwao kwa ajili tu ya kuja
Afrika kuleta maendeleo!?
Wakti huohuo imeenezwa/inaenezwa chuki nyingi mno dhidi ya Waarabu na
myths nyingi mno zinasomeshwa kwenye ma-Skuli/Shule zetu na huku
Serikali ikifumbia macho kwa miaka mingi mno.
Nafikiri matokeo yake ndo utaona hata hapa
Jf,unajadilina na mwanajamvi mwenzio kiundani tena huku wewe ukidhani ni msomi/mtaalamu mahiri...lakini inapokuja kwenye
History ya nchi yetu au hata
Afrika,utagundua udhaifu na chuki nyingi mno with loads of
colonial connotations...kiasi hata waeza kujiuliza hivi kweli nazungumza na
Mtanzania/Mwafrika mwenzangu hapa au maluuni fulani tu wa Kizungu!?
Niwie radhi ndugu yangu,kama kuna lolote labda unakhis sijui/nimekosea au nimenena nawe hukupendezwa nalo!?
Ahsanta sana.