kimboka one
JF-Expert Member
- Jan 23, 2010
- 734
- 85
propaganda za siasa za Tanzania zimeadvance,mngetumia huu muda na akili kuwaletea maendeleo watanzania tungekuwa mbali
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chabuso.
Salaam. Nimeisoma bayana yako kwa utuvu mwingi.
Lakini kwa mtazamo wangu nakhis umechanganya khabar/History nyingi kwa pamoja!?
Kwanini sisi tusijikite mno tu kuanzia pale 1961 onwards!? Nakhis hii itarakhisisha hoja/mazungumzo yetu na kufanza iwe wepesi kufahamiana kwa utuvu baina yetu wanajamvi!?
Nimeshtushwa kiduchu pale uliponena yakuwa ati hakuna Mzanzibary alowahi kuwa mtumwa!?...hii History Sheikh wangu unaianzia tangia mwaka/karne ipi!?
Kama Waarabu waliwahi kufanzana watumwa baina ya makabila ya wao kwa wao,sasa kipi tena ati ndo kiwazuie pale walipofika Unguja/Zanzibar ndio ati waache/wasitishe zile dasturi zao za kinyama na umaluuni!?
Huu unyama na udhalimu umefanzwa na makabila/jumuia takriban zoote duniani na mpaka kesho haya majambo yanaendela kwingi mno duniani.
Tunajua yakuwa hata Wazungu nao walianza kufanziana utumwa na udhalimu mwingi mno baina yao hata kabla hawajaanza kufikiria kufika/kuja Afrika.
Pia tuna mifano ya India,China,Mongols na mpaka hivi karibuni ki-Historia vituko vya Oliver cromwell kwa Ma-Irish!?
Waafrika nao hawakuwa nyuma asilan katika kufanziana utumwa na udhalimu uso mipaka kabla hata yakuwa influenced na hao Waarabu au Wazungu. Tutazame pia kiundani unyama,utumwa na uharamia ulo kubuhu alokua akifanza Kabaka,MwanaMutapa na Chaka Zulu dhidi ya watu weusi wenzao kwa miaka mingi mno,tena wala sio centuries nyingi zilizopita!?
Angalia wale freed Slaves nao ule uharamia,unyama na utumwa waliowafanyia watu weusi/Waafrika wenzao pale Liberia - The freed land!? Inasemekana na ushahidi mwingi wa kina upo,yakuwa mambo walofanza wale Afrikan Amerikans (waliojikhis light/fair skinned) dhidi ya ndugu zao natives Afrikans...hayakuwahi kufanzwa hata na hao manguli wa utumwa na udhalim Wazungu!?
Tukumbuke hivi vituko na unyama huo ndo mpaka kesho bado unaendela na umeacha makovu makubwa katika History ya pale Liberia maskini!
Labda nakuunga mkono tu pale uliposema yakuwa History ya Tanganyika/Tanzania,imepindishwa mno kiasi ya kwamba wasomi/Watanzania wengi wamekua mapunguani wa maarifa.
Nina maana yakuwa Ilm/History;imejazwa chuki ,hasama,fitna,uzandik falsifications and fraudulently claims...ili kuwapendezesha Wazungu(the so called Orientalists) na propagandas zao.
Hii inawasaidia mno Wazungu ati waonekane wao walikua ni "wavumbuzi" na "Missionaries" tu,na walikua wastaarabu na watu wazuri mno kwa watu weusi/Waafrika na wao ndo walokataza biashara ya Utumwa na kuhama makwao kwa ajili tu ya kuja Afrika kuleta maendeleo!?
Wakti huohuo imeenezwa/inaenezwa chuki nyingi mno dhidi ya Waarabu na myths nyingi mno zinasomeshwa kwenye ma-Skuli/Shule zetu na huku Serikali ikifumbia macho kwa miaka mingi mno.
Nafikiri matokeo yake ndo utaona hata hapa Jf,unajadilina na mwanajamvi mwenzio kiundani tena huku wewe ukidhani ni msomi/mtaalamu mahiri...lakini inapokuja kwenye History ya nchi yetu au hata Afrika,utagundua udhaifu na chuki nyingi mno with loads of colonial connotations...kiasi hata waeza kujiuliza hivi kweli nazungumza na Mtanzania/Mwafrika mwenzangu hapa au maluuni fulani tu wa Kizungu!?
Niwie radhi ndugu yangu,kama kuna lolote labda unakhis sijui/nimekosea au nimenena nawe hukupendezwa nalo!?
Ahsanta sana.
Mkuu kinachosumbua hapa ni ubaguzi wa waarabu dhidi ya weusi!
mimi tangu nipo darasa la kwanza hadi for 6, walikuwa wakinipa propaganda hizo hizo waarabu wabaya, walikuwa wakituuwa wakituchinja ..kwanza kama watoto wengine niliwaamini baaade nikaanza kuona kumbe wanatuulia hot air tu hawana la kusomesha
Kama waarabu walikuwa wabaya na madhalimu nimeweka katika makala moja humu mishahara ya Malim aboud Jumbe na Maalim Ali Hassan Mwinyi. Hawa na wengine kama hawa walikuwa na nafasi kubwa tu serikalini.
Lakini kuna watu bado wanatumia siasa za divide and rule zanzibar
Ukimuona mwana CCM anapanda kiriri na kuanza kutukana waarabu ujuwe anatafuta mkono uende kinywani tu, ni njaa tu zinazowasumbuwa hawa.
walipoambiwa wasome walikataa sasa wanasema waarabu hawakuwasomesha waafrika, lakini maajabu zaidi hao yanaosema ni wamkuu ambao siku zao za skuli serikali ilikuwa ya mapinduzi, ukiwauliza kwanini nyinyi hamukusoma jawabu ni kwamba tulikwenda kuvua vibua au kupanda minazi.
Kaka hujakosea chochote hapa tuko kwa kuelimishana,hapa najaribu kuelezaea uhalisia kuhusu zanzibar na enzi zake ninavyouona mimi na sio jengine,nitakurejesha nyuma kidogo tu zanzibar ilipoungana na tanganyika zanzibar ilkuwa na watu takriban laki tatu(300,000),sasa tafuta jibu Dr Livingstone alipotangaza kuondoshwa kwa utumwa katika miaka ya 1800s, je zanzibar ilikuwa na watu wangapi?
jibu la haraka labda kulikuwa na wazanzibari 20,000 hiyo ukifanya thathmini kuwa zanzibar hivi sasa kuna watu millioni moja na nusu(1,500,000),amini usiamini hakuna mzanzibari aliewahi kuwa mtumwa,walikuwepo wazanzibar waliokuwa wanamiliki watumwa walikuwa wanafanaya biashara ya kuuza watumwa akina Tiptip na wenzake.
Wakati huo wa utumwa kama polulation ya zanzibar ilkuwa kidogo hivyo haiwezekani kuwa wazanzibar walikua watumwa la si hivyo wazanzibar wote waliuwa watumwa,Watumwa alikuwa wanaletwa zanzibar kuuzwa kama bidhaa nyengine yoyote ile,wanauzwa wanapakiwa kwenye jahazi wanasafirishwa wanakosafirishwa,mfano kama gari zinavyouzwa Dubai lakini hakuna kiwanda cha gari Dubai,ofcouse is a shame history lakini thats how happened
Kumbuka kaka History imeandikwa na watu kuna walioiposha na kuna waliosema ukweli,kuhusu history ya zanzibar kuna watu wanavutia kwenye uarabu na kuna watu wanavutia kweye uafrika mimi najaribu kuwa "neutral" najaribu kuvutia uzanzibari, karne hii tulionayo ya "information technology "history unaweza kuiandika mwenyewe ingia kwenye google utapata kila kitu
Mimi nina watu/Wazanzibary nilowahi kuwaona kwa macho yangu binafsi ambao waliwahi kuwa Watumwa pale Unguja enzi za Sultan!?
Ikiwa wewe huna asili ya kiarabu au ya kishiraz,lazima utakuwa una Asili ya Tanganyika,kama ww ni mwafrika mweusi.RED Xs
Kwanza sio kweli kwamba washirazi walifanya mapinduzi, washirazi ijapokuwa wanajisema wao ndio wenyeji wa znz lakini kabila lao linatokea Persia, irani ya siku hizi katika mji uitwao Shiraz. Hassan Bin Ali alikuja na watoto wake 7 wakaanzisha Zenj Empire ya kwanza, znz hapukuwa na maisha rasmi, wao wakapafanya ndio kituo chao kuchukuwa maji na mapuumziko kidogo kidogo ndio pakawa na life.
Kwahivo mshiraji na mwarabu sio watu mabli sana, wao hawakushiriki katika mapinduzi
Mapinduzi yalifanywa na watanganyijka, na ikiwa kwa ukweli huu unananihisi mimi ninakuchukieni basi ndio ninakuchukieni kwa kuivamia nchi yetu na kutuulia jamaa zetu kiholela.
wewe utafurahi kama sisi wazanzibar tutakuja tabora au iringa au popote huko tanganyika na kukuuweni kiholela? Jee kwa hilo utatupenda sisi wazanzibari?? be honest pleae!!!!!!
Bosi wako umemuaga?
Nilisema tangu awali hiyo ya RANGI NINA MASHAKA NAYO. NA saabau ni hizi pia nazotoa, hukusoma kiundani post yote kwa vile ulishughulishwa na kutukana watu kwa niaba ya bosi wako (poleni naona uzi wenu umefungwa niliwaonya kuwa hamkujiandaa mkanipuuza!!!!)
Nimesema sina tatizo na documentary ya BBC ya Okello. Na hata Okello mwenyewe kwenye kitabu chake kataja ARABS kama 13,000 waliuliwa, na katika ile post pia nilisema, memory yako vipi?
Na hata hapa nimerudia kumwambia Faza sina tatizo na documentary ya Okello, wewe tatizo liko wapi?
Ikiwa wewe huna asili ya kiarabu au ya kishiraz,lazima utakuwa una Asili ya Tanganyika,kama ww ni mwafrika mweusi.
Na pia jiulize,waarabu walikuwako Tanganyika,miaka mingi kabla hata utawala wa waarabu Zanzibar,mbona waarabu hawa wa Tanganyika,hawajauliwa,hawajateswa,hawajanyanyaswa,mpaka leo wapoTanganyika,na tena idadi ya Waarabu waliopo Tanganyika,wenye asili ya Oman,ni mara kumi na zaidi waliopo Pemba na Unguja.
Pale panapsemwa kuna historia kubwa baina ya Oman na Tanganyika,ufahamu kuna sehemu,Tanganyika ukifika utakuta waarabu ni wengi kuliko hata wenyeji kwa miaka hiyo nampaka sasa,Jiulize sasa kwa nini waarabu hawa Wa Tanganyika,ambao ni wengi kuliko wa Zanzibar,waishi kwa Amani.Lakini Watanganyika hao hao wanaodaiwa kuwauwa waarabu wa Zanzibar,hawakuwauwa,waarabu wa Tanganyika,na wapo waarabu waliokimbilia Tanganyika Toka Zanzibar,akiwemo huyo Sultani wa Zanzibar,kwa nini hakupata madhara yoyote alipokimbilia Tanganyika,kabla ya kwenda Ungereza.
Babou; Baada ya salaam.
Nikushuru sana kwa fikra zilizozama. Ni wachache wenye kukaa na kuleta fikra kama unavyofanya. Japokuwa nasikitika na waliopoteza watu wao, binafsi NAAMINI kabisa kuwa ile video ya kwanza; RANGI ya makaburini ni ya KUGHUSHI (kisa ni kutokuwapo quality color videography 1964, na uwezekano eti waitalia waje zenj na color equipment kupigia picha huku BBC wakimnasa Okello kwenye black and White SIUONI; Kwenye You-tube utaona hata hao maiti wamevaa vibandiko-kofia vyao humo kaburini!!!
Lakini hayo na tuyaache. Tulie na kisa, nani kasababisha huu mkasa? Huyu ndiye wa KUBEBA LAWAMA sio yale MATOKEO. Mbona ASP wapo? Ugumu uko wapi kuwauliza kwanini mlimpindua sultani? Waliopoteza watu wao kwenye hili walitakiwa kwanza kujiuliza HII chuki ya kuja KUUANA ilianzia wapi na vipi? Nani aliyehisi kadhulumiwa kimaisha na kisiasa? ni yupi ALIYEACHIA HII HALI HADI KUFIKIA KUUANA? Jina tuu ASP linawakilisha hisia za watu fulani. Kwanini ni watu wa aina hiyo (waafrika na Washirazi?) WHY? lazima kuna sababu.
Wao warudi kwenye chanzo ndipo WAOMBANE MSAMAHA STAHIKI bila hivyo bado hiyo You Tube itajaa mambo yao huku wanazeekea nchi za watu wengine na hao Viongozi wanaowalaumu wote hakuna aliye hai hivi sasa.
Mnafiki ni chakula ya mamba, wewe kila siku na ulikuwa unatumia hizi hizi video kama ushahidi wa kumtetea bwana wenu Okello leo eti unasema ya kughushi.binafsi NAAMINI kabisa kuwa ile video ya kwanza; RANGI ya makaburini ni ya KUGHUSHI (kisa ni kutokuwapo quality color videography 1964, na uwezekano eti waitalia waje zenj na color equipment kupigia picha huku BBC wakimnasa Okello kwenye black and White SIUONI; Kwenye You-tube utaona hata hao maiti wamevaa vibandiko-kofia vyao humo kaburini!!!
gombesugu
Mkuu
hii yako ya leo kali kidogo, tumewasikia watanganyika wakimapaka matapo sulatan wa zanzibar kwa kila aina lakini hii nadhani unastahiki nobel prize mzee
inavojulikana kimataifa ni kwamba utumwa ulifutwa zanzibar rasmi katika 1886 -1896
sasa hao watumwa unawajuwa wewe waliokuwa zanzibar enzi za sultan iyupi tabidi tukuulize vyema yafuatayo
1. wewe umewahi kufika zanzibar, au uliogopa kwenda huko usije ukafanywa mtumwa?
2. Sultani gani na wamwaka gani huyo alokuwa ndani ya utawala wake kuna watumwa unaowajuwa wewe kw amajina namakubiri yao?
3. Jee unaouthibitisho ya kuwa watu hao walikuwa watumwa?
4. Jee hujichanganyi katika kumbambanuwa baina ya watumwa na watumishi? maana hapa zanzibar wapo hadi leo hii watumishi wa majumbani kutoka tanganyika, wakulima wa mashamba na watumishi wa aina nyengine lakini sio watumwa ni watumishi.
Haaaa haaa! Haya mafundisho kwamba Mtanganyika aliua Wazanzibari ni ya Gaidi Sheikh Ilunga! Kama mwanaume mbona kaikimbia nchi?
Kikwajuni one
kwanza kabisa ujuwe mimi sikubali kulizimishwa katika ubaguzi, mimi nikiwa muarabu, muhindi,mchina, mswahili hapa zanzibar ninajihisi ni mzanzibari halisi.
lakini kukujibu swala lako tu ni kwamba waarbu walioko tanganyika labda ni wengi kama unavodai lakini huko hawakufanya serikali. walikuwa na mado wanabakisha kuwa raia wa kawaida tu.
Waarabu waliokuwepo zanizbar walifanya serikali ndio hiyo munayopenda kuiita serikali ya sultan. kwahivo akina nyerere na watanganyika wenzake wakitumiliwa na wazungu walitaka kufanya kile kiitwacho ethnic cleansing ili waarabu wasije wakatawa tena huko.ndio maana wakakimbilia kufany amuungano mara tu baada ya mapinduzi ili kuhakikisha sultan harejei tena
nadhani nimekujibu
gombesugu
Mkuu
hii yako ya leo kali kidogo, tumewasikia watanganyika wakimapaka matapo sulatan wa zanzibar kwa kila aina lakini hii nadhani unastahiki nobel prize mzee
inavojulikana kimataifa ni kwamba utumwa ulifutwa zanzibar rasmi katika 1886 -1896
sasa hao watumwa unawajuwa wewe waliokuwa zanzibar enzi za sultan iyupi tabidi tukuulize vyema yafuatayo
1. wewe umewahi kufika zanzibar, au uliogopa kwenda huko usije ukafanywa mtumwa?
Bin Faza,
Najua wewe ni msomi mkubwa mno tena ulobobea. Lakini menitia simanzi kiduchu,kuona zile propaganda za makhanatha ya Wazungu ati Utumwa ulifutika duniani/Zanzibar pale tu ati wao Wazungu walipokataza/walipoufuta...si kweli asilan!
Tunajua yakuwa Utumwa uliendelea kwa decades nyingi mbele ya lile tamko.
Mifano ni palepale Uk penyewe palikua na utumwa mwingi ukiendelezwa dhidi hata ya watoto under ages na families zao khasa kule Wales na Ireland.
Sasa kipi wewe kikuthibitishie yakuwa ati utumwa ulikwisha,pale tu Mwingereza/Wazungu walipotangaza au kusitisha!?
Kama wao Waingereza/Wazungu walishindwa kuzima huo utumwa na udhalimu ndani ya nyumba/Taifa lao,kipi kinakufanza wewe uone yakuwa their implemetation was so effective to that extent!?
Takupa mfano mwingine kiduchu;
Sehemu na pahala pengi mno khasa;some parts of Afrika,Indian sub-Continent,middle east, Carribean Islands utumwa uliendelea as early as 1950's...tena huku serikali ya Uingereza ikijua kwa yakini na kufumbia macho. Sababu wengi ya wale waliokua wanamiliki watumwa wale walikua ni familes very powerful/Aristocracies with inherited strong political connections and influences within the Uk and Amerika.
Ahsanta.
Ritz huyu jamaa asikusumbue ana ugonjwa wa yule mjinga mwenzake Yericko unaitwa "amnesia" hasa kipindi hiki cha baridi ndio unawasumbua sana!Wewe acha unafiki hebu hapa jisome mwenyewe mabwana zako hawapo sijui utawaita kina nani.
Mnafiki ni chakula ya mamba, wewe kila siku na ulikuwa unatumia hizi hizi video kama ushahidi wa kumtetea bwana wenu Okello leo eti unasema ya kughushi.
Cc.. gombesugu, Boko haram,