Boko haram
JF-Expert Member
- Nov 7, 2011
- 3,256
- 1,231
Mkuu nakusoma kwa miwani ya 3D ha ha haa waereze waerewe.
Bin Faza,
Salaam.
Mimi nimezaliwa Unguja,tena ni Stone Town/Baghani...na nikifia pale Unguja abadan sitazikiwa Kwerekwe!...na wala sina asili/sitokei ng'ambo,je una jingine!?
Nafikiri ushanifahamu uzuri kama kweli wewe ni Muunguja!?
Unaponambia ati nitofautishe baina ya Mtumwa na House Boy...mie najua uzuri tafauti iliyopo,sijui wewe mwenzangu!?
Ndo maana,kwenye ile post/s yangu kwa ndugu yetu Chabuso, pia nikanena yakuwa wakti mwingine yatulazim kuangalia majambo kwa utuvu wa kina na kitaaluma.
Kwa mtazamo wako wewe Sheikh Bin Faza,Mzanzibary khasa ni nani!?
Na mtu yupi khasa ana-qualify kuitwa Mtumwa tangia zama hizo pale Unguja!?
Lakini penye nilijualo tazungumza japo kiduchu.
Nakufuatilia bayana zako leo takriban wiki kadhaa. Wallahi,wafanza uzuri mno kutufumbua macho wenzio.
Nafikiri unachoharibu kiduchu,ni vile unapojaribu kila mara kuonyesha yakuwa wale Waarabu/ma-Sultan walikua ni kama vile Malaika wakti wa utawala wao pale Zanzibar!?
Usinifanze nikashindwa kukutafautisha na hao jamaa zako wa ki-bara/Watanganyika humu Jf...maana na wao wanawaona Wazungu kama vile ni nusu Miungu na kuwaabudu mno huku wakichukia Waarabu bila ya sababu zozote za msingi!?
Ahsanta kwa kunisikiza.
ahsanta.
Cc Ritz