Haya ndio Mapinduzi ya Zanzibar, yamerikodiwa live na waitaliano 1964


RED Xs,

Vipi ndugu yangu,yale maafa ya 1964 wewe ndo unaita mapinduzi matukufu!?...khalaf wewe ndo unajinasibisha na Ungazija kweli,au ndo wale Wangazija pori!?

Sasa wewe unamstaajabu Bin Faza,khalaf nawewe si ndo unafanza yaleyale!?

Takriban watu 20,000 kupoteza maisha yao katika siku chache mno ikiwemo; virongwe,watoto,walemavu, wanawake wajawazito...khalaf wewe ndo unaita ati hayo ni mapinduzi matukufu!?

Jingine nakusihi jitahidi uondoshe hiyo mifano ya kidini hapa jamvini,maana italazim wengine kukujibu matokeo yake ghafla jamvi lote litachafuka. Kama wewe ni "Muislamu",basi tumeshakusikia!

Jitahidi kuulindia hishma na hadhi yake huo usomi wako ndugu yangu!

Ahsanta.
 
RED Xs


Kwa hisani yako fungu akitabu kiitwacho ZANZIBAR TRADITION AND REVOLUTION kilondikwa na ESMOND GRADLEY MARTIN, published by HAMISH HAMILTON (LONDON) ISBN 0-241-89937-0 MWAKA 1978

soma p25

ripoti ya Marco Polo kuhusu zanzibar ilisema hivi.....zanizbar wakaazi wake ni weusi awana nywele za singa...

sasa pingana na hao wazungu

walipofanya mkutano wa ujerumani wa kuigawa afrika, wakazichukuwa sehemu zote za zanzibar isipokuwa wakaawachia visiwa vya unguja na pemba, mombasa na mafya na fukwe yote ya east afrika kama inavoonekana katika ramani hii ya 1886



kama unaweza kupingana na wazungu sawa

ukitaka kujuwa zaidi uliza tu
 
gombesugu


hawa wana sababu zao lakini hawana uwazi wanaogopa kusema hasa yalioko moyoni mwao
 
..umefatilia mjadala wangu na kaka yangu bin faza toka mwanzo au unarukia tu...!
 


Wajua Faza;
1. hii sii mada ya watu kukubaliana kirahisi. Lives have been lost

2. Binafsi nadhani kama mko-organized na mkaona haja ya kushtaki kuwa hiyo itajwe ilikuwa GENOCIDE why NOT? Nyie mtakuwa mnaishitaki Tanganyika/Tanzania? etc... hamumushtaki Nyerere. Office ya Jamhuri ndiyo itakayosimama kuwajibu huko Hague. Kama mnashitaki bora mkajipanga mfanye hivyo kuliko kukaa mnaumia roho. Nachoona mimi mnafanya kumpuuza huyo mwenyeji wa mwenyeji wa Watanganyika. Yeye ndiye mshatakiwa # 1.

For some reason yeye hamumtaji
 
..umefatilia mjadala wangu na kaka yangu bin faza toka mwanzo au unarukia tu...!


Sikurukia wala sikudandia, nimekuulizia kitu specific...umetumia neno "mapinduzi matukufu" pale ulipozungumzia yale maafa yalotukuta ile 1964.

Khalaf,unajinasibisha na Ungazija...ndo nikakuuliza au wewe ndo wale Wangazija pori!?
 


Kaka; Unapotaka kuipindua serikali, lazima UENDE KWENYE THE SEAT OF POWER. Huwezi kupindua Kenya kwa kuhangaika na Voi, Unalenga Nairobi (Cabinet), huko kwingine kama.....pemba, unajenga utilivu tuuu na utawala. Hupindui bongo kwa kuhangaikia babati una-target the seat of POWER dar. Kwa zenj the seat of POWER ilikuwa Unguja. Ni logical wapinduaji waende pale,Faza. Vipi uhangaike na pemba kabla hujaitia serkali kibindoni?
 
sawa sawa Faza, lkn bado kulikuwa na mkono wa wazenji asili kwenye hiyo massacre, kwa hiyo hupaswi walaumu bara peke yao as if kila kitu tuli plan sie, upo hapo mkuu, no need kujitenga bro let us all together sought out haya matatizo tuwe wawili wamoja pamoja as you can see kuna mwanga tunapoenda, ee bwana. Tunawapenda
 

hahahaa Mkuu siandika kwa hasira labda wewe unasoma kwa hasira,lakini mbona unaniuliza private life yangu?mimi sijakuuliza hata swali moja kuhusu wewe unatoka wapi,au wewe nani,kwafupi sikuhadithii wewe chochote kuhusu zanzibar isipokuwa zanzibar ninayoijua mimi naifanananisha nahistoria ya USA.

Wako walioandika historia ya zanzibar kuwa watu wazanzibar ni watu wa Tanganyika,wako waliosema kuwa watu wazanziabr ni warabu,lakini kutokana na uwazi wa information tuliokuwa nao sasa ni kujua wazanzibari ni watu gani

Historia inasema kuwa wzanziabr waliwaita warabu kuja kuwasaidia kuwaondoa wareno,je hawa watu waliowaita warabu walikuwa akina nani?tuanajua kuwa makabila ya pwani kama wasegeju,wazaramo na makabila mengine yanayoishi kwa kuvua kando kando ya pwani ya afrika mashariki wanautamaduni wa unaoitwa kulala "Dago",wavuvi hawa walikuwa wanalala zanzibar,tanganyika, nk utamaduni huo uko mpaka leo

Kwa muono wangu, wazanzibar wa mwazo walikuwa watu kama hawa,ni watu waliokuwa wakiishi kando kando ya afirka mashariki na kulala "Dago" sehemu mbali mbali pembezoni mwa ya pwani ya afrika mashariki,watu kama wasegeju,wazaramo,wadigo,wasomali,wazugua,wagunya nk ,watu hawa baada ya kukaa kwa muda mwingi sehemu ndogo kama zanzibar na kuchanganya na makabila mengine yaliyokuwa si ya kiafrika kam vilé wachina,warabu.wahindi,wapersia,wareno nk, utamaduni,mila,hulaka za washahili wa zanziabar zikazaliwa

Wazee wa bibi wa bibi yangu ni wazigua na wagunya,hawa ndio waliomwita mwarabu kuja kuwasaida kuwaondoa wareno zanzibar,wewe Je,twambie wewe unatoka wapi? 🙂
 
Ndo maana wanaambiwa kuwa uhuru ulipatikana 1964 lakini wanabisha.
 
Sikurukia wala sikudandia, nimekuulizia kitu specific...umetumia neno "mapinduzi matukufu" pale ulipozungumzia yale maafa yalotukuta ile 1964.

Khalaf,unajinasibisha na Ungazija...ndo nikakuuliza au wewe ndo wale Wangazija pori!?
Duh!ujio wa waarabu kwa kweli una madhara kuliko mazuri kwenye bara letu la Africa hususan Zanzibar na maeneo ya mwambao wa Pwani ya Afrika mashariki.
 



wametudhulumu sana....iko siku
 
Tusichanganye mambo documentary si kitu cha kurekodiwa ni kaz inayotokana na ethnography na kwa mantiki hio inaweza kuongezwa au kupunguzwa tusipotoshwe na rangi kwani hata hip hop ngum ya leo imewezwa kutayarishwa ktk nadharia ya kuonyesha ni yabzamani rusiwe wavivu wa kufikil na lazima ruchunguze kwa makini mambo tunayoletwa na wagen tupo ktk nyakati ambazo kila taifa linataka kuwa kubwa tusome zaid nakufanya tafiti wakati tukiwa katika maswala ya muungano kumekuwepo documentary nyingi za mwarab,mfaransa,mwingereza na wengine wengi lakin nini wanachokitaka kwanini wanatumia technolojia kutupotisha na maredio makubwa TANZANIA NI YETU SISI NDO TUNAIJUA KULIKO WAO WASITUFUNZE MAMBO YALIYOFANYWA NA BABA ZETU KWASABABU TUNAYO NA TUNAYAJUA. Hao wanasiasa uchwara wanatumia hizo documentary kuwapotosha watanzania na hao wenzetu wavivu wa kufokilu MUNGU IBARIKI TANZANIA
 


Gombesugu; I dare say huyu REDx kajiandaa sana na hoja za kimantiki in a very EDUCATED approach manner. wewe ni scholar please mjibu kama alivyojieleza, that will be fair. Is it true Sultan wa Oman kwenye Berlin Conference alikuwapo? na because of that akapewa hilo pande la ardhi toka Mogadishu hadi Beira? Bin Faza, hebu hata wewe toa Msaada, ni kweli?

We know for sure MKWAWA, SINA, KIMWERI hawakuwapo, there should be a reason?

Gombesugu achana na Ungazija wake huyu bwana. Ukipoteza muda kwenye ungazija wake hutakumbuka point za kumjibu

cc RED Xs, Bin Faza,
 
Hayaja rekodiwa live ni documentary sahihisha usemi wako na nidocumentary iliyotengenezwa kujibu waingereza na serikali ya bara.Imetengenezwa na waarabu na wafaransa unategemea nini soma zaid uliza wazee watakusaidia please narudia si live fikiria hali ya kisiasa iliyokuwepo kati ya mfaransa,mwarabu na mwingereza juu ya umiliki wa makoloni. Ukiangalia ya waingereza nayo inaonyesha ubaya wa waarabu TUWEMAKINI TUTAPOTOSHA UMMA
 

Afro; Ile documentary ni Filamu inaitwa AFRICA ADDIO. Ilitustua tu baadhi ya mambo fulani. We now know ni film sio live event. You can access hii link na kuona the original title

‫
 
okello alishesema mwafrika hana shukrani. Zanzibay sijui kwa nini hawasusii sherehe za mapinduzi kama mapinduzi ni mabaya kwao.
 
Sikurukia wala sikudandia, nimekuulizia kitu specific...umetumia neno "mapinduzi matukufu" pale ulipozungumzia yale maafa yalotukuta ile 1964.

Khalaf,unajinasibisha na Ungazija...ndo nikakuuliza au wewe ndo wale Wangazija pori!?
.....ashakhum.....wangazija pori maanaake nini kakaangu? mbona unakuwa na kauli kama za watu wa tabia ya "kijinsia ya elton john"...? ulianzia mwanzo wakati nilipozungumzia ubaya wa matumizi ya silaha bila kujali nani anaitumia? bila kujali kama ni jambazi, polisi, wapigania uhuru, wa polisario, ANC,SWAPO, FRELIMO, UMMA PARTY (YA ZANZIBAR0) PLO?...wenye kuelewa tunalaani matumizi ya aina yoyote ya silaha sbb ya matokeo yake..!matumizi ya silaha hayana heri popote yalipotokea, iwe unguja, iwe rwanda, iwe palestina, iwe kosovo, iwe libya..!wanawake , watoto na vikongwe ndio muhanga wakuu wa matumizi ya silaha..! kilichotokea zanzibar kimetokea kila sehemu duniani ambapo watu waliamua kushika na kutumia silaha..! hatufurahii, lkn hatukubali kuwa chini ya ukoloni..! kama una uelewo wa qur'an tukufu soma ktk 8:25 ya qur'an, tafuta na tafsir ya ayah hiyo kisha tafakari kilichotokea unguja mwaka huo wa 1964...kisha tafakari..! mungu awarehemu wale wote waliodhulumiwa nafsi zao kila mahali hapa duniani, hususan ktk afrika na palestina..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…