Haya ndio Mapinduzi ya Zanzibar, yamerikodiwa live na waitaliano 1964

Wickama,

Salaam ndugu yangu.

Haina neno,kama siku zoote nisemavyo yakuwa sisi soote ni wamoja.

Ndo maana pia ni uzuri kuambiana kweli pale inapojiri.

Vipi Mfalme Obama kishaingia hapo,je atafika Mtae!?ahahaa!

Siku njema.

Ahsanta.

Ustadh huku labda aje na zile APACHE helikopers, kwa yeye atavaa T-shirt kwa hali ya hewa lakini kwa wenzangu wa Bongo watavaa Maka-buti hahahahah

karibu bwana
 
Wickama

Faza; Hapa kwa kweli mimi Napata Darsa ya kunisaidia kuwaelewa huko mliko kwa hiyo wajibu wangu mkubwa kwanza ni kusikiliza tuu.

shukran sana

sawa mkuu wewe sikiliza tu , ukiwa na suala uliza wamo humu watakaokupa jawabu uruwa kabisa

tatizo ni pale mtu mkimya akianza kuzungumza

wazanzibar tumevumilia kwa miaka 50, tumenyamaza ijapokuwa tunaumia roho

leo usijali maandishi ya humu kaka, hapa tunazungumza sisi wasomi wenye maisha yetu , nenda unguja au pemba uingie dala dala zetu uwasikilie raia walala hoi wanavosema, utajuwa kweli sasa watu wamechoka......nyinyi watanganyika mutakiwa kujuwa kwamba mukila na kipofu usimshike mkono ....atajuwa kwamba upoo...au vipi
 


Kazi kweli kweli. Haya niombee Mungu Inshallah siku moja nitafika. Ila sijui mtaniita vipi? Mtanganyika PORI? hahahahah
 
Kazi kweli kweli. Haya niombee Mungu Inshallah siku moja nitafika. Ila sijui mtaniita vipi? Mtanganyika PORI? hahahahah

mbona hamna neno kaka, labda uende umevaa shati lenye chapa ya ccm, ndio kidogo wanaweza kukuona umeanza kuuguwa uchizi
 
mbona hamna neno kaka, labda uende umevaa shati lenye chapa ya ccm, ndio kidogo wanaweza kukuona umeanza kuuguwa uchizi

Ahhhh, haitagomba kwa vile rais wa zenj naye anayavaa na antoka huko basi tutampa kampani hahahah, machizi kama wanatukana waanzie wakwao.
 
..lol..nashukuru kaka..tutaendelea siku ingine na mjadala wetu..nimebanwa na pilika..insha allah ramadhani njema..!
 
Haya mapinduzi ya Zanzibar tuliwahi kuyajadili kwa kina sana hapa jamvini miaka takriban saba iliyopita na tukaweka video pamoja na documents nyingi sana. Ingekuwa ni vizuri MODERETA akarahisisha kazi ya kutafiti topiki kusudi wachangiaji wapya wawe wanaongezea kwenye topiki iliyopo badala ya kuanzisha thread mpya. Mambo mengi yaliyoandikwa hapa yaliwahi kujadiliwa na kupatia maelezo ya kina huko nyuma. Najua waanzisha mada ni watu waliojiunga na jamvi hili miaka michache iliyopita, lakini si vizuri kuanzisha thread kiholela badala ya kuendeleza zile zilizoko.
 
Du!, kumbe inawezekana kabisa yale Mapinduzi ya Zanzibar sii mapinduzi tuu, bali ni Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyoleta utukufu fulani?!.

Pasco
 
Mkuu Wickama asante kusaidia kwenye hili, vinginevyo watu wanalishwa urongo humu mchana kweupe na wanaingia kichwa kichwa!, wazima wazima wanaingizwa chaka!.

Thanks.

Pasco
 
Weye ni ktk wale majuha mnaodanganywa kuukataa ukweli, lete ushahidi kuhs ayo usemayo, aya mambo ya mauwaji ya waarabu sisi tulishayasikia zamani ktk kwa mababu zetu na ukweli ulifichwa na ukageuzwa na mpaka history maskuli hausomeshwi ukweli, mnaodanganyika ni mbumbumbu kama ivo nyie, biashara ya watumwa ilifanywa na wazungu tafuta ukweli usome acha kupotolewa
 
Kuna mengi yalitokea yamefichwa ila hili la John Okelo na Mohamed Babu ni aibu kwa sirikali kuficha mchango wao waliofanya katika mapinduzi ya Zanzibar
 
Hizi ni sinema za kutungwa kutengeneza propaganda.
BADO TULIO YASHUHUDIA MAPINDUZI HATUJAFA. YALIOLEZWA HUMO SIO TU NI UKWELI BALI NI CHEMBE NDOGO SANA TU YA YALE WALIOYAONA

NAKUMBUKA VIVIDLY TANGAZO LA REDIO KUKEMEA NDEGE KADHAA ZILIZOKUWA ZINARUKA KWENYE ANGA YA ZANZIBAR. WAKATI HUO SIKUJUA TU NINI KINAENDELEA KUTOKANA UMRI WANGU. NILISIKIA PIA WAKITAKIWA WAPIGANAJI WASIWADHURU WAZUNGU. HILI NILILIJUA KUWA KUNA MELI YA KIJESHI YA MAREKANI IMEEGESHA KUJA KJUCHUKUA RAIA ZAKE. hakuna cha kutungwahapa. Moja ya kaburi kubwa la halaiki liko kibanda maiti, sasa umegeuzwa jina uwanja wa demokrasia,na sisi wenyeji tunapaita makaburi msafa. Msichangie jambo msililijua. ACHENI TUMALIZIKE,TENA MNAWEZA KUTUNGA HADITHI MZITAKAZO NA KUZIHAKIKI DODOMA. VUTENI SUBIRA KWANZA.
 
Uongo mtupu na povu jingi.
 
Hakika napenda sana kusoma news aina hii.kwanza natoa pongezi sana kwa mleta uzi na pia kwa wachangiaji wote.hongereni sana kwa ilmu yenu tamu.la mwisho ningependa kusema WANZANZIBAR WACHACHE WAPO HAWAJIELEWI NA NDIO WANAORUDISHA NYUMA UHURU WAO.poleni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…