Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
Mkuu hizo thamani za score na pesa ulizoweka vinalingana?Kiswahili - A,
English - A,
Maarifa - B,
Hisabati - A,
Science - A,
Uraia - B,
Average Grade - A
Amemaliza katika shule ya English medium
Mimi baba yake ni kichwa zaidi yake ila matokeo yangu hayakuwa mazuri Kwa sababu ya hali ya maisha magumu ya familia yangu
Ni kama vile nilikuwa najisomesha mwenyewe maana sare za shule na viatu nilivyo nunuliwa na wazazi ni zile nilizovaa siku napelekwa kuanza darasa la kwanza Baada ya hapo nilijinunulia mwenyewe Kila kitu hadi namaliza darasa la saba
Huko secondary na advance ndio kabisa nilikuwa nauza maji Ili kupata naurli ya shule na mahitaji mengine ada zote nimelipa Baada ya kumaliza advance ndio nakachukua vyeti vyangu ada ilikuwa elfu 20 Kwa mwaka lakini bado familia yangu ilishindwa kulipa
Ila bumu la chuo ndio lilinifariji na kunifanya nisome chuo bila ya stress
Ila elimu niliyoipata sio elimu Bora naamini hilo 100% Yani nilikuwa nafaulu tu Kwa sababu Nina akili nyingi
Nikajiapiza watoto wangu sitaki wapitie haya na sitaki wasome kayumba kama Mimi baba yao
Mimi sitaki kukuvunja moyo lakini nataka ufikirie namna hii.
Je hapo alipo akimaliza anaweza kupata kazi? Kama umelipa ada let say milioni moja kwa mwaka je hayo matokeo yanaleta impact gani?
Hizo milions ungenunua ardhi akimaliza Form 4 atakuta ina thamani takriba milioni 50+
Then unawekeza pesa ndefu kwa mtoto ambaye akimaliza anakuja kutembeza bahasha kutafuta Mshahara wa Laki Saba?
Unless wewe ni Mlamba Asali and ofcourse Walamba asali ndio wanaosomesha shule za ghalama ila kwa sisi wavuja jasho ni bora tuwekeze kwenye biashara wapate cha kurithi baadae.
Hongera kwa Mwanao amezingatia masomo kwa bidiii na unatakiwa usimvunje moyo aendelee hivyo hivyo.