Haya Ndio Yanachelewesha Mafanikio Yako

Haya Ndio Yanachelewesha Mafanikio Yako

Dah kwa Idadi ya wavivu na Wazembe walioko Tanzania Nafikiri Tungekuwa Matajiri ni 50 Percent na 50% ya Invention zingekuwa Tanzania.Unless uniambie kwamba Tanzania hakuna Wavivu na Wazembe
Mimi nimemuelewa vizuri sana jamaa pointi yake na yuko sahihi.
Amemaanisha wavivu na wazembe walio smart kichwani,maana unaweza kuwa mvivu na kichwani zero hakuna unachokiwaza hapo utaendelea kuwa maskini wa kutupwa.
Wakati sisi tunalima shamba kwa mikono yetu mzungu kwa vile ni mvivu na yuko smart kichwani akabuni trekta ili kurahisisha kazi ya kilimo.
 
Zote ni sababu za kuparazia ..

Point kubwa ni utegemezi mkubwa kutoka kwa wazazi na familia kama unatokea famili za kimaskini hata ukiwa na ajira na biashara ndogo ndogo ....Jiandae kurudi nyuma unakuwa na mzigo wa wategemezi mapema.
 
Habari za wakati huu;

Ni matumaini yangu kwamba unaendelea salama na shughuli za ujenzi wa maisha yako na taifa kwa ujumla.Leo nachokoza mada kuhusu mambo ambayo huchelewesha mafanikio ya mtu.Ni matumaini yangu kwamba mjadala huu utakufanya uweze kuona mwanga na kuchukua hatua stahiki.

Karibu tuendelee;

Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuchelewesha mafanikio ya mtu, na hali hizi zinaweza kutofautiana kulingana na mtu na muktadha. Hapa kuna baadhi ya mambo yanayoweza kuchelewesha mafanikio ya mtu:

  1. Kukosa malengo wazi: Kutoweza kujua ni nini unataka kufanikisha au kutoweka malengo wazi yanaweza kusababisha kutofautisha jitihada zako na kuelekeza nguvu zako kuelekea kufanikisha kitu fulani.
  2. Uzembe au kukosa bidii: Kutokuwa na bidii au kuwa mzembe katika kazi au juhudi zako kunaweza kusababisha mafanikio kuchelewa au kutofanikiwa kabisa.
  3. Kukosa ujuzi na elimu: Katika baadhi ya kazi au malengo, ujuzi na elimu ni muhimu sana. Kukosa ujuzi wa kutosha au elimu kunaweza kuchelewesha mafanikio.
  4. Hofu ya kushindwa: Hofu ya kushindwa au kukata tamaa inaweza kumzuia mtu kuchukua hatua muhimu kuelekea mafanikio.
  5. Kukosa mtandao na uhusiano mzuri: Mtandao wa kijamii na uhusiano wa kitaalamu unaweza kusaidia kufanikisha malengo. Kukosa mtandao mzuri kunaweza kuchelewesha mafanikio.
  6. Kukosa nidhamu na usimamizi wa muda: Kukosa nidhamu katika kusimamia muda na rasilimali zako kunaweza kusababisha kucheleweshwa kwa mafanikio.
  7. Matatizo ya kiafya au kibinafsi: Matatizo ya kiafya au kibinafsi yanaweza kusababisha kucheleweshwa kwa mafanikio. Hali za kiafya au matatizo ya kibinafsi yanaweza kumzuia mtu kufanya kazi kwa ufanisi au kufuata malengo yake.
  8. Mazingira yasiyofaa: Mazingira ya kazi au maisha ambayo hayasaidii kufanikisha malengo yako yanaweza kusababisha kucheleweshwa kwa mafanikio.
  9. Kukosa motisha: Kukosa motisha au shauku ya kufikia malengo yako kunaweza kusababisha kucheleweshwa kwa mafanikio.
Kwa kawaida, kucheleweshwa kwa mafanikio hakumaanishi kwamba mafanikio hayawezi kufikiwa. Inaweza kuwa ishara ya kutafakari na kurekebisha mambo fulani ili kuongeza nafasi za kufanikiwa. Ni muhimu kutambua sababu za kucheleweshwa na kuchukua hatua za kuboresha hali hiyo ili kufikia mafanikio yako.

Kama kuna mambo mengine ambayo yanaweza kuwa yanachangia kuchelewesha mafanikio unaweza kuyaweka hapa ili tuyajadili zaidi

Bless
 
Mkuu,Staying alive,Healthy,Happy and Free ni Moja kati ya Mafanikio ambayo naweza kuyaweka kama mfano Mengine ni chachu tu hata nikiyaweka hayatabadili kitu katika msingi wa hoja yangu

Hapo kwenye happy and free wengi ndio tumekwama.
 
Tatizo la Tanzania elimu yetu haileti "critical thinkers" or obstruct thinkers mambo mengi yanao andikwa ni ya kawaida sana
Kwa sababu elimu yetu haiko practical oriented ni vitu tunakaririshana miaka na miaka lakini hakuna aliyewahi kuvijaribu au kuvitumia akaona matokeo.
Unakuta Lecturer wa Business Studies ana Phd na anajiita mbobezi wa masuala ya biashara lakini hajawahi kufanya biashara hata ya kuuza pipi au karanga.
 
wapo wavivu 10% na wazembe 20% alafu asilimia zinazobaki wapo wachapa kazi kama walimu, wanajeshi, na wakulima, nk hawa watu wanajituma sana ila mafanikio yao ni gari na nyumba unajua kwanini kwasababu hawawaz nje ya mifumo yao ya uchapa kazi tuje kwa wavivu hawa wapo na wanamafanikio ila baadhi yao kwa hapa nchini target zao hazifanikiw kutokana na mifumo...ya mazingira ya nchi yao, na hawa wazembe wapo kama hawa ma mc,chawa kama kina baba levo, madalali, matapeli, na hata kina mo nawaweka kwenye kundi la wazembe, usiniulize kwanini sugua kichwa bro kwanza elewa maana ya maneno in deep toka hapo utakuwa na uwezo wa kujenga hoja japo hujanielewa ila naeleweka
Nakubali na hoja ndio maana nyerere aliu dislike ubepari baada ya kuona Kuna wazungu kazi Yao kubwa ilikua kuzunguka Shambani akasema ukiwauliza wao ni wakinani walisema wao ni industrist nyerere akasema haiwezekani huu ni wizi akaenda zake ujamaa matokeo yake ndio haya.
 
Kwa sababu elimu yetu haiko practical oriented ni vitu tunakaririshana miaka na miaka lakini hakuna aliyewahi kuvijaribu au kuvitumia akaona matokeo.
Unakuta Lecturer wa Business Studies ana Phd na anajiita mbobezi wa masuala ya biashara lakini hajawahi kufanya biashara hata ya kuuza pipi au karanga.
Ila hii noma sana
 
Back
Top Bottom