Haya ndiyo mambo ya ajabu niliyowahi kuona na kushuhudia kwa macho yangu, sitoyasahau katika maisha yangu

Haya ndiyo mambo ya ajabu niliyowahi kuona na kushuhudia kwa macho yangu, sitoyasahau katika maisha yangu

Mimi natoa Mikasa ambayo nimekutana nayo na nimeshuhudia kwa macho yangu Kama Kuna mtu anaona kuwa hizi ni stori za kutunga basi shauri yake.

Lakini haya ninayoyazungumza Kuna lakujifunza ndani yake hii dunia ni pana sana nitaendelea kutoa au kushea nilivyoviona katika huu ulimwengu .

Kama Kuna mtu pia yalishawahi kumtokea makubwa zaidi ya haya pia asisite kushea ili tuendeleee kupanua ubongo.

(9) SITOSAHAU NILIVYOKUNJANA MASHATI NA WAOSHA MAITI NDANI YA CHUMBA CHA MAITI.

Hii ilitokea mkoa wa pwani, nilipo mrudisha babu yangu mzaa mama nyumbani kutoka hospital aliuugua kwa muda mrefu tulimuuguza sana mwisho wa siku alikata roho.

Pale mtoto wa kiume nilikua nipo Mimi ndiyo mjukuu mkubwa wengine walikua bado hawajafika kutoka mjini, Sasa ilibidi tuanze kushughulika na mazishi.

Msiba ni wakiislam, maana babu kwenye uhai wake alikua ni muislam nakumbuka alifariki alfajir mpaka saa kumi na mbili hivi saa moja moja nilikwenda kutoa taarifa msikitini.

Naam mchakato ulianza walikuja wazee wa makamo watatu wao kazi yao nikuosha maiti nilielewana nao nikawalipa waanze kazi yao yakuosha pamoja na maandalizi ya ushonaji wa sanda.

Utaratibu uliendelea, maiti ya mzee iliwekwa juu ya kitanda Cha kamba, Hilo zoezi lilikua linafanyika ndani ila chini yakitanda palichimbwa shimo ili Yale maji ya maiti au fuo yamwagigikie chini.

Zoezi lilifanyika Kama utaratibu ulivyo na Mimi sikua mbali nilikua karibu sana na waosha maiti kuhakikisha zoezi linakwenda sawiya.

Sasa basi zoezi lilifanyika Kama lilivyopangwa cha ajabu walipokua wanamuosha mzee pale chini ya shimo walitegesha chombo Kama kibeseni hivi ili kukinga maji ya maiti.

Hilo nililiona lakini sikutaka kuuliza maana wao ndiyo wataalam, ikanibidi niwe mpole kwenye sehemu Kama huwezi kuleta ujuaji na ukiangalia ni wazee wa makamo.

Baada yakukamilisha zoezi lao, waliianda maiti vizuri wakafukia pale chini ya kitanda lakini maji waliyokua wanayakinga waliyaweka kwenye kidumu Cha lita na mengine waliyafukia vizuri kabisa.

Mimi muda huo nilikua nawaangalia nakuwatafakari hawa maji wanataka kupeleka wapi??
Nilijiuliza sana lakini nilijisemea moyoni itafahamika tu.

Walipomaliza shuguli zao, si ndiyo walitaka kutoka nje na Yale maji.
Mimi niliwazuia mlangoni, niliwauliza mnapeleka wapi hayo maji??

Mmoja akajibu tunakwenda kuyaombea, niliwaambia hakitoki kitu hapa toka lini maji ya maiti yakaombewa??

Mzee mwingine alidakia nakusema kijana usijitafutie matatizo tunaomba utupishe tupite!

Kabla sijajibu mzee mmoja alinikunja shati, na Mimi niliona liawalo na liwe tukaanza kukabana ndani ya chumba Cha maiti na nje Kuna watu bahati nzuri kile chumba tulichokuwemo tulikua tumejifungia ndani.

Baada ya hizo purukushani ndiyo mzee mmoja akawaambia wenzake jamani hili la leo lishakua gumu tumuachie hayo maji.

Waliyaacha huku wananikata jicho na waliniambia siku nyingine ukipatwa na matatizo hapa kwenye familia yenu hatuji hata kwa dawa.

Na Mimi niliwaambia sawa.

........................................................................

KWA NINI NILIZUIA YALE MAJI YA MAITI??

nilijua kabisa hawa Kama siyo waganga basi watakua washirikina na Kama siyo washirikina basi watakua wanayataka Yale maji wakayauze.

Nirudi nyuma kidogo Kuna wakati fulani nilikua morogoro masikani tumekaa na washikaji tukipiga stori za hapa na pale.

Alitokea dalali mmoja alituambia kuwa Kuna dili la pesa na dili Hilo Kuna mganga anataka maji ya maiti akafanye Mambo yake lakini dalali hakusema kuwa ni Mambo gani .

Tulicheka nakumpuuza mana hiyo dili ilikuwa ya Moto kwa vijana Kama sisi pale tusingethubutu kabisa kuanza kutafuta maji ya maiti.

Kutoka na mfano Kama huo nilijifunza kuwa maji ya maiti ni dili sana yanatafutwa na waganga kila kukicha au washirikina na kwenda kufanyia Mambo yao huko wanayoyajua.

Ndiyo maana nilikua mkalisana nakufikia hatua kukunjana mashati na wale wazee ndani ya chumba Cha maiti,

Hapa Kuna funzo ni muhimu sana Kama umepatwa na msiba na mtu wako wakaribu basi kuwa karibu sana maana Kuna Mambo ya ajabu hutokea pale msibani anaweza akalifanya hata ndugu yako wakaribu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Yale maji yanauzwagwa bei juu sana,, wateja wakubwa ni waganga,, sasa wamama wanapoenda kwa waganga kutafuta dawa ya kuwashika waume zao, hupewa hayo maji kwenye kichupa kidogo kama cha ppf ya sindano,
So mama anapewa maelezo ya kuchanganya kwa chakula cha mume, akila tu basi anakuwa kama kondoo, hafurukuti kama maiti mbele ya mkewe,, 🤷
 
Yale maji yanauzwagwa bei juu sana,, wateja wakubwa ni waganga,, sasa wamama wanapoenda kwa waganga kutafuta dawa ya kuwashika waume zao, hupewa hayo maji kwenye kichupa kidogo kama cha ppf ya sindano,
So mama anapewa maelezo ya kuchanganya kwa chakula cha mume, akila tu basi anakuwa kama kondoo, hafurukuti kama maiti mbele ya mkewe,, [emoji1745]
Duh hatari sana kumbe tunalishwa vingi sana.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Yale maji yanauzwagwa bei juu sana,, wateja wakubwa ni waganga,, sasa wamama wanapoenda kwa waganga kutafuta dawa ya kuwashika waume zao, hupewa hayo maji kwenye kichupa kidogo kama cha ppf ya sindano,
So mama anapewa maelezo ya kuchanganya kwa chakula cha mume, akila tu basi anakuwa kama kondoo, hafurukuti kama maiti mbele ya mkewe,, [emoji1745]
Haya mambo kama hayajawahi tokea kwako unaweza hisi ni story ila yamewatokea watu wangu wa karibu kabisa toka nitoke kiukweli niya kusikia tu.
 
(7) SITOSAHAU TULIVYOKIMBIZWA KWA PANGA NA MZEE MMOJA WA MAKAMO BAADA YAKUCHUKUA PESA ZAKE ZA CHUMA ULETE.

hizi siyo stori za kutunga nahadithia vitu halisi nilivyoviona kwa macho nakuvishuhudia na wala siyo stori zakusadikika.

hii ilitokea dar es salaam sehemu moja panaitwa kitunda kipindi hicho miaka ya 2004 hivi pale kitunda ilikua bado kabisa ni bushi kiufupi palikua hapajachangamka

Mimi na mwenzangu tulikua tunatabia ya kwenda kuwinda mabondeni ukivuka barabara ya ng'ombe unapita kwenye bonde moja walikua wanafuga sana nguruwe panaitwa kwa mama Tyson.

Tulikua tunavuka pale Kisha tunaelekea kwenye poli la jeshi kwa wanaolijua hili eneo nafikiri watakumbuka namna gani pale mwelekeo wa jeshini kulivyokua na kichaka.

Tulikua na akili za kitoto, tulikua tunakwenda kuwinda ndege, nakuchuma matunda fulaani yanaitwa mabungo.

Sasa bwana katika pita pita vichakani niliona chungu kikiwa kimefunikwa na kitambaa cheupe na chini pia kimewekewa kitambaa cheupe lakin kwenye shingo ya chungu kimezungushiwa hirizi zilizovikwa Kama cheni.

Nilimuita mwenzangu, alikuja akaona Kisha tukatoka kwa kukukimbia kwenye lile eneo mwenzangu alikua ni muoga alisema ule ni uchawi.

Tulifika mbele tulikaa Kisha tukatafakari mule ndani Kuna Nini???
Kila mmoja wetu alitaka kujua kwenye lile chungu Kuna kitu gani??

Basi tukashauriana tutafute mti mkubwa twende kwenye eneo la tukio tukifika pale tuusukume ule mtungi uliokuwa umefichwa kichakani ili tujue ni Nini kipo ndani yake.

Tulipofika eneo la tukio, mwenzangu alikataa kushika ule mti ilinibidi nishike Mimi nakuanza kusukuma ule mtungi kwa kutumia mti mrefu.

Mtungi ulikua mzito kuanguka na kila nilipokua nautikisa nasikia sauti ya mlio Kama vyuma vinagongana ndani yake, basi nilifanikiwa kuuangusha chini, na tukaona chenchi nyingi sana zinamwagika mia mia hamsini hamsini na shilingi kumi pamoja na ishirini ishirini.

Tulitazamana na rafiki yangu kwanza, Kisha tukazifuata zile hela maana yalikua ni machenchi mengi, nilivua fulana langu tukaziweka zile chenchi Kisha kile chungu tukakiweka Kama kilivyokua tukaondoka eneo lile.

Zile pesa tulikwenda kuzificha sehemu kwa kuhofia wazazi wakituona na hizo pesa lazima wangehoji tu, tulitafuta sehemu tukazificha tukawa tunatumia kidogo kidogo ikawa ni Siri ya watu wawili

Ile pesa tuliitumia ikaisha baada ya wiki Kama mbili, kwa sababu tunajua ni wapi tulizipata tuliamua kurudi Tena Safari hii hakuna mwenye uoga.

Na tulipofika eneo la tukio kweli tukakikuta chungu kipo vile vile hatukutaka hata kuchukua mti Kama ulivyokua mwanzo , tulifika tukafungua chungu tukakuta chenchi lakini Safari hii hazikujaa Kama mwanzo tukazibeba tukatokomea kusikojulikana.

Nakumbuka hata shuguli zetu zakuwinda katika lile poli laki jeshi zilisimama baada yakua tunakuta pesa za bure tunabeba Kama zetu wala mwenyew hafahamiki ni Nani.

Sasa baada yakukaa wiki moja rafiki yangu akanipitia tena, twende tukachukue pesa kwenye chungu,

Tulipofika katika lile eneo Kama kawaida yetu akili zinawaza pesa tu na hakuna kingine.
Tukiwa tunajiandaa kufungua chungu Mara gafla tulishitushwa na sauti ya kiume iliyokua inatokea kichakani Tena akija huku anakimbia kuja eneo letu ambapo chungu kipo.

Alisema "nilikua nawasubiri kwa muda mrefu kumbe ni nyie wapumbavu'

Alikua ameshika panga ni mzee wa makamo alikua amevaa kibarakashea aise tulipo muona anakuja kasi huku kashika panga na sisi tulitimua mbio kila mtu na njia yake hata sikukumbuka rafiki yangu alipitia wapi maana ilikua ni kila mtu akijaribu kuokoa nafsi.

Jiioni nilikwenda kumtembelea rafiki yangu nikamkuta kwao na yeye alikua ana wasiwasi labda mim nilidhurika, basi hatukwenda Tena tangia hapo ila nilisimulia juu ya zile pesa watu wakubwa walisema ni chuma ulete ya huyo mzee zile pesa zilikua zinajaa pale ni Kama ndiyo benki yake ile.

KITU KAMA HIKI NILIKUTANA NACHO MOROGORO KWENYE MASHAMBA YA SUA.

nilikua natoka chamwino kuelekea kisanga kwa miguu wakati ule nilikua naishi chamwino, nakumbuka nilikua Sina hata mia mbovu mfukoni yakupanda daladala na ndiyo maana niliamua kupita shortcut kupitia mashamba ya SUA.

Katika kupita pita kwangu humo mashambani nilipita kwenye mti mkubwa ule mti ulikua upo katikati lile eneo lilikuwa halijalimwa kwa muda mrefu.

Nilipita kwenye ule mti nilishangaa kuona sinia kubwa la shaba limewekewa kitambaa cheupe na chini Kuna kitambaa chekundu.

Halafu juu ya kitambaa cheupe Kuna shilingi mia tano tano nyingi sana za Silva, ni nyingi kweli kweli na pembeni kulikua na kuku mweupe Yule kuku hakjafungwa lakini yupo kama mgonjwa mwenye mdondo na kulikua na udi umewashwa unaelekea mwisho mwisho.

Kiukweli nilipiga hesabu Sina hela mfukoni na hela naziona Kama hivyo nyingi kweli kweli,

Nilifika mpaka kwenye sinia nikazichota kwa mikono miwili Kisha niliendelea na Safari yangu nilizifanyia matumizi ya yangu hakuna lililonipata na pia nilikua jasiri maana nilikumbuka tukio la chungu kule poli la jeshi hatukuzurika.
Uchawi hauendi kwa muhuni leo nimeamin
Et mtu anakuta hela njiapanda anaogopa kupita nayo
 
Sitasahau nilipolala makabulini kisa kutafuta utajili usiku akaja Simba Kwa macho yangu namuona Simba usiku WA manane tena makabulini nikajikaza kiume baada ya mda akaja mtu na gari mpya Huku kafungulia nyimbo ya Rose mhando nibebe na ni usiku nimelala makabulini ghafla akapotea Yani usiku huo niliuona kama nimelala mwaka makabulini utafutaji huu Acha Tu mauza uza kibao
Vp umetoboa au uliteseka bure
 
(8) NILIMSHITUKIA BINTI MMOJA ALIYEKUA ANAJIPAKA DAWA ZA KIENYEJI KABLA YAKUFANYA MAPENZI.

Hii nilikutana nayo kijiji kimoja kilichopo mlandizi kinaitwa kwa DOSA kipo karibu na kambi ya ruvu jkt.

Kama Kuna kamanda alipiga kozi pale bila Shaka atakua anapajua vizuri tu, maana eneo lile makuruta tulikuwa tunapenda sana kwenda huko kulikua Kuna kila kitu unachokitaka.

Sana sana makuruta na serviceman walikua wanakwenda kufuata wanawake na wasichana wa pale huwa hawana hiyana hasa anapokujua we ni kamanda.

Naam, nilikua napiga kozi pale ya jkt katika pita pita zetu huko mashambani nilikutana na binti mmoja mzuri alinipa baada yakumtongoza aliniambia anaishi kwa DOSA.

Nilisubiri nikipata pass hata ya siku kazaa ndiyo nitakwenda kukutana na huyo binti mitaa ya kwao kwa dosa.

Aliniambia anaishi yeye na mdogo wake wazazi wamesafiri kwa hiyo hata nikienda kwao hakuna shida.

Hiyo ilinipa kigugumizi kidogo kwenda kwa binti Tena kwao, lakini kwa kuwa kichwa chini kilisha simama Cha juu hakifanyi kazi na ukiangalia sina pesa yakumpeleka gest maana posho ya jkt ilikua ndogo inakidhi mahitaji yangu madogo madogo.

Nakumbuka siku hiyo nilipata pass ya siku mbili, niliona huu ndiyo muda wa kwenda kukutana na binti wakwa DOSA

Mishale ya saa mbili usiku Yule binti alinipokea nyumbani kwao na alinipeka moja kwa moja mpaka chumbani kwake

Kwa mazingira ya pale nilivyoyasoma niliona ana uhuru sana maana anaishi na mdogo wake aliyekuwa anasoma darasa la nne.

Nilikaribishwa ndani Yule binti alinipelekea maji yakuoga, kamanda nilibadili nguo zangu chapu nikawahi kuoga bafu lilikua lipo nje halafu mazingira ya kijijini ni kiza .

Sasa nilipomaliza kuoga niliona nisiende ndani moja kwa moja nilianza kukagua mazingira ya nyumba kwa usalama zaidi huku muda huo Yule binti nilimuacha chumbani kwake.

Kipindi nakagua nyumba kwa usalama nyuma ya nyumba ili likitokea lolote nijue kamanda najidhatiti vipi au naweza nikakimbilia wapi ili kuokoa uhai wangu.

Kipindi nipo nje nilipita kwenye lile dirisha la binti alilokuwemo ndani ama kile chumba chake alichonikaribisha.

Nilishitushwa na minong'ono iliyokua ikitokea chumbani kwa Yule binti, nikajiuliza mbona anaongea peke yake.

Kwa binafsi nilihisi au Kuna Jambo binti alipanga na mtu muda mrefu watengeneze fumanizi.

Nilisogea mpaka dirishani nikasogeza pazia kwa utaratibu kabisa ambapo ni ngumu hata yeye kuniona maana nyumba ilikua haina umeme na Yule binti alikua amewasha chemli mwanga hafifu kwa kupitia dirishani niliweza kuona nakujua binti alikua anazungumza Nini

Nilimuona binti alishika kibuyu kidogo akiwa uchi wa mnyama na alikua akinuia kwenye like kibuyu Kisha anaweka kilicho ndani ya kibuyu juu ya kiganja chake baada ya hapo anapakaa sehemu zake za siri hicho alichokitoa ndani yakibuyu.

Alifanya hivyo kwa kurudia nakunong'ona Mara tatu ila sikufanikiwa kusikia alichokua ananuia katika kile kibuyu.

Nilipoona vile ilinibidi niende ndani katika hicho chumba alichopo binti,

Nilitaka kuingia bila ya hodi lakini binti alikua amejifungia kwa ndani mpaka nilipogonga ndyo alifungua akiwa amejifunga kanga moja tu.

Nilivyoingia ndani Cha kwanza nilitazama kibuyu lakini sikukiona Hapo ndipo nilipopata wasiwasi nilijiuliza alikua anapaka Nini huyu sikupata majibu.

Nililala na huyo binti, sikusubutu kumgusa kabisa mpaka asubuhi na yeye alishangaa sana mpaka akaniuliza upo sawa nilimwambia ndiyo.

Saa kumi na moja asubuhi nilibeba begi langu, nilimpa Yule binti elfu tano nikapotea , nilikata na mawasiliano mpaka Sasa sijui anaendeleaje.
Hapo ungepiga ungemwaga ubongo
 
Inaonekana una mengi bro
Tungejifunza meng
Yeah Nina mengi lakini Mimi ni mvivu Sana WA kuandika kiujumla kama nikianza kuhadithia Kwa maandishi nahisi mwezi mzima mana nafulia narudi tena nakosea masharti naanguka lakini sichoki kuna siku nilishawahi kutana na mchungaji mmoja Sana maalufu kwa sasa miaka ya 2011 tukapelekwa makabulini tukaitiwa kiumbe kuingia nacho mikataba Acha utafutaji huu mtu akitumia pesa zake muache
 
Binafsi sijawahi kutana na mauza uza labda Moja tu nilitokaga kuangalia UEFA ilikua Madrid na Bayan kitambo tu nikapita mahali nikasikia nywele zimesimama alafu gafla nikasikia jotoo njia ilikua inapita katikati ya mahindi kuangalia pembeni kwenye jiwe Moja hivi kasimama bonge Moja la bundi macho Yana wakaaa aisee nilitoka mbio Moja hiyo uzuri mbalamwezi ilikua inawaka haswa
Hapo umesahau had tokeo
 
Binafsi sijawahi kutana na mauza uza labda Moja tu nilitokaga kuangalia UEFA ilikua Madrid na Bayan kitambo tu nikapita mahali nikasikia nywele zimesimama alafu gafla nikasikia jotoo njia ilikua inapita katikati ya mahindi kuangalia pembeni kwenye jiwe Moja hivi kasimama bonge Moja la bundi macho Yana wakaaa aisee nilitoka mbio Moja hiyo uzuri mbalamwezi ilikua inawaka haswa
😂🏃‍♀️
 
Back
Top Bottom