Haya ndiyo mambo ya ajabu ya taasisi zetu - NIDA

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Binafsi nimejaribu kukitafuta Kitambulisho changu cha NIDA, bila mafanikio yoyote, ofisi za Kata hakipo, ofisi za serekali za mitaa hakipo, japo nilihama eneo, nikaendelea labda nilijikomfuzi, wapi sikufanikiwa kukipata, Dar ni kubwa mihangaiko ni mingi, nawashauri nida pale ambapo mtu alipeleka maombi ya Kitambulisho na kupata namba yake, ndipo pawe mahala pa kuchukulia Kitambulisho chake! Kwa ni rahisi zaidi mtu kukumbuka pale alipopeleka maelezo yake kuliko huku mitaani ambako watu wanahama kila uchwao na kupoteza kumbukumbu,
N. B,
Vitambulisho vyote virudishwe nida ofisi za kanda watu wakavichukue huko.
 

Attachments

  • FB_IMG_17370838169329938.jpg
    455.3 KB · Views: 2
Usitegemee CCM waweze kufanya hayo.
 
Ndivo ilivo toka awali. Ulipojazia taarifa ndipo utakikuta hapo, sema kinachosumbua tu ni unakuta vimechanganywa kwenye kata ile ile.
Labda tu waweke chip kwenye vitambulisho ili kuwe na uwezo wa ku-trace kitambulisho kilipo, la sivyo hivi vichwa ni ngumu sana kukaa sawa. 😂
 
vitambulisho vimetolewa vingi saana vipo kwenye ofisi za serikali za mitaa lakini cha ajabu hamtaki kwenda kuvichukua mnakuja kulalamika huku, ulitaka wakuletee nyumbani kwako.....jifunzeni kuwa watu wakujitahimini na ww umefanya jitahada gani kuliko kuwa mlalamikaji tu hovyo nenda ukatafute kitambulisho chako au agiza ndugu aende na uthibtisho kwa mtendaji akijilisha atapewa
 
Ukizubaa watafuta namba yako, wajinga sana hawa jamaa
 
Nafikiri wewe ni mnufaika wa hapo NIDA au hayajawahi kukukuta ya ukiritimba uliokithiri wa NIDA yani imefikia hatua ukitaka kitambulisho au no ya Nida ni kama umeomba roho
 
Tatizo hilo ni kubwa sana kwa NIDA, rafiki yangu naye anakabiliwa na tatizo hili hili. Ameanduka barua-pepe kwa NIDA kuwajulisha kuhusu suala hili lakini hadi leo hajapata feedback kutoka NIDA.
Yeye kwa bahati mbaya Kitambulisho chake cha NIDA hakioni kabisa, ameenda kwenye Ofisi zote kabisa za Serikali za Mitaa/Ofisi za Afisa Mtendaji wa Mtaa zilizopo katika Kata hiyo lakini hajafanikiwa kupata Kitambulisho chake. Yaani amepata Usumbufu mkubwa sana, na bado anaendelea kupata Usumbufu na misukosuko ya kupata Kitambulisho chake.
 
Kuna wengine wana changamoto za kufuatilia vitambulisho vyao mbali mikoani na walikojiandikisha. Wakienda local office kuvipata wanaambiwa haiwezekani kuvifuatilia hapo, waende huko mbali mikoani walikojiandikisha
 
Kwa kuwa kuna waliojiandikisha mbali mikoani NIDA waweke angalau muda wa miezi mitatu mtu ajipange kufuatilia kitambulisho chake huko mbali mkoani. wasiweke muda mfupi kusitisha matumizi ya namba ya kitambulisho, hii ni kama wanashitukiza wananchi. waweke muda wa kutosha mwananchi aweze kufuatilia NIDA yake huko alikojiandikisha
 
Mimi kitambulisho changu bado kidogo tu ili kiishe mda wake, taratibu zipi za ku - renewal NIDA? 🤔 🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…