Haya ndiyo mambo ya ajabu ya taasisi zetu - NIDA

Haya ndiyo mambo ya ajabu ya taasisi zetu - NIDA

NIDA wasifanye haraka kusitisha matumizi ya namba ya kitambulisho hicho, watoe muda wa kutosha ili kila mtu asiye na hard copy afanye follow up alikojiandikisha. wengine walijiandikisha mikoani ni mbali, ni shughuli pevu kwenda huko inahitaji maandalizi ya kutosha pasipo kukurupushwa hivi. Uwekwe muda hata wa miezi mitatu ndio wasitishe matumizi kama wanakusudia kufanya hivyo
 
Binafsi nimejaribu kukitafuta Kitambulisho changu cha NIDA, bila mafanikio yoyote, ofisi za Kata hakipo, ofisi za serekali za mitaa hakipo, japo nilihama eneo, nikaendelea labda nilijikomfuzi, wapi sikufanikiwa kukipata, Dar ni kubwa mihangaiko ni mingi, nawashauri nida pale ambapo mtu alipeleka maombi ya Kitambulisho na kupata namba yake, ndipo pawe mahala pa kuchukulia Kitambulisho chake! Kwa ni rahisi zaidi mtu kukumbuka pale alipopeleka maelezo yake kuliko huku mitaani ambako watu wanahama kila uchwao na kupoteza kumbukumbu,
N. B,
Vitambulisho vyote virudishwe nida ofisi za kanda watu wakavichukue huko.
Wewe tu unaona sio sawa. Ila serikali inapeleka kitambulisho kwenye ofisi ya kata yako uliyojaza wakati unajaza taarifa za kuomba NIDA.
Binafsi Kitambulisho nilijisajili manyara miaka 4 iliyopita then nikarudi dar kilipotoka mwaka juzi kikapelekwa ofisi ya kata yangu niliyojaza na nikakipata juzi tu hapa.
Wakati ninachukua mtendaji alikuwa mkali Sana akasema kuna watu wanaiba vitambulisho vya watu wengine halaf wanavitupa mtaani vinaokotwa. Ndio maana alikuwa bampa to bampa na Mimi wakati ninatafuta kitambulisho changu
 
Aidha NIDA watayarishe apps ngamuzi ambayo utakuwa unaingiza nambari yako nayo iwe inakuelekeza uende wapi ukakichukue! (au kipo wapi) uende!
Tatizo kubwa taasisi zetu za serikali na teknolojia, bado wapo mbali sana,leo hii ingekuwa kitu kama NIDA hata siyo cha kuzungushana miaka,tena ingewezekana mtu apate ndani ya muda mfupi,au hata masaa sabini na mbili, sasa hivi unaweza pata namba,kitambulisho ukabaki kukisubiri zaidi ya mwaka mmoja
 
Nida wasumbufu sana
NIDA is a National disgrace!
 
Kwa kuwa kuna waliojiandikisha mbali mikoani NIDA waweke angalau muda wa miezi mitatu mtu ajipange kufuatilia kitambulisho chake huko mbali mkoani. wasiweke muda mfupi kusitisha matumizi ya namba ya kitambulisho, hii ni kama wanashitukiza wananchi. waweke muda wa kutosha mwananchi aweze kufuatilia NIDA yake huko alikojiandikisha
Me kitambulisho kilipelekwa December 2023 nikaja enda mkoa nilikojiandikisha October 2024 bado kilikuwepo
 
wasifute namba wataleta usumbufu mkubwa kwa wananchi, watoe muda angalau miezi mitatu watu waanze kuvitafuta na kuvifuata huko mbali walikojiandikisha
Acha wafute TU. Tanzania Tuna mambo ya ajabu sana. Unaeza ukakuta Kuna wapuuzi wamekaa wakaona wafute watu wajiandikishe upya ili wapige hela.
Kwa maendeleo ya sasa ivi ya teknolijia ya mawasiliano, unashindwaje kumfikia MTU kama hata alihama mkoa ili umpe kitambulisho chake.
Ukitaka kujua hao nida ni wale wale, hebu serikali itoe tenda Kwa private company ya kugawa hivyo vitambulisho uone kama miezi mitatu itafika.
 
Mama yangu alifuatilia nida yake serikali za mtaa, kata, hadi huko ukonga bila mafanikio. Mwisho alipotezea. Baada ya kitambo alifuatwa na mtendaji mmoja na kumwambia kaona nida yake kwenye mabox ofisini. Akampatia. Uzembe wa hali ya juu huu
 
Nida wangeingia kandarasi na benk NMB na CRDB kuwasaidia kugawa vitambulisho.

Hivi vitambulisho vyote vingewafikia walengwa kwa ufanisi mzuri tu tena ndani ya muda mfupi.
 
Acha wafute TU. Tanzania Tuna mambo ya ajabu sana. Unaeza ukakuta Kuna wapuuzi wamekaa wakaona wafute watu wajiandikishe upya ili wapige hela.
Kwa maendeleo ya sasa ivi ya teknolijia ya mawasiliano, unashindwaje kumfikia MTU kama hata alihama mkoa ili umpe kitambulisho chake.
Ukitaka kujua hao nida ni wale wale, hebu serikali itoe tenda Kwa private company ya kugawa hivyo vitambulisho uone kama miezi mitatu itafika.
UKIZINGATIA MWANANCHI ANAKUWA AMEWEKA NA MAWASILIANO YAKE
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Vile vya mwanzo vina mapungufu yafuatayo;

1. Havina signature.

2. Vina expire.

Hivi kweli kuna haja ya kurenew kitambulisho cha Taifa ?

Si ukipewa umepewa?
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Tumsifu Yesu Kristo mkatumeni !

Changu nilipata mapema sana 2017 kikapotea JKT huko sitaki hata kukumbuka
Milele Aminaaa.......

Leo tulikuwa na misa ya shukran na misa ya kuombea mavuno, kwa kweli tumebarikiwa sana.

Hapo andaa laki ya ku renew
 
Back
Top Bottom