Haya ndiyo maneno ya msanii Nick wa Pili juu ya Wasafi.com

Haya ndiyo maneno ya msanii Nick wa Pili juu ya Wasafi.com

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Nikki.jpg

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Weusi, Nikki Wa Pili amefunguka kuzungumzia changamoto zilizopo katika platform mbalimbli za kuuza muziki nchini.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Yakulevya’, amedai Watanzania hawapendi kununua muziki huku akidai bado mambo ni magumu licha ya kunzishwa kwa platform mbalimbali za kuuza nyimbo za wasanii.

“Watanzania hawapendi kununua muziki, platform kama Wasafi.Com haitaleta tija, kama bado unataka kupata wimbo bure kwenye ma groups ya whatsaap,” alitweet Nikki wa Pili.

Kabla ya Diamond kuanzisha kampuni ya Wasafi.Com, Mkito ndiyo kampuni pekee ya Tanzania ambayo ilikuwa ikiuza nyimbo za wasanii

SOURCE; MAHENGA BLOG
 
Better try than never boy..tech culture has a power..nowdays Tanzanians dont even think of cassets. changes are gradual..
 
Nafikiri hizi platform za kuuza nyimbo ziendelee tu kuja kwa wingi, itafika mahali tutauzoea tu mfumo huu. Tukiwa na mtazamo kama wa huyo jamaa tutaendelea na kausemi ka "wenzetu" mpaka mwisho wa dunia.
Mawazo kama ya Nick ndo yaliyofanya tuchelewe kuipeleka bongofleva kwenye ramani ya muziki wa Afrika kwa kufanya video za bei rahisi na kudharau ama kutoona umuhimu wa kuwekeza zaidi katika video.

Bwana Yule kuna wakati aliwaambia wanaDaslam anayeoona hiyo nauli ya kivuko ni kubwa basi apige mbizi. Japokuwa mimi sio muumini wa siasa zake ila kwa hapa nilimuelewa.
 
Better try than never boy..tech culture has a power..nowdays Tanzanians dont even think of cassets. changes are gradual..

Kwa ongezeko wa maharamia wa muziki,hits kabla ya kufika sokoni ishadukuliwa sana,..minadhan wangeanzisha haki miliki kusolve ii ishu,..LA sivo kutakua. Hakuna mapato,
 
Kwa ongezeko wa maharamia wa muziki,hits kabla ya kufika sokoni ishadukuliwa sana,..minadhan wangeanzisha haki miliki kusolve ii ishu,..LA sivo kutakua. Hakuna mapato,
Mbona hiyo hakimiliki ipo, tatizo ni njaa za wasanii wenyewe na umasikini unawafanya wanaziuza
 
Yaani ninunue nyimbo alafu bashite mmoja aniambie nifute yaani ntamla supu
 
Sasa kama juma akinunua via wasafi.com Si atanirushia via WhatsApp .....imekaaje hii ????.....
 
Tunawapenda wanamuziki wetu midomoni tu, na sio kununua kazi zao,na bongo wanamuziki wengi hutegemea zaidi show kuliko mauzo ya nyimbo, ndio maana kwa muda sijasikia msanii akitoa Album, maana wanajua tu watapata hasara..
 
Wapo mbona wenye albamu zao mfano Lady JD na Navy Kenzo
 
Wapo mbona wenye albamu zao mfano Lady JD na Navy Kenzo
Yeah wapo!,sokoni zinafanya vizuri?, hapo tatizo lilipo, utakuta nyimbo wanayo watu wengi sana, lakini siyo kwa kununua kazi halisi sokoni,mijini wamejaa wamachinga wakidulufu kazi za wasanii bila ya wasanii wenyewe kufaidika..
 
wenyewe wanasema zinalipa mkuu
 
Kwa ongezeko wa maharamia wa muziki,hits kabla ya kufika sokoni ishadukuliwa sana,..minadhan wangeanzisha haki miliki kusolve ii ishu,..LA sivo kutakua. Hakuna mapato,
Wamesha eka DCMA kwenye baadhi ya ngoma zao... Ukipakia kwenye blogu yako tuu inalambwa na unafutiliwa mbali kwa platform....
 
Back
Top Bottom