Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Weusi, Nikki Wa Pili amefunguka kuzungumzia changamoto zilizopo katika platform mbalimbli za kuuza muziki nchini.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Yakulevya’, amedai Watanzania hawapendi kununua muziki huku akidai bado mambo ni magumu licha ya kunzishwa kwa platform mbalimbali za kuuza nyimbo za wasanii.
“Watanzania hawapendi kununua muziki, platform kama Wasafi.Com haitaleta tija, kama bado unataka kupata wimbo bure kwenye ma groups ya whatsaap,” alitweet Nikki wa Pili.
Kabla ya Diamond kuanzisha kampuni ya Wasafi.Com, Mkito ndiyo kampuni pekee ya Tanzania ambayo ilikuwa ikiuza nyimbo za wasanii
SOURCE; MAHENGA BLOG