Haya ni baadhi ya maeneo yanayo weza leta maafa makubwa sana, kwenye Mvua za Elinino, unaweza ongezea

Haya ni baadhi ya maeneo yanayo weza leta maafa makubwa sana, kwenye Mvua za Elinino, unaweza ongezea

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
5,532
Reaction score
14,164
1. Mto wa Mbu, hili eneo ni hatari na nusu, na kama kwenye mvua hizi zitakuwa sawa au zaidi ya zile za 1997 basi tujiandae na maafa.

Ziwa Manyara limejaa tope na sehemu pekee ya kumwaga maji itakuwa ni mto wa Mbu pale mjini, ukiachana na hilo kitalamupale Mto wa Mbu hapafai kuishi make pia water table iko juu sana.

2. Ziwa Babati, pale Babati mjijni panaweza geuzwa ziwa na lile ziwa linaweza mwaga maji yake Babati mjini na kuleta maafa makubwa sana, tukumbuke isha wahi tokea mafuriko makubwa sana Babati na nahisi watu walisha sahau hilo.

3. Janga la Mlima Hanang bado halijawa solved linaweza rud tena na kuleta kiama kingine pale.

4.Maji huwa hayasahau asili yake hata ipite miaka 1000, maeneo ambayo yalikuwa ni mabwawa ya asili, mikondo ya maji, tegemea kwamba maji yanaweza kurudi kudai eneo lao.
 
downloadfile-158.jpg
 
Kwani si tumeambiwa Serikali imetenga Mabilioni kwa ajili ya EL Nino! Unatenga Budget Miezi michache kabla ya tukio, halafu unategemea uzuie maafa kwa kusafisha mitaro. Bladifakin.

Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu, kila mtu kwa sasa anajifunzia kunyoa.

Zimeshindwa kutufaa akili zetu, El Nino itakuja kutuonyesha madhara ya Ujinga wetu.

Tanzania bila rushwa, haiwezekani.
 
Moshi tambarare maeneo ya Khaye lazima mto Rau utangulize kadhaa kama kawaida yake. Morogoro wilaya ya kilosa wajiandae.
 
Moshi tambarare maeneo ya Khaye lazima mto Rau utangulize kadhaa kama kawaida yake. Morogoro wilaya ya kilosa wajiandae.
Morogoro mpaka bonde la mto Kilombero wajiandae kisaikolojia. Kilosa pia, bila kusahau bonde la mto Rufiji.
Bwawa la JNHPP lijiandae kufungua milango ya bwawa kwa ajili ya kupunguza maji
 
Morogoro mpaka bonde la mto Kilombero wajiandae kisaikolojia. Kilosa pia, bila kusahau bonde la mto Rufiji.
Bwawa la JNHPP lijiandae kufungua milango ya bwawa kwa ajili ya kupunguza maji
Nchi Kuna sehemu imejengwa kiholela sana. SGR imeziba mikondo asilia ya maji bila kutengeneza mikondo mingine.
 
Moshi tambarare maeneo ya Khaye lazima mto Rau utangulize kadhaa kama kawaida yake. Morogoro wilaya ya kilosa wajiandae.
moshi chini kata ya arusha chini/TPC vijiji vya chemchem, kirungu, mikocheni kule huwa kuna mto unaitwa ronga ni balaa. mto hufurika na kuzamisha vijiji. mafuriko yakitoka watu wanarudi tena kuishi huko. ni shida tupu wakati wa mvua nyingi huko
 
Kwani si tumeambiwa Serikali imetengea Mabilioni kwa ajili ya EL Nino! Unatenga Budget Miezi michache kabla ya tukio, halafu unategemea uzuie maafa kwa kusafisha mitaro. Bladifakin.

Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu, kila mtu kwa sasa anajifunzia kunyoa.

Zimeshindwa kutufaa akili zetu, El Nino itakuja kutuonyesha madhara ya Ujinga wetu.

Tanzania bila rushwa, haiwezekani.
pesa zitasaidia nini kama maafa yatatotokea na watu kupoteza maisha
 
Kimsingi dunia yote ni kama ilikuwa imefubikwa na maji. Siku yakiamua haitajalisha uko mlimani au bondeni
 
Nina wasiwasi sana na bwawa la mwalimu nyerere, kama litajaa kupita kiasi maji yakifunguliwa sujui ita kuwa aje.
 
Kimsingi dunia yote ni kama ilikuwa imefubikwa na maji. Siku yakiamua haitajalisha uko mlimani au bondeni
Bahari ndio ipo bondeni, ni ngumu ardhi ya dunia kufunikwa na maji total
 
Back
Top Bottom