Haya ni machache kati ya mengi niliyoyasikia au kuyaona kutoka kwa maustaz, wachungaji na waganga wa kienyeji. Je, na wewe ushashuhudia lipi?


Ukiona hospital inakwambia tumepima hatujaona ugonjwa tambua hiyo hospital haina vipimo vyote na haina wataalamu wa kusoma vipimo vyote.

Muhimbili yenyewe kuna vifaa vya baadhi vipimo haina. Ndio maana watu wanaenda nje ya nchi kutibiwa.


Wabongo wakiambiwa tumepima ugonjwa hauonekani wanakimbilia kwa waganga ama manabii huku wanasahau wameambiwa ugonjwa hauonekani sababu vipimo vya kupima huo ugonjwa hakuna kwenye hiyo hospital
 
Yah ni kweli, wakati fulani na hospital nazo huchangia watu kuchukua maamuzi ya kwenda kwa mganga.

Na hii nafikiri inatokana na ubovu au uduni wa vifaa vya upimaji wa magonjwa kwa baadhi ya hospital zetu.
 
Kweli kbs mkuu, bila vipimo vya ugonjwa husika, basi madaktari hawawezi kuuona au kuujua ugonjwa wa mtu.
 
Kubadili hospitali ni vizuri zaidi.

Kuna mjomba wangu nae hospital ya kwanza akaambiwa ugonjwa unaomsumbua akaanza kuutibu, lakini hali ikazido kua mbaya. Kwenda hospitali nyingine nayo wakamwbia ile ya kwanza alikosea ila ugonjwa sahihi ni huu.
Lakini badp hali haikua nzuri, mpaka alipoenda muhimbuli ndo akaambiwa ugonjwa sahihi na kuanza kupata nafuu.
 
Kweli kbs mkuu, ndo kama nilivyosema hapo juu kwamba muda mungine huwa ni ubovu wa vifaa au pengine hospital inakuwa haina vifaa vya kupima ugonjwa husika.

Sasa watu wengine wakiona hivyo fasta wanawahi kwa sangoma kupiga ramli chonganishi, na matokeo yake wanatapeliwa na mganga.
 
Hivi Dr tamba wa pale magomeni mikumi bado yupo?. Naomba mnijibu kwanza nijue kabla sijaleta kisa hapa kilichonitokea 2010
Alishaniibia na kunipiga majini ya kutosha iinibidi nikaokoke ndio ilikuwa pona yangu alikuwa anapenda kunyoa panki na kukata way vaa yake tu alikuwa anaonekana taperi afu alikuwa mzee wa PC ila kwa sasa ni marehemu nafikiri mwaka wa tatu sasa
 
Alishaniibia na kunipiga majini ya kutosha iinibidi nikaokoke ndio ilikuwa pona yangu alikuwa anapenda kunyoa panki na kukata way vaa yake tu alikuwa anaonekana taperi afu alikuwa mzee wa PC ila kwa sasa ni marehemu nafikiri mwaka wa tatu sasa
Jini kweli haogopi kelele za 'kwa jina la yesu'..usiwachukulie poa majini
 
Alishaniibia na kunipiga majini ya kutosha iinibidi nikaokoke ndio ilikuwa pona yangu alikuwa anapenda kunyoa panki na kukata way vaa yake tu alikuwa anaonekana taperi afu alikuwa mzee wa PC ila kwa sasa ni marehemu nafikiri mwaka wa tatu sasa
Hapo kwenye majini unanikumbusha yule mama alivyoenda kwa mchungaji akaambiwa hivyo hivyo kuwa alitupiwa kijini na mwl mwenzake ili akifukuzwa kazi au kufa huyo mwl aweze kukaimu na kuchukua nafasi ya mgonjwa (mwl mkuu). Familia kusikia hivyo wakamwaga mahela hadi kupelekea kuuza nyumba zao mbili ili kupata tiba za kiroho mwisho wa siku wakaja kugundua kuwa ule ulikuwa utapeli mtupu.

Hivyo hivyo kwa yule binti mganga alimwambia katupiwa jini na mke wa mchepuko wake, ustaz nae akamwambia huenda kakutana na jini njiani ndomaana linamsumbua. Mwisho wa siku binti akatapeliwa huku ukweli ukaja kujulikana kuwa binti ana ukimwi.

So hayo mambo ya kutupiwa majini na uchawi ndio yanayotumika kuwalaghai watu ili wapige hela na ukizingatia ni vitu tu vya kufikirika, havionekani kwa macho. Pengine ukifuatilia kiundani utakuta hivyo vitu havipo kbs duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…