Haya ni mafanikio yenye kuhitaji shamrashamra?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Huwa naona watu wanapongezwa, wanapongezana au hata kumshukuru Mungu kwa shukrani zote kwa:

1. Kupanda ndege

2. Kuonekana kwenye TV

3. Kufika nchi ya nje na Tanzania

4. Kupata likes au re-tweet ya mtu maarufu

5. Kupiga picha au kukutana na mtu mkubwa au maarufu.

Je, haya ni mafanikio yanayohitaji shamrashamra au shukrani kwa Mungu?
 
Huwa naona watu wanapongezwa, wanapongezana au hata kumshukuru Mungu kwa shukrani aww?
Suala la mafanikio liko subjective sana ni kama pesa na matumizi yake baina ya mtu na mtu.

Na nitatumia mfano wa pesa ili nijenge hoja yangu kwenye kujibu hilo swali, ni kwamba...

The way wewe unavyoitreat pesa ni tofauti na mtu mwingine anavyoitreat, ndio maana huwa ni rahisi sana kumuona mtu mwenye kuitumia pesa yake kinamna tofauti na wewe unavyoitumia mfujaji ila kiuhalisia yeye anajiona kawaida tu na pengine na yeye anakuona wewe haujui namna nzuri ya kutumia pesa.

Sasa rudisha huo mfano wa pesa kwenye swali lako na utagundua kwamba kitu ambacho wewe kwa tafsiri yake unakiona cha kawaida sana mwenzio akikutana nacho hakioni kawaida kama wewe bali anakiona ni kikubwa na yeye kukutana nacho au kukipata nikama miujiza kwake.

Na ujumla wa mambo yote haya yanatokana na background zetu, malezi na maeneo ambayo tumekulia, exposure za familia na neighborhood.
 
Huwa naona watu wanapongezwa, wanapongezana au hata kumshukuru Mungu kwa shukrani zote kwa:

1. Kupanda ndege

2. Kuonekana kwenye TV

3. Kufika nchi ya nje na Tanzania

4. Kupata likes au re-tweet ya mtu maarufu

5. Kupiga picha au kukutana na mtu mkubwa au maarufu.

Je, haya ni mafanikio yanayohitaji shamrashamra au shukrani kwa Mungu?
Kupiga hatua ya kimaendeleo
Kumbe jibu unalo. Hayo uliorodhesha hapo juu hao unaowazungumzia kwao ni kupiga hatua.
 
Suala la mafanikio liko subjective sana ni kama pesa na matumizi yake baina ya mtu na mtu.

Na nitatumia mfano wa pesa ili nijenge hoja yangu kwenye kujibu hilo swali, ni kwamba...

The way wewe unavyoitreat pesa ni tofauti na mtu mwingine anavyoitreat, ndio maana huwa ni rahisi sana kumuona mtu mwenye kuitumia pesa yake kinamna tofauti na wewe unavyoitumia mfujaji ila kiuhalisia yeye anajiona kawaida tu na pengine na yeye anakuona wewe haujui namna nzuri ya kutumia pesa.

Sasa rudisha huo mfano wa pesa kwenye swali lako na utagundua kwamba kitu ambacho wewe kwa tafsiri yake unakiona cha kawaida sana mwenzio akikutana nacho hakioni kawaida kama wewe bali anakiona ni kikubwa na yeye kukutana nacho au kukipata nikama miujiza kwake.

Na ujumla wa mambo yote haya yanatokana na background zetu, malezi na maeneo ambayo tumekulia, exposure za familia na neighborhood.
Uko sahihi.
Kwa mfano kuna watu walio wengi wanakuja kupanda ndege ukubwani baada ya kuchapa kazi kwa miaka mingi kisha anatokea sponsor wa kumlipia tiketi lazima afurahie ila kuna wengine walianza kupanda ndege tangu wakiwa wadogo bado wanasoma familia zao zinawagharamikia tiketi so hatuwezi kufanana
 
Kabisa mkuu...
 
Suala la mafanikio liko subjective sana ni kama pesa na matumizi yake baina ya mtu na mtu.

Na nitatumia mfano wa pesa ili nijenge hoja yangu kwenye kujibu hilo swali, ni kwamba...

The way wewe unavyoitreat pesa ni tofauti na mtu mwingine anavyoitreat, ndio maana huwa ni rahisi sana kumuona mtu mwenye kuitumia pesa yake kinamna tofauti na wewe unavyoitumia mfujaji ila kiuhalisia yeye anajiona kawaida tu na pengine na yeye anakuona wewe haujui namna nzuri ya kutumia pesa.

Sasa rudisha huo mfano wa pesa kwenye swali lako na utagundua kwamba kitu ambacho wewe kwa tafsiri yake unakiona cha kawaida sana mwenzio akikutana nacho hakioni kawaida kama wewe bali anakiona ni kikubwa na yeye kukutana nacho au kukipata nikama miujiza kwake.

Na ujumla wa mambo yote haya yanatokana na background zetu, malezi na maeneo ambayo tumekulia, exposure za familia na neighborhood.
Kupiga picha tu na Rais au waziri inaweza kuwa mafanikio pia?
 
Yeah inaweza kuwa mafanikio kwa mtu... kuna watu wametokea familia za kawaida familia ambazo hazina connection za watu wa namna hiyo kwahiyo unakuta ukoo mzima hakuna mtu ambae aliwahi kujitengenezea connection ya kukutana na wakuu kwahiyo mtu wa namna hiyo unahisi akifanikisha jambo la hivyo atajionaje?

Na hiyo haitaishia kwake tu bali katika ukoo mzima na kuna kaheshima fulani hivi atakapata kwa wana familia kwamba nae amepata neema ya kuketishwa na wakuu hadi kupiga nao picha 😆😆
 
Vipi kama nikikupa hongera kwa kuanzisha huu Uzi,utajisikiaje?

Ukianza kuhoji vitu ambavyo vinapaswa mtu kupewa hongera,mwisho utakuja kuhoji pia vitu ambavyo havipaswi mtu kupewa Pole.
 
Back
Top Bottom