Haya ni makosa watu huyafanya na kuwagharimu kwenye ngumi za Mtaani (Street Fights)

Haya ni makosa watu huyafanya na kuwagharimu kwenye ngumi za Mtaani (Street Fights)

Watu ni wagonjwa sana siku hizi, ni vyema zaidi kuzuia pambano,... pigana ikiwa ndo last option tu,......kuna mtu alilazwa mwezi mzima kwa kupigwa ngumi moja tu,.....

Kumbuka ukiwa mwanaume Dunia haina huruma na wewe, ni vyema ukajiweka fit,....👊💪👊👊🥷🥷
 
Pengine unaweza kujiona upo salama kwa kudhani ngumi za mtaani ni kwa wapiga debe, bodaboda, n.k. ACHA KUJIDANGANYA !! Unaweza ukawa unajenga nyumba yako mmepishana kauli na fundi kiasi cha kutwangana, Makazini huko mnaweza kupishana kauli mkatwangana, Jela ni kawaida sana kupigana lasivyo unakuwa target, Hata watu wazima huwa kuna kuoneana kuna muda itabidi ujitetee, n.k.

Kufikiri Kuna Sheria​

Ni kosa kuingia kwenye mapambano ya mtaani ukidhani kuna sheria za kufuatwa. Hii sio boxing, hakuna mwamuzi, hakuna muda wa kupumzika, na mara nyingi, hakuna huruma. Kufikiri kwamba mpinzani wako atafuata kanuni ni kosa kubwa. Mapambano ya mtaani mara nyingi hayana heshima, na ni muhimu kuelewa kuwa usalama wako unapaswa kuwa kipaumbele.


Kutokukimbia Kisu au Silaha inapotolewa​

Kuna mikoa kama Arusha ugomvi huambatana na visu hawawezi kuzichapa kavu, Unapoona kisu kwenye pambano, jambo bora zaidi unaloweza kufanya ni kukimbia, Kiburi cha kuendelea kupigana kwa hofu ya kuonekana muoga waweza poteza uhai wako. Mapambano dhidi ya mtu mwenye silaha ni hatari sana na mara nyingi huishia kwa madhara makubwa. Kisu hakihitaji nguvu nyingi ili kusababisha majeraha mabaya, na kukabiliana nacho kunaweza kuwa kosa la maisha.


Kutohifadhi Nguvu​

Watu wengi hutumia nguvu zote kwa mpigo ndani ya zile sekunde 30 za mwanzo, matokeo yake huchoka haraka kwa kutumia nguvu nyingi mwanzoni mwa pambano, Hii ni advantage kubwa kwa mtu unaepigana nae alietunza nguvu atakudonoa sana ukiwa huna nguvu, Ni vema kutumia nguvu kwa sekunde 10 za mwanzo ukiona adui bado anastahimili ni muda wa kujitafakari kutunza nguvu zako.. Ni muhimu kugawa nguvu zako ili usiwe rahisi kushindwa.


Kujitamba na Kuongea Maneno mengi (Kupiga Bla Bla)​

Ni pambano la kimwili sio kuchambana kwa mdomo, Usiongee sana kabla ya pambano, Anza kuongea ukiingia kwenye pambano na dalili zinaonesha unammudu, Kuchimba mkwara au kujigamba kuhusu kile utakachofanya huchochea hasira za mpinzani na kumpa nafasi ya kujipanga jinsi ya kukushushia kipigo. Kimya na umakini ni silaha bora za akili wakati wa mapambano ya mtaani.


Kujaribu Kuiga Mapigo ya Kwenye Filamu​

Mapambano ya kwenye filamu ni ya kubuni na mara nyingi hayahusiani na hali halisi. Kujaribu kuruka au kufanya miondoko ya kushangaza kama unavyoona kwenye filamu kunaweza kukuweka kwenye hatari zaidi. Badala yake, elewa hali halisi na tumia mbinu za msingi.


Kufikiri Kuzuia / Kublock ngumi ni Rahisi Kama Kwenye Game​

Katika hali halisi, kuzuia ngumi sio rahisi. Badala ya kujaribu kuzuia ngumi zote, ni bora zaidi kurudi nyuma au kuendelea kumshambulia mpinzani. Kuwaza kuwa unaweza kuzuia kila ngumi kama kwenye game ni kosa litakalo kugharimu.


Kutoshusha Kidevu Chini​

Kidevu kilichoinuliwa huacha uso wazi na rahisi kushambuliwa kwa uppercuts na vifuti. Kuweka kidevu chini ni mbinu ya msingi ambayo inapunguza hatari ya kupata pigo kubwa kwenye uso. Hakikisha unalinda kichwa chako vizuri.


Kuacha baada ya Kumwangusha Mpinzani​

Baada ya kumwangusha mpinzani, usidhani pambano limeisha na kugeuza mgongo kuondoka. Wengi wao huweza kusimama tena na kuendeleza shambulizi. Hakikisha unadhibiti hali na kuwa tayari iwapo atajaribu kushambulia tena. Usimpe nafasi ya kukushambulia unapogeuka.

Kumsukuma Mtu Baada ya Kusukumwa​

Kusukuma hakutatatua chochote. Ikiwa umesukumwa, jibu kwa ngumi badala ya kurudisha msukumo. Hii inakupa nafasi ya kujilinda na kushinda pambano kabla mpinzani hajapata nguvu ya kushambulia tena.

Kupigana na Mtu Mwenye Mwili Mkubwa au Mrefu​

Kupigana na mtu mwenye nguvu nyingi, mwili mkubwa, au mrefu ni hatari zaidi. Watu hawa mara nyingi wana faida ya kimwili inayoweza kukuangamiza kwa urahisi. Badala ya kupigana, tafuta njia ya kuzuia au kujiepusha kabisa.


Kutaka kuendelea Kulinda Heshima baada ya kushushiwa kipigo​

Kutaka kuendelea kupigana kwa sababu ya kiburi au kujaribu kuokoa heshima mara nyingi hupelekea madhara makubwa. Ikiwa umeona hali ni mbaya umeshushiwa kipigo hevi ni bora zaidi kukubali kushindwa au kutoroka. Hakuna aibu katika kuokoa maisha yako.

Kurudia Mbinu Zisizozaa Matunda​

Ikiwa mbinu fulani haifanyi kazi kwa mpinzani, kuendelea kujaribu hakuwezi kubadilisha matokeo. Badala yake, kuwa mbunifu na badilisha mkakati wako. Kurudia makosa yale yale kunaongeza tu nafasi ya kushindwa.

Una umri gani bro, ambaye mpaka wa leo unawaza kupogana ngumi.
Siku hizi kuna usemi, kabla ya kupigana na mimi, utapigana na hela yangu. No physical fights, kama kipindi cha ujima
 
Kutokutumia lugha ya staha mwenzako anapokuja kwa jazba.
Ulimi ni moja ya kiungo makini sana katika kuepusha ugomvi, neno dogo kama samahani mkuu linaweza epusha mengi, ukiona haliepushi hakikisha unakuwa wa kwanza kushusha konde zito kwenye utosi maana hakuna namna ingine.
 
" Kumsumkuma mtu baada ya kusukumwa"
..................
" Ikiwa umesukumwa jibu kwa ngumi, usijibu kwa msukumo".😁😁😁 SIO RAHISI KIHIVYO MKUU.


Mkuu kusema ni rahisi kuliko kutenda. Ngumi sio sawa na mpira wa miguu kwamba useme ukizidiwa utampasia mwenzako.


Uzi wako ni sahihi kabisa kama unaongea na watu wangumi na sio wenzangu na Mimi ambae anaingia kwenye pambano la ngumi huku kimoyomoyo akiomba Mungu afanye muujiza atokee mtu wa kuamua.

Kikubwa kuliko vyote ambacho umekisahau ni kuhusu saikolojia ya watu kwenye ngumi.

Unajua kwanini mtu huwa anasukuma baada ya kusukumwa? Do u know the psychology behind?


Ni kwamba wote wana ogopana? Anaeanza kusukuma anaogopa na anae rudisha msukumo anaogopa pia.

Wanasukumana kwa ajili ya kubuy time waje watu wagombelezee au kujaribu kugather courage ya kurusha ngumi kwa mara ya kwanza.

Kupigana sio jambo rahisi kama ambavyo mtoa mada unajaribu kuiweka
Umeongea uhalisia zaidi, sio nadharia
 
kwenye Kunfu kukimbia ni silaha pia.Lingine Nawapa hii akiba siku inakulazimu no way zaidi ya kupigana hakikisha una sindano ya kushonea Viatu kiunoni hii inatumika kwa watu warefu na mbavu hawa hakikisha usimweke mbali na mpinzani akikuweka maungoni fasta unamaliza pambano.
 
Kama hujawahi kupigana tangu utotoni hasa shule ya msingi basi usithubutu, ukimya ni silaha tosha.

Nawashauri vijana wangu siku zote wasipigane. Siku hizi watu wengi wabovu. Unaweza ukamkusa kidogo tu, tayari mtu chali. Unaanza kuozea Segerea. Usimpige mtu. Hiyo ni mbaya. Nakumbuka miaka zaidi ya 30 iliyopita, jamaa mmoja alimpiga jamaa mwingine ngumi mpaka akazimia. Watu wakaanza kupiga kelele, ameua ameua. Jamaa akaanza kulia nisamehe. Anataka kukimbia. Watu wakamshika, wanamuambia hapa ni polisi tu. Du jamaa ndiyo akazidi kulia. Uzuri yule jamaa akazinduka kabla ya kwenda polisi. Alivyoona hivyo yule jamaa akanyamaza, na kwenda mbele ya yule jamaa aliyezinduka akapiga magoti akisema nisamehe. Lakini naomba usife tena. 😛 😀
Kweli hasira hasara
 
Uzi mzuri huu. Binafsi mimi yalinikuta. Jamaa walinipora simu yangu smart mpaka leo hii naingia jf na kiswaswadu. Walikuwa wamebebana wawili kwenye bike nite ngoma tatu hivi.. Mmoja wao akashuka na panga na kisu . Nikataka ku fight back. Wee kidogo nishushiwe la utosini. Ikabd niwe kama nalizuia lile panga kwa mkono . Kilichotokea vidole vyote vinne vya mkono wa kushoto vilikwatwa na sikutegemea kama vingepona . Nilijua vimekatiwa chini. Dah. Ilichukua almost a year ku recover japo nimebaki na kovu la kudumu kwenye vidole vya mkono wangu wa kushoto. Ningekuwa na smart ningepg picha mjionee jinsi vilivyo. Polisi nilienda na hakuna msaada wowote hadi leo hii. Nikasema anyway life goes on. Nilimshukuru mungu sikujeruhiwa kichwani maana ingekuwa ni RIP.
 
Kutokutumia lugha ya staha mwenzako anapokuja kwa jazba.
Ulimi ni moja ya kiungo makini sana katika kuepusha ugomvi, neno dogo kama samahani mkuu linaweza epusha mengi, ukiona haliepushi hakikisha unakuwa wa kwanza kushusha konde zito kwenye utosi maana hakuna namna ingine.

Akizima hapo hapo, itakuwaje?
 
Watu hawalijui hili! Yaani unafungwa maisha huku unajiona! Jamaa alikuwa na pumu kugusa kidogo pumu hiyo na kuzima juu!

Watu wanakimbia wanakuacha wewe mwenyewe! Nilijifunza sana kitu kwenye ule ugomvi! Polisi plus jamhuri hawana dogo! Epuka ugomvi kwa gharama zozote!
Nakuelewa sana kwenye hili.
 
Kuna muda ukimwa wako watu wanaweza kukuchukulia advantage kama weak point. Hili unalizungumziaje?
 
Last time kupigana sikumbuk ni lini... mara nyingi Wauni, walevi, vibaka wa mitaani huwa nachapa makofi mawili matatu.. Ngumi situmii kbs ntaua.

Nakumbuka nilirusha ngumi jamaa akaikwepa kwa kubahatisha ikaenda ktk mpapai, ule mpapai uligawanyika katikati jamaa alikimbia mbio ambazo Usain bolt asingefata..
 
Back
Top Bottom