Uchaguzi 2020 Haya ni mambo 10 niliyoona kwa CCM Vs CHADEMA mpaka sasa kuelekea kipute cha kampeni rasmi

Uchaguzi 2020 Haya ni mambo 10 niliyoona kwa CCM Vs CHADEMA mpaka sasa kuelekea kipute cha kampeni rasmi

Wanadanganywa na JF FB
Kama 2015
Hahaha mambo Ni Rahisi sana Ka Jpm
Tena hao hata wakiungana wakipata 20% Washerehekee
 
Hivi huyo magufuli takwimu gani zinambeba?

Hali ya kiuchumi Kwa wananchi ikoje? Kwa wakulima wa mbaaazi, korosho, tumbaku takwimu zikoje?

Suala la ajira kwa vijana kafanya nini? Ameua uwekezaji na sekta binafsi kaishia kufanya maelfu ya vijana kuwa jobless na watu kupoteza ajira

Ameua watu, kubambikia watu makesi, kuonea watu mpaka hata watoto wadigo wanajua

Ameharibu biashara kupelekea watu kufunga biashara zao na wengine kufirisiwa na mabenki?

Huyo magufuli kafanya ya nini zaidi ya haya? Njia ni nyeupe sana kwa Tundu Lissu mwaka huu.
Asante sana Mkuu
 
Records,records
Records nzuri au mbaya,kitu gani kipya ambacho kabisa maraisi waliotangulia hawakukifanya yeye kafanya Tena chenye manufaa?
Mtu anatukana watu hovyo,Hakuna utawala wa sheria ,hafuati sheria Wala katiba Unawezaje kumsifu Kama wewe sio mhalifu?

Dk Slaa alijinasibu kuwa Ni mpenda utawala wa sheria,je huyu anaongoza kwa kufuata sheria?
Jipange ndugu acha kuleta mada za chuki.
Unaukumbuka uchaguzi wa serikali za mitaa? Wewe ndio unaona sawa hivyo?
 
Wakuu,

Haya ni mambo 10 niliyoona mpaka sasa kuelekea kipute cha kampeni rasmi.

1) What a match!, Mpaka sasa CCM inabebwa na watu wenye experience ambao kipindi kama hiki ndio unajua uwezo wao. Wao kelele nyingi ziko kwenye mipango (strategies) kuliko kelele na matamko ya majukwaani.

2) Tundu Lissu is impressive as usual lakini seems Chadema hawakumuandaa, experience yake ya uanaharakati ndio unaofanya aonekane active uwanjani lakini bado hajawa na madhara kihoja ingawa bado mapema. Mambo ya kusema atamshtaki JPM kwa rushwa ya kununua jogoo laki moja ni uanaharakati si level zake tena kama mgombea Urais.

3) John Pombe Magufuli yuko composed sababu ya records zake awamu hii ya kwanza. Lakini pia kwasasa nguvu kubwa ipo kwenye kupanga vyema mabeki majimboni na udiwani.Hapo ndio unapoona timu kubwa na yenye watu wazoefu inavyohandle mchezo. Ni kama wameamua kuacha wapinzani wacheze huku wao wakikamilisha ramani ya ushindi.

4) Kimbinu Chadema wanahitaji timu bora kumzunguka Lissu wakiwemo waandamizi wa serikali zilizopita akiwemo Nyarandu ili kumshape Lissu kama mgombea Urais lakini pia mipango ya kusaidia kampeni majimboni ambako hali si nzuri

5) Kimbinu CCM wana kazi kubwa ya kumaliza mchakato wa wagombea ubunge na udiwani bila mpasuko lakini maeneo mengi kimbinu wamejipanga kushinda.

6) JPM takwimu zinambeba na wananchi wanajua matokeo yake wakimchagua tofauti na Lissu ambaye anapaswa kujikita kwenye hoja zenye matarajio ya wananchi hasa wanyonge walio wengi. Je ataweza kuaminisha wananchi ili wamchague?

7) Financially CCM wako stable kuhandle kampeni kuliko Chadema ambayo imepanga pia kusimamisha wagombea majimbo yote.

8) JPM amefanikiwa kuhakikisha watendaji wake wote wanajua takwimu za mambo yaliyofanyika awamu hii hivyo itabidi kila hoja za Lissu zinazogusa takwimu ajipange otherwise akikosea atapingwa hata na makatibu tarafa. Hizo takwimu zimeimbwa muda mrefu na hata wananchi wengi wamezikariri.

9) Angalizo, Lissu usihangaike na wimbo wa katiba mpya hauna mashiko kwa wananchi wanyonge na hautampa kura. JPM pia awekeze hoja kwenye mipango mipya hasa mapinduzi kwenye kilimo na uwekezaji.

10) Wapinzani bila kusimamisha mgombea mmoja huu utakuwa uchaguzi mgumu hadi majimboni kuliko wakati wowote.

Mizania pima mwenyewe, hayo ni maoni yangu binafsi [emoji41]
MTAZAMO Kwanza ongera kwa kupost Uzi Mara nyingi wewe sio mtu wa kupost.Ningependa jamiiforum iwe na watu kama wewe wanaoleta facts na unadeserve kuitwa great thinker umeleta hoja nzuri Cha ajabu mashabiki uchwara a.k.a small mind badala la kujibu hoja yako kwa hoja wao watajikita kukutukana zaidi
 
MTAZAMO Kwanza ongera kwa kupost Uzi Mara nyingi wewe sio mtu wa kupost.Ningependa jamiiforum iwe na watu kama wewe wanaoleta facts na unadeserve kuitwa great thinker umeleta hoja nzuri Cha ajabu mashabiki uchwara a.k.a small mind badala la kujibu hoja yako kwa hoja wao watajikita kukutukana zaidi
Great thinker kwa uzi huu?????😀😀😀😀😀

Kweli Lumumba mnatia huruma aisee
 
Ndiyo umefikia hapa! Unajitoa ufahamu na kujidhalilisha namna hii? CCM wana mbinu gani zaidi ya mbinu ya ''dola''? Hebu tuwe fair: CCM bila nguvu ya dola itapata shida kubwa sana kushinda uchaguzi.
 
Nikafikiri ni Lowassa tu aliwakera kumbe hata Lissu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ndo mngeaminiwa nyie kweli? Papuchi isingeleta rabsha katikati ya mapambano?
Mkuu kumbe huyu jamaa ''unamnyaka'' vizuri kama mimi! Huyu ni Chadema wa zamani aliyejeruhiwa na maamuzi ya Lowassa kujiunga mwaka 2015. Alisubiri wee Chadema ife lakini ameona baada ya Lissu kurudi na kila mtu amekuwa kama amepewa uhai mpya hivyo roho inamuuma.
 
Hiyo issue ya jogoo nimeona jamaa yenu anaropoka pasi kujua hata anachoongea na sidhani kama huo ndo uanaharakati bali uzwazwa tu.

Hata uki-search "kuchi" humu jamvini utakutana na bei za hadi 500,000 kwa jogoo mmoja.

Hizo siasa za ulaghai wa kitoto hivyo zimepitwa wakati.
 
Back
Top Bottom