Haya ni maringo ya Wakenya au ni kujiwekea standard juu dhidi ya majirani?

Itakuwa kila nchi ina vigezo vyake, ndio maana Dodoma au Mbeya hayawezi kuwa majiji Kenya.
Kweli kabisa kwa mfano UK wao kuwa jiji zamani ni lazima iwe na Cathedral
Ingawa sasa sio lazima
Ila nafikiri kuwa na watu wengi ni kigezo kimoja na hata vyuo vikuu ila sio magorofa
 
Eldoret ni mji umepangiliwa vizuri sana na kati ya miji misafi sana ya Kenya. Mji uko vizuri kuliko Chuga, Mbeya na Hata Tanga.

Phyllis wangu, mtoto wa kikalei, kama bado upo Eldoret, nistue nije tupashe viporo!
 
Tanzania Jiji ni Dar na Mwanza tu kwa vigezo vyote
Kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa vya Uanishaji wa Miji kuwa Jiji, Dsm na Mwanza vimekosa kabisa sifa za kuweza kuwa Jiji, hata kwa kuzingatia kigezo kimoja tu Kupangilika kwa Mji na Miundombinu yake (Town Planning and Infrastructures Planing and its Quality).
Mathalani, takribani asilimia 80 Ardhi yote kabisa ya Mji wa Dsm haijapimwa (usurveyed) na wala haiko katika Mpangilio mzuri, hata miundombinu yote kabisa ya ujenzi na majenzi pia haipo kwenye mpangilio licha ya kwamba Ina ubora ulio duni kabisa. Mji wote upo shagala-bagala, hovyo hovyo, mchafu na karibia takribani asilimia 70 ya Nyumba na majengo yote kabisa yaliyopo kwenye mji huo hayafikiki kabisa kwa barabara.
 
Ipo mbali kushinda majiji mengi uchwara ya TZ.
Tanzania haina jiji uchwara hata moja shida ni miundombinu, siku ukienda huko eldoret, kisumu au Nakuru ndio utajua kuwa Tanzania ina majiji mazuri sana na yenye vibrant na chaotic feelings.
 
Hii na Iringa bora Iringa. Haistahili kuwa jiji labda kama wana vigezo vyao vingine ila muonekano wa mji ni chini ya kiwango.
Wanababaishwa na tughorofa tuwili vya hapo, kisumu inazidiwa na eldoret kwa maghorofa lakini kisumu ni jiji la tatu.
 
Tazama vibrant, chaotic feeling, mandhari na pia uchumi wa sehemu hiyo hizo ni sifa tukukq nje ya population.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…