Haya ni mazao matano ambayo hayana mkono wa Serikali, ukikaza huko unachomoka na pesa

Mpunga hata serikali waje na sera gani ukilima mpunga na ukafanikiwa kuwa na mavuno ya kutosha wewe tunza store tu, ukianza kuuza mwezi December faida ipo
Hapa safi πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Umeandika kikulima sana
Kilimo labda ununue mazao lakini siyo kulima utakufa kwa kihoro- utakosa bei na utavuna mavuno usiyoyategemea.
Umeandika kibiashara zaidi.
Haiwezekani tuache kulima tugeukie ulanguzi wa mazao!
Nani atalima?
Kila kazi ina changamoto zake, kikubwa kuzijua na hivyo kujiandaa kukabiliana nazo.
Lakini lazima tulime.
 
Hahahaha,🀣🀣 safi sana.
Ila uwe una edit.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ waambie ndio maana hata jina lako ni Tangatika na sio Tanganyika.
 
Umeandika kibiashara zaidi.
Haiwezekani tuache kulima tugeukie ulanguzi wa mazao!
Nani atalima?
Kila kazi ina changamoto zake, kikubwa kuzijua na hivyo kujiandaa kukabiliana nazo.
Lakini lazima tulime.
mi binafsi ni muumini wa yale mazao yasiyo ya msimu,kama ndizi
ila hAYA ya msimu, mimi ni big no
 
mi binafsi ni muumini wa yale mazao yasiyo ya msimu,kama ndizi
ila hAYA ya msimu, mimi ni big no
Kilimo cha mboga, matunda na viungo ndiyo kinachoweza kubadilisha maisha ya mkulima, lakini pamoja na changamoto lazima tulime chakula kwa wingi maana tunakihitaji.
 
Alizeti??, mbaazi? Miogo?
 
Mazao yote ambayo Serikali imeyaundia bodi ukilima hauwezi toboa.

Bodi ya Korosho
Bodi ya Tumbaku
Bodi ya Pamba
Bodi ya Kahawa
Bodi ya Pareto
Bodi ya Mazao mchanganyiko (humo kuna ufuta, mbaazi, n.k)

Hizi bodi ni wakala wa Serikali kumfilisi mkulima
 
Nmesoma mpaka ukurasa wa mwisho nikitafuta kujua maharagwe yame-elezewaje katika muktadha wa mada hii
 
Watu wanavyo lalamika hapa sijui kilimo kigumu, sijui mazao yanaharibika.
Mimi naona mleta mada yupo sahihi, sijawahi kusikia wauza chips wanalalamika viazi hakuna sokoni sasa wanaolima ni kinanani na kwanini hawaachi kama hawapati faida, the same kwenye ngano, mpunga, viungo vinapatika na watu wanalima sasa kama vinahasara kwanini hawaachi kulima.
Mleta mada anacho zungumzia nikwamba ikitokea vimekubali shambani utauza bila buguza ya serikali kwa asilimia kubwa kuliko mazoa mengine ambayo serikali imetolea macho.
 
Gunia la debe sita la viazi eti 30,000 we jamaa ni mwehu. Viazi huuzwa kwenye kiroba cha debe tatu ambacho bei hupanda hadi 60,000.
Kiazi kikiuzwa debe 5000 faida ipo , Kuna msimu vinatembea hadi 12,000 kwa bei ya shambani hapo lazima uokote pesa
 
Acha uongo wewe mimi nalima korosho,ufuta na mbaazi na napiga hela vizuri tu...humu ndani wengi wenu hamjawahi hata kulima zaidi ya kujifanya wajuaji tu wa kila jambo
 
Sawa
 
Katika yote NGANO......NGANO DILI SANA....serikali iliyaua mashamba ya NAFCO Basotu.....wanatoa vibali watu wana Import ngano kimya kimya....lakini hata hivyo...bado ukilima itakulipa tu πŸ‘
Noted
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…