Haya sio mafuta ya kupikia kweli?

Haya sio mafuta ya kupikia kweli?

Dada,
Hayo ni mafuta mazuri sana kwa ngozi na nywele. Ni mafuta bora kuliko mafuta ya aina yoyote unayoyajua chini ya jua kwa ajili ya kuitengeneza ngozi na nywele na ukawa na ngozi inayovutia daima na kila mtu akabaki kuishangaa ngozi yako ilivyo nzuri. Kuhusu kunukia hayo mafuta hayana harufu mbaya, kwahiyo wewe baada ya kupaka hayo mafuta unaweza ukajipulizia perfume ili unukie kama unataka kunukia.
Pia hayo mafuta unaweza ukapikia ni mazuri pia kwa kupikia.
Ila watu wengi wenye ufahamu juu ya mafuta za mizeituni wanatumia kujipaka kwa kupenda kuwa na ngozi Bora na nzuri isiyo na makovu wala chunusi au mabaka mabaka.
Ni mafuta ghari sana kutokana na ubora wake, na kwakuwa ni mafuta ya mmea halisi mzeituni.
Mimi nakushauri penda kutumia mafuta hayo utakuwa mzuri zaidi wa ngozi na mengineyo, hachana na mafuta yote uliyokuwa unayatumia hata lotion.
Sawa ngoja nipake mpaka yaishe nione inakuwaje yakinipendeza ntapaka haya haya
 
Back
Top Bottom