Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Wanasiasa wa Kenya ambao waliutangazia Ulimwengu kwamba Katiba yao mpya ndo dawa ya matatizo yao yoote na kuisimika kwa mbwembwe nyiiingi huku wakisifiwa kila kona kwa ni Katiba bora siajabu kuliko zote Afrika kama siyo Duniani, sasa miaka michache baadaye Wanasiasa wale wale waliotaka Katiba leo hii wanataka nyingine tena na kuna kila dalili kwamba kura ya maoni itafanikiwa na kuanza mchakato wa Katiba mpya tena, mpaka kieleweke dadadeki, kama hata hiyo isipowaingiza madarakanai wataikataa tena, eti sasa hvi wanataka Cheo cha Waziri mkuu iweje hawakuliona hilo wakati wanaunda hii ya sasa, wakati walisema walishirikisha Wataalamu wa Katiba kutoka Dunia nzima?