GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Ni Kiungo ambaye hadi hivi sasa hajawahi kutokea nchini Tanzania hasa kutokana na aina ya uchezaji wake wa nafasi ya Kiungo na ule ' udambwi dambwi ' wake huku akiwa anatokea katika Klabu ya baraka nyingi za Mwenyezi Mungu ya Simba Sports Club anaitwa Shekhan Rashid.
Bahati nzuri ni Kiungo ambaye hata Wana Yanga SC wengi walikuwa wakimpenda na wakimkubali mno kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchezesha timu nafasi ya Kiungo huku akisaidiana vizuri sana na Kiungo mwenzake wa chini na Nahodha wake Selemani Matola a.k.a Veron a.k.a Mzambia.
Mlio katika tv / runinga zenu hebu ' bonyezeni ' Clouds tv katika Kipindi cha Sports Bar muweze kumuona Fundi wa mpira Mchezaji Shekhan Rashid akiwa anatiririka na anaserereka mbele ya ' Kioo ' huku akitoa ' madini ' yake hasa baada ya kuwa nje ya nchi huko nchini Sweden kwa muda mrefu.
Ni Kiungo ambaye nilikuwa nikimpenda sana na nilivyomuona leo amenifanya nimkumbuke sana Mtangazaji wa RTD na ambaye alikuwa ni ' Mnazi ' mkubwa wa Yanga Ahmed Jongo alipomsifia sana Shekhan Rashid katika ile mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa Zanzibar katika Kombe la Muungano huku akisema kwamba hajawahi kuona ' engine room ' nzuri kama iliyokuwepo kati ya Shekhan Rashid na Selemani Matola.
Nawasilisha.