Haya wale tunaojua mpira vizuri Fundi Shekhan Rashid yupo live Sports Bar Clouds tv

Haya wale tunaojua mpira vizuri Fundi Shekhan Rashid yupo live Sports Bar Clouds tv

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ni Kiungo ambaye hadi hivi sasa hajawahi kutokea nchini Tanzania hasa kutokana na aina ya uchezaji wake wa nafasi ya Kiungo na ule ' udambwi dambwi ' wake huku akiwa anatokea katika Klabu ya baraka nyingi za Mwenyezi Mungu ya Simba Sports Club anaitwa Shekhan Rashid.

Bahati nzuri ni Kiungo ambaye hata Wana Yanga SC wengi walikuwa wakimpenda na wakimkubali mno kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchezesha timu nafasi ya Kiungo huku akisaidiana vizuri sana na Kiungo mwenzake wa chini na Nahodha wake Selemani Matola a.k.a Veron a.k.a Mzambia.

Mlio katika tv / runinga zenu hebu ' bonyezeni ' Clouds tv katika Kipindi cha Sports Bar muweze kumuona Fundi wa mpira Mchezaji Shekhan Rashid akiwa anatiririka na anaserereka mbele ya ' Kioo ' huku akitoa ' madini ' yake hasa baada ya kuwa nje ya nchi huko nchini Sweden kwa muda mrefu.

Ni Kiungo ambaye nilikuwa nikimpenda sana na nilivyomuona leo amenifanya nimkumbuke sana Mtangazaji wa RTD na ambaye alikuwa ni ' Mnazi ' mkubwa wa Yanga Ahmed Jongo alipomsifia sana Shekhan Rashid katika ile mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa Zanzibar katika Kombe la Muungano huku akisema kwamba hajawahi kuona ' engine room ' nzuri kama iliyokuwepo kati ya Shekhan Rashid na Selemani Matola.

Nawasilisha.
 
Huyu jamaa alikuwa fundi sana.
Alianza kucheza Simba akiwa na umri Mdogo.
Umenikumbusha Simba ya
1. Tanzania one Mohammed Mwameja
2. Kimti
3. Dua Saidi
 
Mkuu, Shekhan hakucheza na hawa wahenga! Labda uwe umewakumbuka tu.

Nadhani Wewe ndiyo hujamuelewa Mkuu kwani amemtaja tu ' Fundi ' Shekhan Rashid na uwezo wake lakini akakisifia sana Kikosi chake Kizuri cha Simba hicho alichokitaja cha akina Mwameja, Kimti na Dua.
 
Nadhani Wewe ndiyo hujamuelewa Mkuu kwani amemtaja tu ' Fundi ' Shekhan Rashid na uwezo wake lakini akakisifia sana Kikosi chake Kizuri cha Simba hicho alichokitaja cha akina Mwameja, Kimti na Dua.
Naona leo nna stress Mkuu, maana siamini kama leo nalala bila kula Papa![emoji22]
 
jamaa alikuwa fundi enzi zake ukimuendea bila timing lazima akupige kanzu

Ila ilikuwa ukitaka umpende zaidi na uone ' mavituz ' yake nyuma yake awepo ' Mtaalam ' mwingine Selemani Matola ni balaa Mkuu. Pasi mpasuko, pasi mpenyeko, pasi mchanyato na pasi mnyumbuliko zilikuwa zinapigwa mno pale katikati huku Mashabiki wengi wa Simba Sports Club kila mara tukiwa ' tunatapika ' tu Majukwaani kwa furaha. Na usisahau wakati wao hawa akina Shekhan Rashid ' Kocha ' Mkuu alikuwepo Marehemu Mzee Aggrey Sianga ( R.I.P ) mno Kwake.
 
Nakumbuka alisajiliwa kutoka Mji Mpwapwa iliyokuwa inalelewa na Mbunge wao George Lubeleje na matajiri wa mji ule.
Jamaa alikuwa fundi haswaa....hivi ile simba si ndio ilikuwa ikiwadhalilisha wa-Misri?
 
Simba hiyo ilikuwa:
  1. Juma Kaseja
  2. Said Swedi
  3. Ramadhan Wasso
  4. Boniface Pawasa
  5. Patrick Betwell ' Buba ' Mchezaji Kipenzi changu na Mmasai anayejua kucheza mpira hadi anakera
  6. Seleman Matola a.k.a Veron a.k.a Mzambia
  7. Steven Mapunda a.k.a Garincha
  8. Shekhan Rashid a.k.a Injini
  9. Joseph Kaniki a.k.a Golota
  10. Emanuel Gabriel Mwakyusa a.k.a Batigol
  11. Ulimboka Mwakingwe
Simba hii kila wakati ' Mashabiki ' majukwaani tulikuwa ' tunatapika / tunashangilia ' tu kwa raha zetu huku wengi wetu tukiwa muda wote tunakula ' Bisi ' na Vinywaji baridi meno yote 32 nje kama ' Ngisi ' vile.
 
Umemsahau Mark Selengo yule mkenya
 
Umemsahau Mark Selengo yule mkenya

Huyo alikuja baadae kabisa Mkuu au umesahau tena! Unaniangusha bhana kwani hizi Kumbukumbu ukiwa mwana Simba Sports Club wa Kindakindaki huwezi ukazisahau mapema yote hii. Mtafute mwana Simba SC yoyote atakukumbusha zadi juu ya hili tafadhali.
 
Simba hiyo ilikuwa:
  1. Juma Kaseja
  2. Said Swedi
  3. Ramadhan Wasso
  4. Boniface Pawasa
  5. Patrick Betwell ' Buba ' Mchezaji Kipenzi changu na Mmasai anayejua kucheza mpira hadi anakera
  6. Seleman Matola a.k.a Veron a.k.a Mzambia
  7. Steven Mapunda a.k.a Garincha
  8. Shekhan Rashid a.k.a Injini
  9. Joseph Kaniki a.k.a Golota
  10. Emanuel Gabriel Mwakyusa a.k.a Batigol
  11. Ulimboka Mwakingwe
Simba hii kila wakati ' Mashabiki ' majukwaani tulikuwa ' tunatapika / tunashangilia ' tu kwa raha zetu huku wengi wetu tukiwa muda wote tunakula ' Bisi ' na Vinywaji baridi meno yote 32 nje kama ' Ngisi ' vile.
Mwaka huu hamtapiki?
 
Mwaka huu hamtapiki?

Tutatapika tena kwa Kikosi hiki Jumamosi ya wiki hii:
  1. Aishi Manula
  2. Erasto Nyoni
  3. Mohamed Hussein Zimbwe Jr ' Tshabalala '
  4. Juuko Murshid
  5. Method Mwanjale ( Captain )
  6. Jonas Gerald Mkude ' Xavi '
  7. James Kotei
  8. Muzamiru Yasin
  9. Emanuel Okwi
  10. Haruna Niyonzima
  11. Shiza Kichuya
Kipindi cha pili tutawaingiza hawa tu kumaliza Kazi na ' watutapishe ' zaidi:
  1. Mohamed Ibrahim ' Mo '
  2. Said Khamis Ndemla
  3. Nicolas Gyan
  4. Laudit Mavugo
Je una swali lingine tena Mkuu?
 
Huyo alikuja baadae kabisa Mkuu au umesahau tena! Unaniangusha bhana kwani hizi Kumbukumbu ukiwa mwana Simba Sports Club wa Kindakindaki huwezi ukazisahau mapema yote hii. Mtafute mwana Simba SC yoyote atakukumbusha zadi juu ya hili tafadhali.
Hahaaa kweli mkuu nilichanya japo ilikuwa ni mwishoni mwa akina Joseph kaniki na Nteze John Rungu
 
Simba hiyo ilikuwa:
  1. Juma Kaseja
  2. Said Swedi
  3. Ramadhan Wasso
  4. Boniface Pawasa
  5. Patrick Betwell ' Buba ' Mchezaji Kipenzi changu na Mmasai anayejua kucheza mpira hadi anakera
  6. Seleman Matola a.k.a Veron a.k.a Mzambia
  7. Steven Mapunda a.k.a Garincha
  8. Shekhan Rashid a.k.a Injini
  9. Joseph Kaniki a.k.a Golota
  10. Emanuel Gabriel Mwakyusa a.k.a Batigol
  11. Ulimboka Mwakingwe
Simba hii kila wakati ' Mashabiki ' majukwaani tulikuwa ' tunatapika / tunashangilia ' tu kwa raha zetu huku wengi wetu tukiwa muda wote tunakula ' Bisi ' na Vinywaji baridi meno yote 32 nje kama ' Ngisi ' vile.
Sijamuona Marehemu Christopher Alex "Massawe"
 
Sijamuona Marehemu Christopher Alex "Massawe"

Marehemu alikuwa ' anasubiri ' kwa Kipenzi changu Patrick Betwell ' Buba ' Mmasai ' Kamarada ' wangu. Huyo Betwell alikuwa anaujua mpira hadi wengi tulikuwa tunashangaa na kujiuliza ni kwanini hakutaka kwenda Ulaya kwani asingekosa Timu. Hivi sasa yupo zake tu Mkoani Ruvuma ( Songea ) anavuna Mahindi na kushinda tu kunywa Gongo japo makazi yake mengine ni Mkoani Morogoro. Kuna wakati ' Rafiki ' yangu mmoja aliniambia alimuona ' Vibanda ' vya Gongo pale eneo la ' Manzese ' Mkoani Morogoro jirani na Uwanja ule wa Sabasaba akiwa ' kalewa ' chakari na Gongo niliumia, nilihuzunika na kusikitika sana ' Kamarada '.
 
Back
Top Bottom