Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante koku
Ameen Mpenda Yesu.
Basi na tuendelee kupata barak za bwana katika uombaji
HAYA EE MOYO WANGU.
1.Haya ee moyo wangu, imba kwa furaha
Umwimbie muumbaji, mbingu na dunia
Atukuzwaye pote umsifu na wewe
Kwa nguvu zako zoote umri wako wote
2.Mungu wake Yakobo ndiye Mungu wetu.
Ukimchagua yeye, una fungu jema.
Unacho ktu chema, umepata mali.
Moyo utakung'aa, shida zitakwisha.
3.Ni mwenye nguvu nyingi, hana amshindaye.
Kwa hekima, aumba, vyote ni vya ajabu.
Misitu na mabonde, milima na mashamba.
Vilivyo baharini, wanyma porini
4.Ana mizungu mingi, kuponya wanawe,
Anawapa riziki, hata siku za njaa.
Wenye chakula haba, wanenepa miili
Hata waliofungwa, anawafungua.
5.Mashangilio yote, hayamtoshi yeye.
Ni mwema peke yake, nami ni vumbi tu
Ananihurumia, kwa kuwa ni wake.
Kwa hiyo nalikuza jina lake pote
Amen, na tuimbe kwa zeze na vinubi
Kwala zote katika kuufurahia utukufu wa Mungu katika uumbaji.Kayamba na vinanda..Amen
Nimesoma hii thread nimepata wepesi.......kwa nini thread nzuri kama hizi ni nadra sana humu.....
Haya sasa......tuimbe pamoja hii.....
Pana jito lina maji mazuri .......
kitabu changu sijui nani kanionea? Asprin, wapi chuo changu kidogo cha sala?Moja mbili, tatu tuimbe.....
1.Pana jito lina maji mazuri, yaenda ulimwenguni.
Lameta meta nalo linang'aa, walijua jito hilo?
CHORUS
Ninakuita nawe njoo
Utafute jito hilo
Maji yake yapooza moyo.
Nawe yateke unywe.
2. Wanywayo maji haya wafurahi, waimba kwa shangwe kubwa
Makosa na shida yanaondoshwa, wote waoshwa na BWANA.
3. Jito hili latoa maji mengi, matamu yapendezayo.
Yaponya wagonjwa yatia nguvu, uchafu watakasika.
4. Maji ya jito hilo ni uzima,unaotoka kwa YESU.
Damu yake yenye kiasi kikuu, imemwagwa tusafike.
Endelea kupata baraka za uimbaji Preta
ha haaa, kaa mkao wa kuburudika na KUBARIKIWA
ha haaa, kaa mkao wa kuburudika na KUBARIKIWA
Praaaaaaaaaraise the Lord!!!!