Haya wana Chit-Chat,TUIMBE SOTE!!

Haya wana Chit-Chat,TUIMBE SOTE!!

Kima Mchanga ubarikiwe saaaaana.

Na ninavyopenda kuimba . . . nimeimbaje kwa sautiiiiiiii!!!

Asante mpenzi.
 
Last edited by a moderator:
Moja mbili, tatu tuimbe.....

1.Pana jito lina maji mazuri, yaenda ulimwenguni.
Lameta meta nalo linang'aa, walijua jito hilo?

CHORUS
Ninakuita nawe njoo
Utafute jito hilo
Maji yake yapooza moyo.
Nawe yateke unywe.

2. Wanywayo maji haya wafurahi, waimba kwa shangwe kubwa
Makosa na shida yanaondoshwa, wote waoshwa na BWANA.

3. Jito hili latoa maji mengi, matamu yapendezayo.
Yaponya wagonjwa yatia nguvu, uchafu watakasika.

4. Maji ya jito hilo ni uzima,unaotoka kwa YESU.
Damu yake yenye kiasi kikuu, imemwagwa tusafike.

Endelea kupata baraka za uimbaji Preta

Naupenda sana huu wimbo....
 
Ameen Mpenda Yesu.

Basi na tuendelee kupata barak za bwana katika uombaji

HAYA EE MOYO WANGU.



1.Haya ee moyo wangu, imba kwa furaha
Umwimbie muumbaji, mbingu na dunia
Atukuzwaye pote umsifu na wewe
Kwa nguvu zako zoote umri wako wote

2.Mungu wake Yakobo ndiye Mungu wetu.
Ukimchagua yeye, una fungu jema.
Unacho ktu chema, umepata mali.
Moyo utakung'aa, shida zitakwisha.

3.Ni mwenye nguvu nyingi, hana amshindaye.
Kwa hekima, aumba, vyote ni vya ajabu.
Misitu na mabonde, milima na mashamba.
Vilivyo baharini, wanyma porini

4.Ana mizungu mingi, kuponya wanawe,
Anawapa riziki, hata siku za njaa.
Wenye chakula haba, wanenepa miili
Hata waliofungwa, anawafungua.

5.Mashangilio yote, hayamtoshi yeye.
Ni mwema peke yake, nami ni vumbi tu
Ananihurumia, kwa kuwa ni wake.
Kwa hiyo nalikuza jina lake pote

Uzi wa kitambo ila nyimbo zimenigusa

Ubarikiwe
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini wataka kungojaa..ondoka upesi ndugu.
Bwana Yesu ataka kukupa..pumziko na raha telee.

Mbona mbona mbona hutaki kumjiaa
Mbona mbona mbona hupendi raha................




Sent from my SM-A510F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom