Ngoja aje mpekuzi wa mambo ya ndani njaakalihatari aweke bayana, ninachojua Matola ni Kocha MsaidiziHivi kazi ya Matola pale Simba ni nini????????????????????????????
Asaivi mna bilion26 plus billion 20 kweli matajiri.Uongozi umeshindwa kuleta wachezaji Bora kama
Victoria Adebayo.
Stephen Azizi key.
Lobi Cesar Manzoki.
Harve Ngomo.
Luis Joseph Miquesson .
Bobosi.
Fabrice Ngoma.
Sopu nk
Bilioni 20 inafanya nini.
Mkude sijui ana kitu gani maana kila mchezaji akisajiliwa kwenye namba anayo cheza yeye basi lazima mchezaji huyo atapata majeraha ya kuachwa na timu kabisa ila kwa Lwanga wamebugi kumuachaKuhusu Mkude ni kuwa wanaojua mpira wameishamchabua sana udhaifu wake hapa lakini viongozi wameziba masikio. Na mbaya zaidi kila kocha anayekuja anamtumia sijui ana nini kinchomsaidia mpaka hata makocha wazungu nao wanazima fegi hawaoni mapungufu yake. Mashabiki wa Simba wale hoya hoya huwaambii kitu kuhusu Mkude. Kiujumla jamaa ana nyota kali sana ya kupendwa. Mkude hana mbio, ana "anticipation" ndogo sana, hawezi kupora mipira na muda wote anakabia macho. Derby nyingi sana anachomesha lakini mpaka uujue mpira vizuri ndio utaweza kutambua anachomeshaje. Inonga na Outara walionekana kama mabeki wa sekondari kwa sababu hakukuwa na mtu mwenye uwezo wa Fraga au Tadeo kuwalinda wao wakutane na "second attempt".
Benchi la ufundi nalo hovyo kabisa. Kwa takribani wiki tatu walizokaa Misri wameshindwa kutengeneza kiungo mkabaji ndani ya takribani wachezaji 30 waliosajiliwa maana wakati mwingine kwa kocha mbunifu anatengeneza mchezaji kutokana na mapungufu aliyonayo. Na watu wasikariri kuwa eti lazima kiungo mkabaji lazima asajiliwe mpya. Ni kiasi tu cha kumbadilisha mtu kama Akpan au hata Outara nikiwaangalia haraka haraka wanaweza kubadilishwa na wakafanya vizuri kwa kiasi fulani sio lazima iwe 100% mpaka dirisha dogo ndipo asajiliwe mchezaji kwenye hiyo nafasi.
Kazi anayofanya Mkude katikati pale Simba hata ukimchukua kiungo wa Simba "B" anweza kuifanya hiyo kazi ya kupiga "square pass" . Kwenye mechi nzima sidhani kama "penetration pass"kutoka kwa Mkude zinafika hata tano.
Wewe hizi mechi za karibuni umemwona phiri,, au ndo nyinyi mashabiki matukio??Kwa vyovyote vile Kocha alizingua kuanzia Kikosi cha mwanzo mpaka Sub yake, sijui kwa nini Kocha alimuacha Phiri na hata Akpan hakucheza, naendelea kufanya utafiti na nitakuja na majibu soon.
Kuhusu Kocha Nabi kukaa miaka 2 na kikosi ndo maana nikasema kwa Simba wakati ule tulihitaji wachezaji wa kusupport kikosi kilichopo.
Sina maana nadharau baadhi ya wachezaji la hasha, ila mabadiliko kwa wachezaji kuingia na kutoka ni jambo la kawaida.
Mkuu umemaliza kila kitu . Kanywe soda pale nakuja kulipa.tuache kumlaumu kocha kwa makosa ya viongozi,
kocha alijitahidi sana kulingana na aina ya wachezaji alionao, kosa lake kubwa ni kumtoa chama tu,
huwezi kuwa na malengo makubwa huku umejaza wachezaji aina ya boko, dejan na mkude pale mbele na katikati,
huwezi kuwa na malengo ya kufika nusu final ya caf champions league halafu unashindwa kumchukua striker mkali kwa tsh 400mls, viongozi hawako siriazi,
wakati Uchebe anaondoka alituambia namnukuu "ili simba ipige hatua inahitaji kuwaondoa viongozi wasio na elimu katika bodi" mwisho wa kunukuu.
Phiri hakuwepo kwenye PRE-SEASON na hakucheza game yoyote kule Misri?Wewe hizi mechi za karibuni umemwona phiri,, au ndo nyinyi mashabiki matukio??
Akizungumza kwenye Pre-Meeting ya Watani wa Jadi Simba SC na Yanga SC, Kocha Zaron Maki alisema kuwa amekutana na derby nyingi, huku akiamini kuwa ubora wa wachezaji ndo unaamua mechi kushinda na sio ubora wa mbinu ndani ya uwanja, kwani game kubwa huamuliwa na mambo kama Kona au Free Kick.
Kwangu Ghazwat, hili lilikuwa kosa kubwa sana alifanya Zaron Maki, kwani hapa ni dhahiri ameshindwa kumuheshimu mpinzani wake, ameleta dharau na ndo maana aliamua kuingia na kikosi cha kawaida mno hali iliyosababisha kufungwa kizembe na ndo kilikuwa Kiini hasa cha matokeo.
Kwahivyo ili kuweza kufikia malengo ya timu, Viongozi wa Simba wamwambie Kocha abadilike kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF kuanza, aache dharau na kukariri na mambo ya Morocco, Sudan na Angola, na kwa game dhidi ya Yanga, Nabi ndo ameonekana kuzijua zaidi game za Derby, na amekumbushwa la kufanya.
April 30 2022, niliandika Uzi kuhusu Kocha Pablo Flanco Martin kuwa ni Kocha nzuri sana ila anahitaji wachezaji Quality, hapa ni wachache sana walielewa hii Nukta akiwepo Pettymagambo na Goguryeo asanteni sana nyie Wanamsimbazi
Pablo Flanco ni kocha aliyemsumbua sana Nabi kimbinu ingawa alikuwa na wachezaji wa kawaida, tofauti na sasa, Kocha Nabi ili aweze kumfunga Pablo ilikuwa lazima baadhi ya wachezaji katika kikosi cha Simba kuwa majeruhi, na pia alifanya vizuri Kimataifa kwa matokeo ya ndani na nje hasa game dhidi ya Orlando Pirates.
Kuelekea msimu wa Ligi Kuu na michuano CAF, Simba SC wanahitaji Defensive Midfielder, (DM) na siku zote hakuna mabeki wazuri kama hakuna Defensive Midfielder, Simba SC inahitaji Proper Replacement ya Prime Kanoute.
Haya ndo mambo yakufanya kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF, ili kubaki na mwendo wa ngiri tu meno nje, naona baadhi wengine wamesusa na wakafika mbali zaidi kwamba viongozi waache ngazi, mashabiki waache kwenda uwanjani haya yote sidhani kama ni sahihi kwa sasa, na si afya kwenye medani ya soka, hii ni Simba yetu Nguvu Moja.[emoji881]
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Yaani Iko hivi hawa viongozi wa Simba ni wapigaji wanatafuta wachezaji wabovu wawauze kwa jina Simba kupitia Barbra, ndio maana ukamsikia anataka amuuze sakho sasa embu muulize akimuuza sakho anabakiwa na nani.Pale samba hatuna viongozi wafia clab wote wale mamluki wanawaza kula hela za Mo, natamani watoke wote tuanze moja.inaumiza sana, halafu haitoshi kiongozi huyohuyo anayetusajilia kapama na dejan ndio huyo huyo anataka kumuuza sakho!
na huyohuyo anataka timu ifike nusu final ya caf champions league,
daah! salaaale.
Sasa hivi ndio mnaanza kuyajua madhaifu ya timu yenu sio?mshachelewa.Ukienda Yanga huwakuti hata kama walikuwa na majina as longer Hana uwezo wa kuchezea tena timu anapewa mkono wa shukrani ila huku Simba wamekumbatiwa na kusifiwa
Kanoute na chama waliweza kuidhibiti Yanga half ya kwanza sababu tu farid na sure boy walishindwa kutekeleza majukumu yao huku aziz ki akiwa anatokea pembeni,simba mkafanikiwa kuchukua eneo la kati,nabi alipogundua hilo half ya pili ile sub timu ikaanza kutembea,fei alirudi namba 8,ki akaenda namba 10,wings zote zikawa zinatembea,chama mzuri timu ikicheza lkn sio ikishambuliwa huku huyo kanoute tayari alikua na yellow wakati Yanga iko chini,Yanga ilipoanza kutembea kwa akili yule chogo na mirafu yake angekula umeme fasta,yule kocha wenu makolo bonge la kocha bila yule kwa ile sub siku ile mngechezea goli za kutosha,ile sub iliwasaidia sana kuja kuzuiaKanoute alikuja vema mpaka kuna Uzi yeye na Sakho nikiwaelezea lakini sasa kuna kitu hakiko sawa upande wake, ana rafu ambazo si lazima kufanya.
Kwahivyo kwenye michezo kama hii ukimtoa Kanoute, mbadala (anayeingia) anatakiwa kuwa kama yeye au zaidi yake tutaendelea kujiuliza kwanini Akpan hakucheza ndo maana nikasema Kocha Zaron Maki alizidiwa mbinu ya Kocha Nabi.
Kwa upande wangu naona Kile alichoingia nacho ni kikosi dhaifu kwa maana kilikuwa na wachezaji baadhi wasioanza kwenye 1st 11 ambalo ni kosa na dharau kwa mpizani. Makosa ya Mwenda yalikuwa mengi na asingefanya makosa yale mtu kama kapombe.Hii pointi ya kusema kocha aliingia na kikosi dhaifu sio kweli, wale wote ni wachezaji wa Simba SC na lazima waungwe mkono, na wao ndio waliocheza mpira mwingi kipindi cha kwanza tukaenda mapumziko tunaongoza 1-0.
Kipindi cha pili ndio mambo yakabadilika, mbinu alizokuja nazo kocha wa Yanga ndio ziliiua Simba hasa sehemu ya kiungo cha chini Mkude akapotezwa, na sub alizokuja kuzifanya kocha wa Simba SC ndio zikaiua kabisa timu, hapa sioni kama kocha wa Simba aliwadharau Yanga.
Kwangu mimi ile mechi tulipoteza kwa kuzidiwa na mbinu za wapinzani pamoja na uwezo wa wachezaji walionao kutimiza maelekezo wanayopewa na kocha wao, sisi kocha wetu alifanya mabadiliko ambayo hayakuisaidia timu.
Kocha wa Simba SC simlaumu sana, bado namuona ni mpya, hajawafahamu vizuri wachezaji alionao na ajue ni vipi awatumie ili kupata matokeo, hii ni tofauti na Nabi ambaye amekaa na kikosi cha Yanga karibia mwaka wa pili sasa, kocha apewe muda atengeneze timu. Mtu kama Phiri nataka apewe nafasi ya kutosha arudishe match fitness yake bado naamini ubora anao.