Haya ya kufanyiwa kazi haraka Simba SC kabla ya kuanza Ligi Kuu na michuano ya CAF

Haya ya kufanyiwa kazi haraka Simba SC kabla ya kuanza Ligi Kuu na michuano ya CAF

Kuhusu Mkude ni kuwa wanaojua mpira wameishamchabua sana udhaifu wake hapa lakini viongozi wameziba masikio. Na mbaya zaidi kila kocha anayekuja anamtumia sijui ana nini kinchomsaidia mpaka hata makocha wazungu nao wanazima fegi hawaoni mapungufu yake. Mashabiki wa Simba wale hoya hoya huwaambii kitu kuhusu Mkude. Kiujumla jamaa ana nyota kali sana ya kupendwa. Mkude hana mbio, ana "anticipation" ndogo sana, hawezi kupora mipira na muda wote anakabia macho. Derby nyingi sana anachomesha lakini mpaka uujue mpira vizuri ndio utaweza kutambua anachomeshaje. Inonga na Outara walionekana kama mabeki wa sekondari kwa sababu hakukuwa na mtu mwenye uwezo wa Fraga au Tadeo kuwalinda wao wakutane na "second attempt".

Benchi la ufundi nalo hovyo kabisa. Kwa takribani wiki tatu walizokaa Misri wameshindwa kutengeneza kiungo mkabaji ndani ya takribani wachezaji 30 waliosajiliwa maana wakati mwingine kwa kocha mbunifu anatengeneza mchezaji kutokana na mapungufu aliyonayo. Na watu wasikariri kuwa eti lazima kiungo mkabaji lazima asajiliwe mpya. Ni kiasi tu cha kumbadilisha mtu kama Akpan au hata Outara nikiwaangalia haraka haraka wanaweza kubadilishwa na wakafanya vizuri kwa kiasi fulani sio lazima iwe 100% mpaka dirisha dogo ndipo asajiliwe mchezaji kwenye hiyo nafasi.

Kazi anayofanya Mkude katikati pale Simba hata ukimchukua kiungo wa Simba "B" anweza kuifanya hiyo kazi ya kupiga "square pass" . Kwenye mechi nzima sidhani kama "penetration pass"kutoka kwa Mkude zinafika hata tano.
 
Uongozi umeshindwa kuleta wachezaji Bora kama

Victoria Adebayo.
Stephen Azizi key.
Lobi Cesar Manzoki.
Harve Ngomo.
Luis Joseph Miquesson .
Bobosi.
Fabrice Ngoma.
Sopu nk

Bilioni 20 inafanya nini.
Asaivi mna bilion26 plus billion 20 kweli matajiri.
 
Simba imemuacha Lwanga kwa haraka sana, pale simba kuna kundi linakazi ya kunadi wachezaji na kuponda wengine lwanga alitibu tatizo la defensive kazi ambayo mkude ilikuwa ngumu kwake mpka akasajiliwa yeye matokeo yake pamoja na kupona majeraha wamemtema na kumuacha mkude aliewahi kuwa na mapungufu kwenye kiungo wa chini,
Same applied kwa Fraga yote hiyo ni kumlinda mtu.
 
Kuhusu Mkude ni kuwa wanaojua mpira wameishamchabua sana udhaifu wake hapa lakini viongozi wameziba masikio. Na mbaya zaidi kila kocha anayekuja anamtumia sijui ana nini kinchomsaidia mpaka hata makocha wazungu nao wanazima fegi hawaoni mapungufu yake. Mashabiki wa Simba wale hoya hoya huwaambii kitu kuhusu Mkude. Kiujumla jamaa ana nyota kali sana ya kupendwa. Mkude hana mbio, ana "anticipation" ndogo sana, hawezi kupora mipira na muda wote anakabia macho. Derby nyingi sana anachomesha lakini mpaka uujue mpira vizuri ndio utaweza kutambua anachomeshaje. Inonga na Outara walionekana kama mabeki wa sekondari kwa sababu hakukuwa na mtu mwenye uwezo wa Fraga au Tadeo kuwalinda wao wakutane na "second attempt".

Benchi la ufundi nalo hovyo kabisa. Kwa takribani wiki tatu walizokaa Misri wameshindwa kutengeneza kiungo mkabaji ndani ya takribani wachezaji 30 waliosajiliwa maana wakati mwingine kwa kocha mbunifu anatengeneza mchezaji kutokana na mapungufu aliyonayo. Na watu wasikariri kuwa eti lazima kiungo mkabaji lazima asajiliwe mpya. Ni kiasi tu cha kumbadilisha mtu kama Akpan au hata Outara nikiwaangalia haraka haraka wanaweza kubadilishwa na wakafanya vizuri kwa kiasi fulani sio lazima iwe 100% mpaka dirisha dogo ndipo asajiliwe mchezaji kwenye hiyo nafasi.

Kazi anayofanya Mkude katikati pale Simba hata ukimchukua kiungo wa Simba "B" anweza kuifanya hiyo kazi ya kupiga "square pass" . Kwenye mechi nzima sidhani kama "penetration pass"kutoka kwa Mkude zinafika hata tano.
Mkude sijui ana kitu gani maana kila mchezaji akisajiliwa kwenye namba anayo cheza yeye basi lazima mchezaji huyo atapata majeraha ya kuachwa na timu kabisa ila kwa Lwanga wamebugi kumuacha

na wawe makini Yanga pale wakimnasa watamtumia vizuri kwa yule beki wao mvivu Bakari Nondo arelax
 
Kwa vyovyote vile Kocha alizingua kuanzia Kikosi cha mwanzo mpaka Sub yake, sijui kwa nini Kocha alimuacha Phiri na hata Akpan hakucheza, naendelea kufanya utafiti na nitakuja na majibu soon.

Kuhusu Kocha Nabi kukaa miaka 2 na kikosi ndo maana nikasema kwa Simba wakati ule tulihitaji wachezaji wa kusupport kikosi kilichopo.

Sina maana nadharau baadhi ya wachezaji la hasha, ila mabadiliko kwa wachezaji kuingia na kutoka ni jambo la kawaida.
Wewe hizi mechi za karibuni umemwona phiri,, au ndo nyinyi mashabiki matukio??
 
tuache kumlaumu kocha kwa makosa ya viongozi,

kocha alijitahidi sana kulingana na aina ya wachezaji alionao, kosa lake kubwa ni kumtoa chama tu,

huwezi kuwa na malengo makubwa huku umejaza wachezaji aina ya boko, dejan na mkude pale mbele na katikati,

huwezi kuwa na malengo ya kufika nusu final ya caf champions league halafu unashindwa kumchukua striker mkali kwa tsh 400mls, viongozi hawako siriazi,

wakati Uchebe anaondoka alituambia namnukuu "ili simba ipige hatua inahitaji kuwaondoa viongozi wasio na elimu katika bodi" mwisho wa kunukuu.
Mkuu umemaliza kila kitu . Kanywe soda pale nakuja kulipa.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Wewe hizi mechi za karibuni umemwona phiri,, au ndo nyinyi mashabiki matukio??
Phiri hakuwepo kwenye PRE-SEASON na hakucheza game yoyote kule Misri?

Phiri hakuwepo sehemu ya mchezo kwenye game dhidi ya Saint George?

Sasa kusema hivi karibuni unamaanisha nini..? Ficha Ujinga Wako.
 
Hapo hakuna kocha. Wqtuletee hata Gomez tu. Kwa simba ya juzi angekua Gomez tungepiga mtu sio chini ya 3 kwa 0
Akizungumza kwenye Pre-Meeting ya Watani wa Jadi Simba SC na Yanga SC, Kocha Zaron Maki alisema kuwa amekutana na derby nyingi, huku akiamini kuwa ubora wa wachezaji ndo unaamua mechi kushinda na sio ubora wa mbinu ndani ya uwanja, kwani game kubwa huamuliwa na mambo kama Kona au Free Kick.

Kwangu Ghazwat, hili lilikuwa kosa kubwa sana alifanya Zaron Maki, kwani hapa ni dhahiri ameshindwa kumuheshimu mpinzani wake, ameleta dharau na ndo maana aliamua kuingia na kikosi cha kawaida mno hali iliyosababisha kufungwa kizembe na ndo kilikuwa Kiini hasa cha matokeo.

Kwahivyo ili kuweza kufikia malengo ya timu, Viongozi wa Simba wamwambie Kocha abadilike kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF kuanza, aache dharau na kukariri na mambo ya Morocco, Sudan na Angola, na kwa game dhidi ya Yanga, Nabi ndo ameonekana kuzijua zaidi game za Derby, na amekumbushwa la kufanya.

April 30 2022, niliandika Uzi kuhusu Kocha Pablo Flanco Martin kuwa ni Kocha nzuri sana ila anahitaji wachezaji Quality, hapa ni wachache sana walielewa hii Nukta akiwepo Pettymagambo na Goguryeo asanteni sana nyie Wanamsimbazi

Pablo Flanco ni kocha aliyemsumbua sana Nabi kimbinu ingawa alikuwa na wachezaji wa kawaida, tofauti na sasa, Kocha Nabi ili aweze kumfunga Pablo ilikuwa lazima baadhi ya wachezaji katika kikosi cha Simba kuwa majeruhi, na pia alifanya vizuri Kimataifa kwa matokeo ya ndani na nje hasa game dhidi ya Orlando Pirates.

Kuelekea msimu wa Ligi Kuu na michuano CAF, Simba SC wanahitaji Defensive Midfielder, (DM) na siku zote hakuna mabeki wazuri kama hakuna Defensive Midfielder, Simba SC inahitaji Proper Replacement ya Prime Kanoute.

Haya ndo mambo yakufanya kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF, ili kubaki na mwendo wa ngiri tu meno nje, naona baadhi wengine wamesusa na wakafika mbali zaidi kwamba viongozi waache ngazi, mashabiki waache kwenda uwanjani haya yote sidhani kama ni sahihi kwa sasa, na si afya kwenye medani ya soka, hii ni Simba yetu Nguvu Moja.[emoji881]

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
 
simba hata turudiane na Yanga kesho tutafungwa tu... Tuseme ukweli ile formation yao ya Morrison Mayele Azizi Moloko ni beki gani wanaweza kuwatuliza hawa watu..? Yanga ukiikaba kushoto katikati inakufunga, ukiikaba katikati basi Morrison au Azizi hakuachi salama... Mkitaka tuifunge Yanga basi yule beki wao Mwamnyeto acheze dakika 90 halafu Bangala asicheze... Simba hatuna forward za kutisha
 
inaumiza sana, halafu haitoshi kiongozi huyohuyo anayetusajilia kapama na dejan ndio huyo huyo anataka kumuuza sakho!

na huyohuyo anataka timu ifike nusu final ya caf champions league,

daah! salaaale.
Yaani Iko hivi hawa viongozi wa Simba ni wapigaji wanatafuta wachezaji wabovu wawauze kwa jina Simba kupitia Barbra, ndio maana ukamsikia anataka amuuze sakho sasa embu muulize akimuuza sakho anabakiwa na nani.Pale samba hatuna viongozi wafia clab wote wale mamluki wanawaza kula hela za Mo, natamani watoke wote tuanze moja.
 
Ili kuna kitu kimoja kinanishangaza. Jinsi watu wanavyo changia kwa uchungu ingekuwa hivyohivyo kuichangia timu kwa fedha.

Mfano sisi mashabiki milioni 10 wa Simba kila mmoja achangie shilingi laki 1. Bilioni moja isaidie usajili. Tungekuwa tuna uhalali wa 100% kulalamikia uwekezaji wetu.

Hata huko Yanga wanao chekelea sasa wakiombwa kuchangia kiasi kama hicho sijui kama watatokea.

Hizi timu ziandae utaratibu watu wawekeze pesa ya kutosha sio ya vibakuli.

Sasa watu timu ikifungwa hawalali, lakini ukiuliza umechangia nini hakuna.
 
Ukienda Yanga huwakuti hata kama walikuwa na majina as longer Hana uwezo wa kuchezea tena timu anapewa mkono wa shukrani ila huku Simba wamekumbatiwa na kusifiwa
Kuna kiungo Punda na kiungo Nungunungu.
 
Ukienda Yanga huwakuti hata kama walikuwa na majina as longer Hana uwezo wa kuchezea tena timu anapewa mkono wa shukrani ila huku Simba wamekumbatiwa na kusifiwa
Sasa hivi ndio mnaanza kuyajua madhaifu ya timu yenu sio?mshachelewa.
 
Simba hii inasikitisha sna, Babra team imemshinda huyu, nakumbuka wenzake waliijenga team akairithi ikiwa nzuri il alipoingia tu project ya kwanza ikawa kuuza key players chama na Luis, alaf akasajili watt wakina Banda, nyoni sjui wakwap.

Nilidhan dirisha hili tungekuwa very aggressive cha kushangaza licha ya usajili ila bado team inategemea Mzamiru na Mkude, Boko wakupe positive results.

Mara unasajili Kyombo kweli ndo awe mkombozi? Hata Sopu hatukumuona? Jamn hii Simba hapa kuna tatizo kubwa.
 
Kanoute alikuja vema mpaka kuna Uzi yeye na Sakho nikiwaelezea lakini sasa kuna kitu hakiko sawa upande wake, ana rafu ambazo si lazima kufanya.

Kwahivyo kwenye michezo kama hii ukimtoa Kanoute, mbadala (anayeingia) anatakiwa kuwa kama yeye au zaidi yake tutaendelea kujiuliza kwanini Akpan hakucheza ndo maana nikasema Kocha Zaron Maki alizidiwa mbinu ya Kocha Nabi.
Kanoute na chama waliweza kuidhibiti Yanga half ya kwanza sababu tu farid na sure boy walishindwa kutekeleza majukumu yao huku aziz ki akiwa anatokea pembeni,simba mkafanikiwa kuchukua eneo la kati,nabi alipogundua hilo half ya pili ile sub timu ikaanza kutembea,fei alirudi namba 8,ki akaenda namba 10,wings zote zikawa zinatembea,chama mzuri timu ikicheza lkn sio ikishambuliwa huku huyo kanoute tayari alikua na yellow wakati Yanga iko chini,Yanga ilipoanza kutembea kwa akili yule chogo na mirafu yake angekula umeme fasta,yule kocha wenu makolo bonge la kocha bila yule kwa ile sub siku ile mngechezea goli za kutosha,ile sub iliwasaidia sana kuja kuzuia
 
Hii pointi ya kusema kocha aliingia na kikosi dhaifu sio kweli, wale wote ni wachezaji wa Simba SC na lazima waungwe mkono, na wao ndio waliocheza mpira mwingi kipindi cha kwanza tukaenda mapumziko tunaongoza 1-0.

Kipindi cha pili ndio mambo yakabadilika, mbinu alizokuja nazo kocha wa Yanga ndio ziliiua Simba hasa sehemu ya kiungo cha chini Mkude akapotezwa, na sub alizokuja kuzifanya kocha wa Simba SC ndio zikaiua kabisa timu, hapa sioni kama kocha wa Simba aliwadharau Yanga.

Kwangu mimi ile mechi tulipoteza kwa kuzidiwa na mbinu za wapinzani pamoja na uwezo wa wachezaji walionao kutimiza maelekezo wanayopewa na kocha wao, sisi kocha wetu alifanya mabadiliko ambayo hayakuisaidia timu.

Kocha wa Simba SC simlaumu sana, bado namuona ni mpya, hajawafahamu vizuri wachezaji alionao na ajue ni vipi awatumie ili kupata matokeo, hii ni tofauti na Nabi ambaye amekaa na kikosi cha Yanga karibia mwaka wa pili sasa, kocha apewe muda atengeneze timu. Mtu kama Phiri nataka apewe nafasi ya kutosha arudishe match fitness yake bado naamini ubora anao.
Kwa upande wangu naona Kile alichoingia nacho ni kikosi dhaifu kwa maana kilikuwa na wachezaji baadhi wasioanza kwenye 1st 11 ambalo ni kosa na dharau kwa mpizani. Makosa ya Mwenda yalikuwa mengi na asingefanya makosa yale mtu kama kapombe.

Suala la kumpa kocha muda mimi pia siliafiki. Yule tumeaminishwa ni kocha wa calibre ya CAF na mwenyewe anajinadi kwa kuwa na uzoefu wa kucheza derby nyingi anapaswa kudeliver. Mwenyewe umekiri sub alizofanya hazikuisaidia timu ni lazima tumlaumu kwa hilo. Kocha wa daraja kama yake anakoseaje kufanya sub!? Mbn Pablo game zake za kwanza kwanza alikuwa bora sana kwenye kufanya sub hakungoja apewe muda (msimu mzima). Pia nimesikia usajili wa bwana Dejan ni pendekezo la kocha hapa napo ni lzm alaumiwe mchezaji aliyemleta labda alikuwa ni mzuri huko ulaya kwa hapa kwetu anaweza kumaliza msimu mzima bila on target.
 
Kocha na mzungu wajiandae mwisho wa msimu
 

Attachments

  • Mra.jpg
    Mra.jpg
    20.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom