Haya ya kufanyiwa kazi haraka Simba SC kabla ya kuanza Ligi Kuu na michuano ya CAF

Haya ya kufanyiwa kazi haraka Simba SC kabla ya kuanza Ligi Kuu na michuano ya CAF

Acheni hizi imani zenu potofu, kama kweli walituibia mbinu mbona kipindi cha kwanza tulicheza Simba SC na goli tukapata?

Tujifunze kukubali matokeo, hata wakifanyia mazoezi mwezini ukizidiwa mbinu na mwenzako utapigwa tu.
unaona hadi topo topolo lime like jibu lako kwangu jiulize sana narudia jiulize sana, nani anaonaga mazoezi ya yanga? hujui kwamba kwa aliyehudhuria mazoezi ya simba siku mbili za mwisho kama ni mtaalamu alishajua kikosi kikoje?
leo na kesho kuna mazoezi na sababu ni ya wazi geita gold watakuwepo unadhani msoma mbinu mzuri hatajua kikosi kitakuwa kipi na kitachezaje?
Hivi mazoezi ya arsenal na man utd huwa yanahudhuriwa waziwazi hivyo?na hizo mbinu kuzidiwa haziwezi zikawa zimeonekana hukokwenye mazoeziya wazi?
 
Kuna kiungo gani pale wa kumfikia sadio kanoute box to box hunter na alivyotoka yeye kati kati palikuwa wazi maana alikuwa anafika katika kwenye hatari kabla yanga hawajaanzisha mashambulizi kawapoteza aucho sure boy na feisal first half sadio kanoute ndio midfielder bora simba kwa sasa sio lazima ukubali.
 
Kanoute alikuja vema mpaka kuna Uzi yeye na Sakho nikiwaelezea lakini sasa kuna kitu hakiko sawa upande wake, ana rafu ambazo si lazima kufanya.

Kwahivyo kwenye michezo kama hii ukimtoa Kanoute, mbadala (anayeingia) anatakiwa kuwa kama yeye au zaidi yake tutaendelea kujiuliza kwanini Akpan hakucheza ndo maana nikasema Kocha Zaron Maki alizidiwa mbinu ya Kocha Nabi.
 
Ghazwat mkuu mimi sikuwa na imani tangu kufukuzwa kwa yule mspain! yaan kisa kufungwa game 1 na uto tena akiwakosa kikosini key players kina mkude, chama, morison na kapombe. na bila kuangalia perfomance ya timu kwenye robo fainal dhidi ya timu yenye uwekezeji wa nguvu kwenye soka ya orlando pirates? kwa machungu mpaka mda huu nmejifungia ndani sina raha kwakweli! kumkosa ki aziz, adebayor, morlaze silla na manzoki naona viongozi hawathamini hisia zetu juu ya timu yetu! ukiangalia miaka 4 ya mafanikio yetu utopolo hatukuwatesa kwa vipigo vya kila mara kama wanavyotufanyia wao! MWANA KULITAKA MWANA KULITAFTA!
 
Kwa uchungu na hasira niliyonayo nimeamua kuchana na ushabiki wa moira..sijui ni hasira!!!!!
Anyway,kama nitapona maumivu haya nikarudi kwneye hali ya kawaida naweza nikarudi kuipenda Simba sc!!!!

Lakini kiukweli moyo wangu unavuja damu!!!!

Kiungo cha Kanoute na Mkude ni takataka!!!!
 
Hivi ilikuwaje tukamkosa herve ngomo?
 
Simba Ina matatizo makuu mawili.
1. Kamati ya usajili.
2. Tactics

1a.TATIZO la Simba sio DM
defensive midifilder.

TATIZO la Simba lipo kwenye kiungo wa kati wa UKABAJI. CDM.
Central defensive midifilder.
Aina ya Thadeo Lwanga,Mafisango Au Bangala,kidogo Kotei na Flaga.

1b. Kanute Akpan Mzamiru ni wakabaji wazuri Sana lakini sio CDM woteni 8. Box to box.
Mkude mkabaji mbovu Sana ni DM

2. KUSHINDWA KUMSAJILI MANZOKI NA KUSHINDWA KUMTUMIA MOSES PHILI.

NILIKUWA WA KWANZA KUANDIKA MZUNGU TUMEPIGWA.
 
Hivi ilikuwaje tukamkosa herve ngomo?
Kocha Zaron Maki alimuhitaji zaidi Mohamed Ouattara kuliko Herve Ngomo ambapo kamati ya usajili walimtaka.

Lakini rejea kwenye Uzi, hakuna beki bora kama hakuna Defensive Midfielder
 
Fraga na Lwanga kazi yao moja tu, ni kukaba na kuharibu mashambulizi, Mkude si Defensive Midfielder ni Holding Midfielder.
Mkude so kiungo mkabaji defensive middfilder sio CDM Wala attacking Wala box to box, Wala holding.

Yeye ni midifilder kiungo tu.
Uwezo wake ni kupiga pass ndefu.
Madhara.

kucheza sehemu ndogo....
KUSHINDWA kukaba......
KUSHINDWA kulinda back four.
KUSHINDWA kunusa hatari nk nk nk.

Mkude ni kiungo zaifu sana
 
Kwa uchungu na hasira niliyonayo nimeamua kuchana na ushabiki wa moira..sijui ni hasira!!!!!
Anyway,kama nitapona maumivu haya nikarudi kwneye hali ya kawaida naweza nikarudi kuipenda Simba sc!!!!

Lakini kiukweli moyo wangu unavuja damu!!!!

Kiungo cha Kanoute na Mkude ni takataka!!!!
Kwenye game ya michuano ya Azam Sports Federation Cup Jijini Mwanza

Simba waliacha space kubwa sana kati Beki na Viungo kiasi kwamba Feisal alidrible mpira kama mara tatu akiwa free kisha akaachia fataki na hakutokea Kiungo kumkaba wala kuharibu mashambulizi.

Tukisema tunahitaji Kiungo Defensive Midfielder tumeangalia panavuja.
 
Ule uamuzi wa kumfukuza uchebe kwangu bado naona ndio chanzo cha haya majanga yote yanayotukuta kwa sasa.

Kila mara kubadilisha makocha kabla hawajatengeneza timu, matokeo yake ndio haya ni vipigo mfululizo toka kwa wale tuliokuwa tumewaweka mfuko wa nyuma enzi za uchebe.
Binafsi siioni kama simba ni mbovu kufungwa ni hali ya mchezo, ila uchebe angekuwepo hadi leo simba ingekuwa yamoto sana
 
Binafsi siioni kama simba ni mbovu kufungwa ni hali ya mchezo, ila uchebe angekuwepo hadi leo simba ingekuwa yamoto sana
Lazima tukubali matokeo ya aina tatu uwanjani, lakini kama haturekebishi mapungufu niliyanayotaja hapo yamkini Kauli hii We Are Unstoppable haiwezi kufua dafu.
 
Lazima tukubali matokeo ya aina tatu uwanjani, lakini kama haturekebishi mapungufu niliyanayotaja hapo yamkini Kauli hii We Are Unstoppable haiwezi kufua dafu.
Ukweli kila mwanasimba ameumia kufungwa na hasa kufungwa na yanga, lakini bado naamini simba hii ni bora na itafanya makubwa mno
 
Ukweli kila mwanasimba ameumia kufungwa na hasa kufungwa na yanga, lakini bado naamini simba hii ni bora na itafanya makubwa mno
Kwa msimu huu viongozi wa Simba SC wamejitahidi sana usajili, licha ya kumkosa Adebayor na Lobi Manzoki

Kocha Zaron anaweza kuchagua Kikosi chake cha ushindi na kuacha kujaribu Wachezaji na Sub yake ambayo imegharimu timu, nina imani Simba itakuwa moto sana na hasa wakipata Defensive Midfielder, aanze sasa kusoma mbinu za wapinzani wake na hizi Derby namna ya kupambana nazo.

Lengo ni kufanya vizuri Ligi na michuano CAF, hawa Yanga wameshtua nini la kufanya kwa msimu ujao.
 
Kipindi cha Kwanza Yanga walikuwa tumewakamata, Kitendo cha kumtoa mbunifu wa pasi za Magoli yaani Chama na Mkabaji asiyepewa heshima yaani Kanoute ili mkosti Kocha, nafikiri suala la Kocha msaidizi lifikiliwe upya ikiwezekana aondolewe kama tulivyofanya kwa Djuma basi Matola naye amshe tu.
 
Hivi kazi ya Matola pale Simba ni nini????????????????????????????
 
Back
Top Bottom