Haya yakifanyika uhalifu utaisha, panya road watakwisha na raia watakuwa wanalala milango wazi hadi asubuhi

Operation Kama hii ishawahi kufanyika miaka kadhaa huku kwetu mkoani (nafikiri ni miaka karibu kumi hv). Wakati huo kulikuwa na Kijiji jirani ambacho kilijaa wahuni, wezi na wababe ilikuwa mkicheza nao mpira mkiwafunga kichapo kinawahusu hata wakishinda bado wataanzisha vurugu ilimradi tu kuonesha ubabe, mtu ukienda na usafiri wako huko(baiskeli wkt huo) jamaa wanapita nayo. Sasa ilifikia hatua raia walichoka na vurugu zao wakaandaa mkakati wa kumsaka mmojammoja popote walipo dah walipukutishwa wote nakumbuka mmoja tulisoma nae jamaa aliuliwa kikatili Sana na wanakijiji na ndo alikuwa mwizi konki alikimbizwa na kundi la raia akakimbilia mtoni alifuatwa hukohuko akapigwa ndani ya maji mpaka akafa.
Nowdays full amani
 
Serikali ituachie tu tuwaue hawa watu kwa sababu wao wameshindwa kulinda amani ya raia wake
Inashangaza kuona serikali mpaka leo imeshindwa kuirudisha OPARATION MREMA. Afu wa halifu wa leo sio kama wa miaka ile. Enzi zile wahuni wengi walikuwa wanacheza ngumi, karate nk. Pia walikuwa na miili iliyoshiba, mtu anakula kilo ya unga na fungu la samaki, afu hawakuwa na masihara hata kidogo, lkn serikali ilipoamua iliwamaliza. Leo hii panya road umri ni 14, 15 hadi 18. Hawana nguvu za mwili wala za mapambano ya kiakili, unakuta panya road anashindia mihogo miwili kwa siku, afu eti wanatingisha mji mzima huku serikali ikiwaangalia tu.
 
Asante mkuu kwa kutuelewesha kilichotokea huko kwenu. Ki ukweli wananchi sasa hivi wanatakiwa waombe OPARATION MREMA irudishwe, bila hivyo raia wataangamia.
 
Mtu yeyeto mbabe sijui muhalifu, sijui kachanjia chuma kisiingie kuanzia bunduki, panga, kisu, nk Ili atese jamii kwa uhalifu, ubabe, nk. Dawa yao huwa ni acid, acid huwa aiongopi. Yeye kachanjiwa chuma kisiingie mwilini na sio acid,fizia usiku mwagia usoni machoni acheze nayo.
 
Nimeguswa!. Very touching story.
Sijapenda jinsi starring alivyo uwawa bila kosa lolote!.
Wale wote walio husika kumuua kamanda huyu bila kosa lolote, karma inawahusu.

RIP Kuveta, Kamanda wa Commando Yosso.
 P
Vp na wale waliouwawa au kujeruhiwa na huyo sijui kuveta, ni vigezo gani umetumia kusema Hana hatia.
Ukikuta watu waliojeruhiwa na Hawa watu ndio utajua sio binadamu ni wanyama, Wacha wale haki yao
 
Huyu ndo mwanzilishi wa komando yosso siku hizi ni mtumishi wa Mungu, na ndie aliyepiga tukio la kiwanda cha sukari moshi wakaua Muhasibu wa kiwanda wakapora milioni 600,wakatoroka wenzake walikuja kuuwa njiapanda ya himo na police.
Mrema akiwa Waziri mambo ya ndani akatoa ultimatum kwamba wasambaratishe kundi nao wakampiga mkwara Mrema wakamwambia kwamba wao ndio yosso, ikapigwa operation safisha jiji huku raia huku police wakala bullets za kutosha wakasambaratika.Bunduki ndio njia pekee ya kumaliza wahalifu kwenye Jamii na siyo mahakama.

 
Umejuaje alibadilika au unahisi, Kila mtu atakula haki yake km anavyostahili na alivyopangiwa.
 
Kabisa mkuu Hawa jamaa wa mapindi hayo unakuta linabeba vyuma, walikuwa wanaogopeka mtaani mtu anaibiwa unaona kabisa ila unakausha husemi.
Hivi vya sasa hivi vitoto kabisa tunavilealea yaani ukifanikiwa kukakaba kamoja kwenye angle unakaua kabisa
 
Vp na wale waliouwawa au kujeruhiwa na huyo sijui kuveta, ni vigezo gani umetumia kusema Hana hatia.
Ukikuta watu waliojeruhiwa na Hawa watu ndio utajua sio binadamu ni wanyama, Wacha wale haki yao
Hao watu inatakiwa kurudishwa kuzimu walipotoka
 
Mkuu huyu mbona ukifuatilia maelezo yake mengi, anaonekana ni msaka fursa tu wa sadaka kupitia kanisa. Kwa wakongwe tuliozaliwa na kuishi Dar miaka hiyo hasa maeneo ya mburahati, mabibo, kigogo manzese hatukuwahi kuumfahamu huyu mwamba, labda kutokana na umri pengine muonekano wake umebadilika sawa. Lakini Commando Yosso asili yake ni maeneo hayo niliyoyataja na huyo Kuveta ninaekwambia hakuna mtu wa miaka hayo na maeneo hayo ambae alikuwa hamjui. Nakwambia mpaka jamaa wa bongo movie nasikia walicheza cinema kuhusu maisha ya mtemi huyo, japo wachezaji wa bongo movie hao inasemekana waliweka chumvi nyingi kama kawaida yao. Laiti nikibahatika kuipata hivyo movie nitaiweka hapa, japo na yenyew haizungumzii maisha yake halisi kutokana na kujaza machumvi mengine movini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…