wa kupuliza
JF-Expert Member
- Jun 15, 2012
- 15,216
- 37,757
Kagame alitumia hio style,Sasa hivi Rwanda watu wanalala milango wazi,matukio Ni ya kuhesabu.Naunga mkono hoja ,dawa ya hao WEHU ni kupiga vyuma mmoja mmoja mpaka wanaisha.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kagame alitumia hio style,Sasa hivi Rwanda watu wanalala milango wazi,matukio Ni ya kuhesabu.Naunga mkono hoja ,dawa ya hao WEHU ni kupiga vyuma mmoja mmoja mpaka wanaisha.
Operation Kama hii ishawahi kufanyika miaka kadhaa huku kwetu mkoani (nafikiri ni miaka karibu kumi hv). Wakati huo kulikuwa na Kijiji jirani ambacho kilijaa wahuni, wezi na wababe ilikuwa mkicheza nao mpira mkiwafunga kichapo kinawahusu hata wakishinda bado wataanzisha vurugu ilimradi tu kuonesha ubabe, mtu ukienda na usafiri wako huko(baiskeli wkt huo) jamaa wanapita nayo. Sasa ilifikia hatua raia walichoka na vurugu zao wakaandaa mkakati wa kumsaka mmojammoja popote walipo dah walipukutishwa wote nakumbuka mmoja tulisoma nae jamaa aliuliwa kikatili Sana na wanakijiji na ndo alikuwa mwizi konki alikimbizwa na kundi la raia akakimbilia mtoni alifuatwa hukohuko akapigwa ndani ya maji mpaka akafa.Habari zenu ndugu zangu. Baada ya salam, ningependa niende kwenye mada husika kwa kutumia mifano hai iliyopita.
Katika historia ya nchi yetu toka tapate uhuru mpaka leo, hakuna kipindi kilichokuwa na changamoto za kiusalama kama kipindi cha miaka ya 1989 hadi 1993. Hiki ndio kipindi ambacho nchi ilishuhudia vikundi mbali mbali vya kihalifu kama vile COMANDO YOSSO, RED SOLDIER (red sonja) SIAFU FAMILY, WATOTO WA SHETANI nk.
Kati ya hayo makundi mimi nililijua zaidi kundi la "COMMANDO YOSSO" hili kundi lilikuwa ni kundi hatari kati ya makundi yote yaliokuwepo wakati huo. Kundi hili lilianzishwa na lilikuwa na masikani yake huko Mburahati, ambapo vijana wa kundi hilo walikuwa ni wenyeji wa maeneo hayo ya Mburahati, Kigogo, Mabibo, Manzese, na baadhi ya vijana kutoka maeneo ya Tandale na Kagera mikoroshini pia walikuwemo. Kiongozi mkuu wa kundi hilo alikuwa ni baba yangu mdogo kwa jina alikuwa anaitwa Kuveta R.I.P. Bila shaka wazee, vijana, na watu mbali mbali wa maeneo hayo miaka hiyo walikuwa wanamfahamu aidha kwa kumuona au kumsikia.
Baba yangu mdogo huyo hakuwa katili kivile, ila ukiingia kwenye 18 zake hauwezi kubaki salama. Kwenye 18 zake yeye hakujali wewe ni askari, muhuni mwenzake au nani. Mara nyingi alikuwa na machale kiasi kwamba akikaa maskani akiwaambia tuondokeni basi watakaopuuza baada ya dakika mbili jela itawahusu, japo sometimes na yeye polisi walikuwa wanamuotea, pia alijaaliwa uwezo wa kupambana na adui yeyote.
Alikuwa kaenda hewani, mwili jumba hasa kwa upande wa kifua na mikono, miguu iliyo imarika. Utotoni alijifunza michezo hatari ya ngumi na karate maeneo mbali mbali, swala la kuvunja tofali kwa ngumi au kichwa lilikuwa la kawaida kwake. Kwahiyo alikuwa fit na aliogopeka kweli kweli, maana hata kukamatwa kwake, alikuwa anamatwa na lundo la askari tena wenye silaha za moto.
Hakuna jela ya Tanzania ambayo hakuwahi kufungwa, na kote alipokwenda wababe mkwara walimpa heshima yake, na alikuwa mpaka na tandiko lake. Nasikia kuna bongo movie washawahi kucheza sinema yake (japo sijaiona kutokana na kuishi nje ya Tz muda mrefu).
Tukiachana na yeye pia kulikuwa na baadhi ya watemi wengine wa chini yake kina Domokeka, Kaboka mchizi, Chura dume, na wengine wengi wa makundi hayo ambao nimewasahau majina yao. Pia kulikuwa na vikundi vya michiriku ambavyo navyo vilikuwa vikifuga wahuni mbali mbali jijini. Yani hicho ndio kilikuwa kipindi hatari kwa utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi usiokuwa na kipimo, wizi wa usiku na mchana kweupe.
Ilifikia kipindi kukiwa na mnanda karibu yenu basi msicheze mbali na milango au madirisha yenu, au kundi la wahuni linaweza kumteka mwanamk mbele ya mumewe likaenda kufanya mambo yao na wakimaliza wanamuacha arudi kwao nk.
Watu walikatwa mapanga hovyo bila sababu, makundi haya yalimiliki silaha za moto, na za jadi kama vile bunduki, mapanga, shoka nk. Yani hicho ndio kilikuwa kipindi kibaya cha umwagaji damu jijini Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla. Raisi Mwinyi alipoona hali ya usalama nchini inazidi kuwa mbaya ikabidi amteuwe mh Augustino .L. Mrema kuwa waziri wa mambo ya ndani.
Mrema alipoteuliwa akaapa kuyatokomeza makundi hayo kwa kuandaa oparation maalumu ya polisi, wakishirikiana na sungu sungu ambao yeye (Mrema) ndo muasisi. Basi bwana shughuli ikaanza huku Mrema mwenyew akiwa mstari wa mbele katika oparation ile.
Kwa vile serikali ilishirikisha sungu sungu ambao ni wananchi wa maeneo mbali mbali ya jiji, basi ilikuwa rahisi kuwatambua kimya kimya wahusika wa makundi yale pamoja na wahalifu wengine. Ikawa wakijua nyumba fulani kuna kijana muhalifu wazee wa kazi askari wakishirikiana na sungu sungu wanakuja usiku wanagonga mlango askari wanaingia, wanamchomoa waliemfuata wanaondoka nae. Kama wewe ni mzazi au ndugu, basi asubuhi utaletea taarifa na mjumbe kuwa uende sehemu fulani ukachukue mzoga wako uuzike.
Oparation hii haikushia kwenye nyumba tu bali mpaka kwenye maskani zao walifuatwa na kuangamizwa huko huko. Nakumbuka bamdogo Kuveta aliuwawa siku ya tatu tu akiwa ametoka jela. Akiwa ameenda kulala kwa demu wake, siku hiyo ghafla usiku walivamiwa na kundi la watu zaidi ya 50 wakiwemo askari wenye silaha na sungu sungu wenye mapanga na kuanza kumshambulia.
Maiti yake tulikuta ikiwa na majeraha makubwa kwenye maungio ya mikono yake, kifuani na kichwani. Tulipomuuliza demu wake akasema alipata yale majeraha ya mikononi baada ya kupambana na askari mwenye silaha, ambapo sungu sungu waliona angefanikiwa kumpokonya askari ile bunduki basi ingekuwa hatari kwa uhai wao, so suluhisho likawa ni kuikata mikono yake kwa mapanga japo hiyo haikumfanya aache kupambana, ndipo wakaamia kichwani na kifuani so kutokana na kuvuja sana kwa damu akaishiwa nguvu akaanguka na kufariki.
Pia yule demu wake walimjeruhi baadhi ya sehemu za mwili wake, ila hawakumuua. Baada ya mauaji hayo ya wahalifu mbali mbali, wizi ukapungua kama sio ukaisha kbs jijini Dar es salaam. Vikundi vya michiriko (minanda) navyo vikaanza kusambaratika, amani ikarejea.
Watu wakaanza kuishi kama Saudia Arabia ambapo mida ya sala inafika, watu wanaenda kusali huku wakiwa wameacha biashara zao wazi kabisa. Sasa inashangaza sasa hivi vipanya road vyenye umri wa miaka 14, 15 hadi 18 vinafunga mtaa wa wanaume wenye umri mkubwa na kuchukua kila kitu ndani ya majumba yao.
Kwanini ile oparation maalumu ya Mrema isirudie kuwamaliza mbwa hao. Au polisi kwanini wasishirikane na wananchi (sungu sungu) kwa style ile ile waliyotumia wenzao kumaliza ushenzi huo unaoendelea kwa kasi jijini na nchini kwa ujumla?
Inashangaza kuona serikali mpaka leo imeshindwa kuirudisha OPARATION MREMA. Afu wa halifu wa leo sio kama wa miaka ile. Enzi zile wahuni wengi walikuwa wanacheza ngumi, karate nk. Pia walikuwa na miili iliyoshiba, mtu anakula kilo ya unga na fungu la samaki, afu hawakuwa na masihara hata kidogo, lkn serikali ilipoamua iliwamaliza. Leo hii panya road umri ni 14, 15 hadi 18. Hawana nguvu za mwili wala za mapambano ya kiakili, unakuta panya road anashindia mihogo miwili kwa siku, afu eti wanatingisha mji mzima huku serikali ikiwaangalia tu.Serikali ituachie tu tuwaue hawa watu kwa sababu wao wameshindwa kulinda amani ya raia wake
Ya hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kuwauwa tu ili kumaliza uhalifu nchini.Si alikuwa kiongozi wa kikundi cha uharifu?
😂😂😂🤣🤣 Dah umenivunja mbavu mkuu wangu.ila kimsingi inafikia kipindi kumuacha mshenzi aishi ni gharama kuliko kumu eliminate.
😂😂🤣🤣🤣Fxck you kalinde kaburi
Hahaha 🤣🤣🤣 huo msemo wako umeniacha hoi mkuu.Kutoka jela hakumaniishi aliacha ujambazi! Tena awamu hizo "ililikuwa tabu sana kutofautisha rushwa na takirima"
Usicheke mkuu kuna watu wanakera ingekuwa tunaruhusiwa kumiliki bastola kama ilivyo kwa magari sahizi wengi tungekuwa tumeshawazika😂😂😂🤣🤣 Dah umenivunja mbavu mkuu wangu.
Bila OPARATION MREMA hakuna uhalifu utakaoisha jijini.Naunga mkono hoja ,dawa ya hao WEHU ni kupiga vyuma mmoja mmoja mpaka wanaisha.
Asante mkuu kwa kutuelewesha kilichotokea huko kwenu. Ki ukweli wananchi sasa hivi wanatakiwa waombe OPARATION MREMA irudishwe, bila hivyo raia wataangamia.Operation Kama hii ishawahi kufanyika miaka kadhaa huku kwetu mkoani (nafikiri ni miaka karibu kumi hv). Wakati huo kulikuwa na Kijiji jirani ambacho kilijaa wahuni, wezi na wababe ilikuwa mkicheza nao mpira mkiwafunga kichapo kinawahusu hata wakishinda bado wataanzisha vurugu ilimradi tu kuonesha ubabe, mtu ukienda na usafiri wako huko(baiskeli wkt huo) jamaa wanapita nayo. Sasa ilifikia hatua raia walichoka na vurugu zao wakaandaa mkakati wa kumsaka mmojammoja popote walipo dah walipukutishwa wote nakumbuka mmoja tulisoma nae jamaa aliuliwa kikatili Sana na wanakijiji na ndo alikuwa mwizi konki alikimbizwa na kundi la raia akakimbilia mtoni alifuatwa hukohuko akapigwa ndani ya maji mpaka akafa.
Nowdays full amani
😂😂🤣🤣🤣Usicheke mkuu kuna watu wanakera ingekuwa tunaruhusiwa kumiliki bastola kama ilivyo kwa magari sahizi wengi tungekuwa tumeshawazika
Vp na wale waliouwawa au kujeruhiwa na huyo sijui kuveta, ni vigezo gani umetumia kusema Hana hatia.Nimeguswa!. Very touching story.
Sijapenda jinsi starring alivyo uwawa bila kosa lolote!.
Wale wote walio husika kumuua kamanda huyu bila kosa lolote, karma inawahusu.
RIP Kuveta, Kamanda wa Commando Yosso.
P
HahahahaKagame alitumia hio style,Sasa hivi Rwanda watu wanalala milango wazi,matukio Ni ya kuhesabu.
Umejuaje alibadilika au unahisi, Kila mtu atakula haki yake km anavyostahili na alivyopangiwa.People changes, maadam alitoka jela na hakufanya uhalifu wowote, then, there is no any justified cause ya kumuua!.
Na kwa tukio hili lilitokea siku nyingi, wahisika wote kila mmoja ameisha lipwa na karma, kwa kadri ushiriki wake katika dhambi ya mauaji ya mtu asiye na hatia.
P
Kabisa mkuu Hawa jamaa wa mapindi hayo unakuta linabeba vyuma, walikuwa wanaogopeka mtaani mtu anaibiwa unaona kabisa ila unakausha husemi.Inashangaza kuona serikali mpaka leo imeshindwa kuirudisha OPARATION MREMA. Afu wa halifu wa leo sio kama wa miaka ile. Enzi zile wahuni wengi walikuwa wanacheza ngumi, karate nk. Pia walikuwa na miili iliyoshiba, mtu anakula kilo ya unga na fungu la samaki, afu hawakuwa na masihara hata kidogo, lkn serikali ilipoamua iliwamaliza. Leo hii panya road umri ni 14, 15 hadi 18. Hawana nguvu za mwili wala za mapambano ya kiakili, unakuta panya road anashindia mihogo miwili kwa siku, afu eti wanatingisha mji mzima huku serikali ikiwaangalia tu.
Hao watu inatakiwa kurudishwa kuzimu walipotokaVp na wale waliouwawa au kujeruhiwa na huyo sijui kuveta, ni vigezo gani umetumia kusema Hana hatia.
Ukikuta watu waliojeruhiwa na Hawa watu ndio utajua sio binadamu ni wanyama, Wacha wale haki yao
Huyu ndo mwanzilishi wa komando yosso siku hizi ni mtumishi wa Mungu, na ndie aliyepiga tukio la kiwanda cha sukari moshi wakaua Muhasibu wa kiwanda wakapora milioni 600,wakatoroka wenzake walikuja kuuwa njiapanda ya himo na police.
Mrema akiwa Waziri mambo ya ndani akatoa ultimatum kwamba wasambaratishe kundi nao wakampiga mkwara Mrema wakamwambia kwamba wao ndio yosso, ikapigwa operation safisha jiji huku raia huku police wakala bullets za kutosha wakasambaratika.Bunduki ndio njia pekee ya kumaliza wahalifu kwenye Jamii na siyo mahakama.